China anatafutwa na nchi nyingi tu sio Marekani pekee, akiingia mtegoni ameisha

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
593
2,037
Yaani kwa mtu asiyejua maswala ya biashara namna mchina alivyokuwa mafia ndio anaweza kumtetea, ila mchina sio mtu mzuri kabisa linapokuja swala la uharamia wa biashara ya mtu.

Wazungu wamekaa zaidi ya miaka 100 wakitengeneza brand zao kwa shida kama LV, FENDI ,TIMBERLAND ,CLARKS, GIORGIOARMANI, GUCCI , HISENSE, SONNY, PHILIPS , CHANNEL , CAT , NIKE ,PUMA, halafu anatokea mchina anakuzia bidhaa ya yenye chapa Ya Gucci sh 5,000.

Yaani ni kwamba anaharibu brand za watu kwa kutoa bidhaa feki, mwisho wa siku wenye brand zao wanakosa mapato na hichi kitu kinawakera sana wazungu. Kinachowakera zaidi ni namba mchina anavyopata ushawishi mkubwa Africa kwa kutumia mgongo wa wazungu akiuza bidhaa feki kitu ambacho kinayaathiri makampuni mengi ya Japan, Ulaya hadi Marekani.

Jux aliwahi kuja na Brand yake ya African boy akawa anatengeneza nguo zake hadi kofia kwa brand yake, mwisho wa siku mchina akawa anafyatua kopi anauza kwa bei chee zinamwagwa hapo kariakoo hadi Jux akaanzisha operation ya kukamata bidhaa feki ambazo zinafuatuliwa kwa jina lake.

Mara nyingi wachina wameshakamatwa wanaviwanda bubu wakitengeneza konyagi hadi kvant feki, kuna siku niliona wamekamatwa wanatengeneza soda feki. Yaani wanaathiri uchumi wa nchi hadi watengenezaji wa bidhaa original wanawaharibia, maana kuna kipindi watu walikuwa wanalalamika baadhi ya pombe kali wakinywa kama zimechakachuliwa kumbe nyuma ya pazia watu wanacheza na brand za watu.

Anachotafutiwa mchina sasa hivi ni kuingia mtegoni tu, ili apigwe ban ya kusafirisha bidhaa zake sehem alizokuwa na ushawishi, ili wazungu warudishe tena ushawishi wao. Maana bara la Africa, wazungu wamekuja kushtuka washachelewa kuwa mchina kashawapiga gape kubwa kibiashara hadi Asia huko bidhaa za kichina hazikamatiki.
 
0ozg Tz

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
4,083
10,221
Nasubiri mchina anichongee hammer lenye injini ya gari ndogo kama ist nilinunue kwa milioni 20

Ila mchina anachofanya sio poa kabisa,inaumiza sana,eti "adiddas" anaibadili anaandika "adibbas"

Nasikia hivyo viwanda vinavyofyatua hzo bidhaa zinazoiga brands za watu hata serikali ya uchina haivijui
 
Zodwa

JF-Expert Member
May 20, 2019
26,889
77,485
Taratibu mkuu usiwaseme sana miungu wa watu maana kuna waafrika wenzetu wanawaona hao jamaa kama miungu yani

Hata Kampuni ya Land Rover waliwahi kuwashitaki kwa kutoa copy za Range Rover Evoque na kuita Land Wind walichotofautisha ni door handles tu

Wachina ni certified copy cats
 
themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
593
2,037
Taratibu mkuu usiwaseme sana miungu wa watu maana kuna waafrika wenzetu wanawaona hao jamaa kama miungu yani

Hata Kampuni ya Land Rover waliwahi kuwashitaki kwa kutoa copy za Range Rover Evoque na kuita Land Wind walichotofautisha ni door handles tu

Wachina ni certified copy cats
duuh aisee
 
let the caged bird sings

JF-Expert Member
Sep 19, 2020
2,104
4,842
Russia ni China wana usuuba mkubwa sana na ndiye mashirika wake mkuu lakini bila haibu na hofu akamuuzia Urusi matairi fake. Magari mengi yalikuwa yakiwa na shehena ya silaha kwasababu ya tairi kupasuka.
Ikiwa China hana haibu kwa mshikaji wake na mkuu vipi apate haibu kwa Africa?. China ni sehemu ya kufeli operation ya Urusi ndani ya Ukraine..
 
china sio kabisa
 
Carlitos Way

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
1,105
2,290

Operation ya Urusi imefeli??? unadanganywa na CNN, BBC etc. ??? Urusi wamemaliza operation yao wanajilia kuku kwa mrija..
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
21,352
17,557
Anachotafutiwa mchina sasa hivi ni kuingia mtegoni tu, ili apigwe ban ya kusafirisha bidhaa zake sehem alizokuwa na ushawishi, ili wazungu warudishe tena ushawishi wao. Maana bara la Africa, wazungu wamekuja kushtuka washachelewa kuwa mchina kashawapiga gape kubwa kibiashara hadi Asia huko bidhaa za kichina hazikamatiki.
Wazungu wa wapi unawazungumzia? Maana wazungu ninaowafahamu, ukienda kwao wamejaza vifaa vya Mchina!!
 
Carlitos Way

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
1,105
2,290
Mie nipo huku tunapoionja joto ya jiwe ya Urusi moja kwa moja ...sihitaji hizo media kunidanganya wakati hali ya maisha ninakumbana nayo live na jamaa Urusi ndio ilikua lengo lake, halafu wewe huko hujui kitu unadanganywa eti Urusi kafeli.nyoooooo.
 
V-sulley

Member
Aug 24, 2022
5
7
Nasubiri mchina anichongee hammer lenye injini ya gari ndogo kama ist nilinunue kwa milioni 20

Ila mchina anachofanya sio poa kabisa,inaumiza sana,eti "adiddas" anaibadili anaandika "adibbas"

Nasikia hivyo viwanda vinavyofyatua hzo bidhaa zinazoiga brands za watu hata serikali ya uchina haivijui
:Dni abibbas, yani wamefanya kugeuza zile d tu
 
7 Reactions
Reply
Top Bottom