Ni kweli mikataba haijawahi kuwa wazi Tz na ndo maana watu wanalia. Ni kwamba wanaona ingekuwa wazi nao wangechangia mawazo. Lkn kuna ukweli gani hapo?Ni lini mikataba ilikua wazi Tanzania? Kuanzia wa SGR mpaka Ya Gesi ila kuna aliewahi kuhoji? Kipindi Tanzania inajitoa OGI mbona hamkupinga mlikaa kimya ila leo ndio mnahoji mikataba iwekwe wazi kwa sheria ipi? Hamkujua OGI ndio ilibana serikali kuweka wazi mikataba yote public?
Je, kwa mfano, mikataba hiyo iwekwe mitandaoni km. JF!!? Kweli?Ingetekelezeka? Tungeonekana watu wa aina gani? Kuna kitu kama hicho duniani!?
Nafikiri wanaoingia/fanya majadliano wanafanya maksudi kwa manufaa binafsi huku wakiingiza maufisadi yao humo. Kiasi kwamba value for money haina nafasi. Wala dawa sio uwazi huo tunaoufikiria. Nionavyo mimi ni kuwa na wahusika muafaka wenye uzalendo wafanyao kazi "professionaly", wakiweka kando matumbo yao na kujikomba kwao kwa mwajiri. Lkn kutamani ni jambo moja, kupata ni jingine.
Katika nchi ambapo wanasiasa wanaona kusifiwa na kutukuzwa ndo dili, watasifiwa saaana, watatukuzwa pia. Na kwa kuwa vitendo hivyo vinalipa, yatachaguliwa maimba mapambio kutuingiza katika mikataba bomu na nyimbo nyingi kuhusu maendeleo zitatungwa na zimeshatungwa tayari - tutazisikia Des. 9, 2021.
Dawa ni katiba mpya, maviongozi bomu yatupiliwe mbali. Nje ya hapo tutaendelea kulazimishwa kuchangia madawati huku tukinyang'anywa kidogo (kuku?, mbuzi?) tulichonacho kwa kisingizio cha kugoma "kuchangia" maendeleo. Haya yanapatikana Tz tu, kuku inachangia maendeleo na kodi inamlipia mwanasiasa maendeleo ...duh! WaTz tumemkosea nini Mungu!?