Kipilipili
JF-Expert Member
- May 25, 2010
- 2,272
- 1,880
- Thread starter
- #381
Kuhusu bidhaa zinazolipa, naweza kusema bidhaa yoyote inalipa ISIPOKUWA inategemea tu na soko lako ulilolikusudia likoje huku nyumbani Tanzania.Mkuu heshima kwako kwa kushea uzoefu wako, big up. Nilitaka kupata mtazamo wako wa uzoefu wa bidhaa zinazolipa kutoka huko uchina kwa mtu ambaye anaanza (beginner) na kwa mtaji mdogo say 10m, mfano bidhaa kama handbag za akina dada? Waonaje?. Nimesikia pia ukinunua bidhaa huko china unawapa wauzaji adress ya kampuni ya usafiri (eg silent ocean) kisha wao wanapeleka kwa wasafirishaji, unalipia (usafirishaji)ukishachukua bongo. Je hii ndio tratatibu? Na pia huwa nasikia pia bangkok, vp huko kuna bidhaa nzuri pia? Ushauri wowote kwa beginner asie na uzoefu wowote
Cha muhimu ANZIA SOKONI ndio uende kiwandani. Hakikisha unajua soko linataka nini kwa muda husika.
Kwa hali ya sasa ya kiuchumi Tanzania, sishauri sana (mtazamo wangu) kwa anaeanza biashara aingie kwenye bidhaa za fasheni na urembo kama nguo na mikoba au viatu.
Kwa sasa "purchasing power" ya watanzania wengi imeshuka kwenye bidhaa za nguo, viatu na mikoba.
Mabadiliko ya kiuchumi, watu wengi wameanza kujiongeza na kufikiria kuwekeza kwenye ujasiriamali mdogo mdogo.
Kwa hiyo kwa sasa ukiuza bidhaa ambayo itatatua changamoto za watu basi utakuwa umejihakikishia soko lako. Kwa mfano: sasa hivi wajasiriamali wadogo wamejikita katika kilimo, ufugaju na usindikaji. Pia wamejikita katika kuongeza thamani ya bidhaa ambazo zimeshazalishwa. Kwa hiyo ukija na bidhaa mfano packaging materials utauza sana kwa sababu hiyo ni moja ya changamoto ya wajasiriamali wengi hawana parking materials kwa ajili ya bidhaa zao. Kwa hiyo utakuwa umetatua matatatizo ya wengi na unaweza ukawa general supplier mikoani (usifocus DSM tu, angalia pia mikaoni).
Bidhaa za nguo na fasheni watu wamepunguza kuvaa "vyuma vimekaza" unless labda utumie mbinu ya kukopesha ambayo nayo ni risk sana na mtaji unaweza ukazama huku unajiona!
Kingine kuhusu bidhaa za nguo na mikoba ni kuwa biashara hiyo inaendeshwa kwa nguvu ya fashion iliyopo, hivyo unaweza kununua mzigo china, mpaka unafika TZ (Kama ni meli umetumia siku 45 hivi) unaweza kukuta nguo au mikoba uliyoleta iloshaingia kariakoo kitambo (wakati mzigo wako ukiwa majini) na bei haipo kama ulivyotarajia, mwisho wa siku unajikuta unauza kwa hasara.
Pia ni muhimu kujikita kwenye biashara ambayo ushindani wake si mkubwa . Biashara ya nguo na mikoba ipo kila baada ya nyumba kadhaa. Kuna maduka ya madera, viatu kila kona! Shangwe za kuvaa siku hizi sio kiviiiileeee...hali si hali.
Biashara ya nguo na viatu ukiwa wewe ndio unaanza itakulazimu ushushe bei uweke "penetrating price" ili uweze kuingia sokoni vizuri mana tayari sokoni kuna wenzio ambao wapo kitambo, unless wewe uje na kitu cha kipekee sana.
Kuhusu usafirishaji, hiyo ni moja ya taratibu lakini binafsi nashauri uwe na mtu kule ambaye atasimama katikati yako na muuzaji ili kuondoa risk mana wachina nao si wote wa kuwaamini. Kuwa na mtu alieko kule yeye akague bidhaa kiwandani, kisha malipo fanya mwenyewe kwenye akaunti ya muuzaji (ambayo iko secured na incase of anything unaweza kuclaim refund na hela yako ikarudi mf. kupitia paypal/alibaba trade assurance nk nk) kisha mzigo ukifika kwenye Ghala la wasafirishaji basi huyo mtu wako aende akaukague na ajiridhishe kuwa ndio ule ule alioukagua kiwandani)
Kuhusu Bankok sina uzoefu napo. wenye uzoefu na huko wataongezea.
NB: Ni maoni yangu tu na yanaweza yasiwe mujarab kwa wengine