CHINA DASHENG BANK (CDBL), Benki mpya inayotishia soko.

Jun 25, 2019
15
45
Taarifa za fedha za mabenki kwa robo ya tatu ya mwaka 2019 zimetolewa kuanzia mwezi wa tisa mwishoni na mwezi wa kumi katika vyombo mbalimbali vya habari hasa magazeti kama ambavyo kanuni ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2014 inaelekeza. Kiujumla kumekuwa na kupanda kwa faida kwa mabenki mengi hasa makubwa yakiongozwa na CRDB na NMB.

Upepo wa mafanikio katika sekta ya kifedha haukuiacha benki changa ya China Dasheng tofauti na benki ya Guaranty Trust (GT Bank) ambapo zote zilianzishwa mwaka 2018 katika soko la Tanzania. Benki ya China Dasheng iliingia rasmi katika soko la Tanzania tarehe 26 mwezi novemba mwaka 2018 ikiwa na mtaji wa kiasi cha shilling billioni za kitanzania 100 mara sita Zaidi ya kiasi kinachohitajika na benki kuu ya Tanzania ambacho ni shilling za kitanzania billioni 15 tu.

China Dasheng, iliyoanzishwa na makampuni sita ya umma na binafsi kutoka majiji ya Shangai na Jiangsu katika ukanda wa delta ya mto Yangtze, ilifanikiwa kupata faida katika robo zote tatu za mwaka 2019 kama ifuatavyo; robo ya kwanza shilling za kitanzania billioni 1.05, robo ya pili shillingi za kitanzania millioni 229 na shilling za kitanzania million 174 katika robo ya tatu. Kwa upande wa benki nyingine ngeni katika soko, Guaranty Trust Bank hali haikuwa shwari, hasara mfululizo katika robo zote tatu ilipatikana kama ifuatavyo; shillingi za kitanzania billioni 1.01, millioni 744 na millioni 827 katika robo ya kwanza, pili na tatu mtawalia.

Pengine matokea hayo ya faida katika benki hizi mbili yanatokana na utofauti wa mali zinazomilikiwa na mabenki husika, Nyaraza za mizania katika taarifa za fedha za robo tatu zinaonyesha benki hizi zinamiliki mali za kiasi cha shillingi za kitanzania billioni 30.3, 32.9 na 31.1 kwa Guaranty Trust Bank na 90.5, 106.3 na 105.1 kwa China Dasheng Bank mtawalia.

Licha ya uchanga wake katika soko la Tanzania, China Dasheng Bank imeng’aa mbele ya benki kongwe nyingi zilizovuna hasara katika robo tatu zote za mwaka 2019. Mfano wa benki zilizovuna hasara katika robo zote tatu ni NIC (billioni 3.19, 2.32 na 2.99), UBL (billion 1.10, million 60 na billion 1.99), FNB (billioni 1.33, 5.99 na 2.71), FHB (millioni 531, 259 na 85) na Eco Bank (billioni 1.64,millioni 358 na millioni 452).

Vipimo vingine vya ufanisi katika taarifa ya mapato na matumizi ya benki ya China Dasheng Bank kwa robo inayoishia septemba 30, 2019 ni kama ifuatavyo; uwiano wa gharama zisizo riba na faida ghafi ulifikia asilimia 86.7% wakati uwiano wa mapato halisi ya riba na wastani wa mali zinazozalisha ulifika asilimia 1.0%.

Benki ya China Dasheng yenye wafanyakazi 24 katika tawi moja, imekuwa na uwiano mzuri wa idadi ya wafanyakazi na faida; yaani millioni 60 kwa kila mfanyakazi. Kwa kutegemea na mtawanyiko wa wateja wake, benki hii inaweza kuongeza idadi ya matawi mpaka kufikia mawili na bado ikawa na uwiano mzuri wa idadi ya wafanyakazi na faida kuliko benki ya CRDB na NMB yenye uwiano wa 26.9 na 23.6 mtawalia.Mwandishi wa Makala hii ni mwanafunzi wa shahada ya pili ya Usimamizi wa Mashirika, Mhasibu aliyeidhinishwa(CPA), Mhitimu wa Shahada ya Uchumi na fedha na ni mwajiriwa wa Benki.
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
9,341
2,000
wasambaze matawi waweke riba ndogo ambazo hazikinzani na sheria za b.o.t kisha waone watkvyo kimbiza mwenge
 

Nedago

JF-Expert Member
Sep 26, 2018
889
1,000
Duh hizo hela nilikuwa nazisoma hadi jasho linanitoka,
Hao mabeberu warudishe hela zetu,

Wakajipeleke kwa dpp na kuomba msamaha siku ya jumanne
Au sivyo wafungwe jera.

son of almighty God.
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,457
2,000
wasambaze matawi waweke riba ndogo ambazo hazikinzani na sheria za b.o.t kisha waone watkvyo kimbiza mwenge
Hii ni tafsiri yangu inaweza isiwe kweli!!

Nadhani hiyo benki ya China Dasheng mafanikio yake yanaletwa na uasili (Nature) wa benki hiyo. Hiyo Benki ni ya wachina waliojiunga kuja kuwekeza Tanzania. Swali la msingi kwa nini walikuja kuwekeza Tanzania.

Kimsingi wachina waliiona fursa ambayo mabenki ya Tanzania waliipuuzia. Mabenki ya Tanzania hawakuitafakari fursa ya kuwekeza kwenye biashara iliyokuwa inakuwa kati ya Tanzania na China.

Fikiria china ina makampuni mangapi ya Kichina yanayofanya kazi za Ukandarasi hapa Tanzania na ni biashara ya shilingi ngapi inafanyika kati ya Tanzania na China. Hapo ndipo unapoona ni kwa nini benki hiyo ya China Dasheng inafanikiwa kibiashara.

Hebu fikiria Mtanzania anataka kununua au kuuza bidhaa china na kuwe na benki inayomrahisishia mtanzania huyo kulipa ama kulipwa fedha zake,unadhani si ataona amerahisishiwa ufanyaji wake biashara?

Jee Kampuni za Kichina zinazofanya kazi hapa Tanzania kati ya kwenda kukopa kwenye mabenki ya Tanzania na hiyo ya kichina watachagua ipi kama siyo China Deshang?
 

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
8,989
2,000
Umetuletea ripot nzuuri sana mkuu. GT Bank ni wahuni hasa yule Mkurugenzi wao Mnigeria. Ana wa treat vibaya sana wafanyakazi kiasi kwamba sishangazwi na kufanya kwake vibaya kwenye lota tatu za mwaka 2019
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom