Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,439
Hili ni moja ya kabila ambalo linapatikana hapa hapa Tanzania hasa upande wa mashariki.
Japo habari na historia la kabila hili zilishaandikwa, hasa juu ya asili ya neno Uzaramo au Wazaramo. Kwa kuwakumbusha tu, Wazaramo maana yake ni waamiaji. Naweza kusema kuwa, kwa mujibu wa wataalamu walioandika habari za makabila ya tanzania na Afrika kwa ujumla , wanasema kuwa, Wazaramo ni jumla ya koo mbalimbali zilizofika Pwani ya Afrika mshariki, hasa maeneo ya mwambao wa Dar es salaam hata kabla ya miaka ya 1600.
Koo hizo ambazo zilitokea bara zilikuja Kuzarama yaani kuhamia maeneo ya Pwani kwa lengo la kufanya shughuli mbalimbali za kibaishara na uvuvi kwenye meneo hayo. Ukweli ni kwamba neno Kuzarama ni la kibantu na maana yake ni Kuhamia.
Hivyo mtu anayehamia huitwa Mzaramo na wakiwa wengi wanaitwa Wazaramo. Na wakati wageni hao wanafika pwani, waliuliza nyinyi ni wakina nani na ndipo wenyeji hao walipojibu kuwa wao ni Wazaramo, yaani wahamiaj. Basi kuanzia hapo yaani miaka ya 1840/1850 kipindi wageni wanafika na kuandika habari za waafrika Watu waliofika Pwani walifahamika kama Wazaramo.
Jambo la kufahamu hapo ni kwamba, koo zilizokuja kuzarama ni kutoka maeneo mbalimbali. Hivyo kuna uwezekano wa kuwa , koo za makabila mengi ziliunda kabila hili la kizaramo. Na ndio maana tamaduni nyingi za kizaramo zipo kwenye makabila mengi japo kuna utofauti kidogo ambao ulisababishwa na masuala ya kijiografia.
Mara baada ya kufahamu habari hizo, tupate kufahamu chimbuko au mahali ambapo kabila hili la kizaramo zilianzia. Inafafanuliwa kuwa, kabila la wazaramo lilipata kuchimbukia maeneo ya Moneromango au wengi hutamka Mwanarumango.
Hama kuhusu Maneromango, ni sehemu inayopatika katika wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani. Inafafanuliwa kuwa eneo hili ndio chimbuko la Wazaramo kwa kuwa, kiongozi wa kabila hili Bwana Pazi Kilama alipata kuishi maeneo hayo, na hata mpaka vita kati ya Wazaramo na Wakamba vinatokea, vilipiganiwa maeneo haya.
Hata koo za Kibena kwa mara ya Kwanza walikutana hapo na Wazaramo na kuachana maeneo ya Moneromango. Na zaidi ya hapo, hata zile koo maarufu kama ukoo wa wakina Samatha na ukoo wakina Kawambwa, zilipata kuishi maeneo ya Monerumano au Mwanarumango.
Na pia kulikuwa na habari nyingi za kuvamiwa na simba, inasimuliwa kuwa maeneo hayo ndio yalikuwa maeneo ambayo yalikuwa yakivamiwa sana na simba. Hivyo maeneo ya Monerumango ndio moja ya maeneo ya mwanzo kukaliwa na Wazaramo.
Sent using Jamii Forums mobile app