Chimbuko la Uislam na Karen Armstrong

Kabla hujamalizia, armstrong na wenzie wanawapa nguvu wale waamini wa dhana kuwa dini zote hizi zimeletwa na viumbe wa ajabu kutoka nje ya dunia yetu hii..higher dimensional na kadhalika.

Maana mwanzo wa uislamu kusema mt. Mohammad alivyotokewa na malaika, n.k.

Na zile kauli za mwanzo " na tuumbe mtu kwa mfano wetu"

Haya yote ukijifunza mambo ya elimu ya sayansi ya anga la nje ya dunia na teknolojia zake, utaelewa namaanisha nini.

Kama huna elimu hii, utaniona ni chizi ninayeongea kisichoeleweka.
 
Kabla hujamalizia, armstrong na wenzie wanawapa nguvu wale waamini wa dhana kuwa dini zote hizi zimeletwa na viumbe wa ajabu kutoka nje ya dunia yetu hii..higher dimensional na kadhalika.

Maana mwanzo wa uislamu kusema mt. Mohammad alivyotokewa na malaika, n.k.

Na zile kauli za mwanzo " na tuumbe mtu kwa mfano wetu"

Haya yote ukijifunza mambo ya elimu ya sayansi ya anga la nje ya dunia na teknolojia zake, utaelewa namaanisha nini.

Kama huna elimu hii, utaniona ni chizi ninayeongea kisichoeleweka.
Lakini hayo ya Tuumbe Mtu kwa mfano wetu, Mtume kutokewa na Jibril, ndivyo vitabu vyenyewe vinasema hivyo. So kama waanzilishi wa dhana hii sio sisi au kina Armstrong 'wanadamu' ni mitume wenyewe.
 
SEHEMU YA II.

Mapokeo ya Quran yalimfanya Muhamad ajihisi woga na hofu kubwa. Aliwaza kuwa labda naye amekuwa Kahin. Kahin ni watu katika jamii ya waarabu ambao waliokuwa ni waganga wa kienyeji waliaminika kuwa na majini yaliyowawezesha kupiga ramli na kuona yasiyoonekana. Katika jamii za waarabu waliamini kuwa Maeneo yao yenye matatizo yalikuwa yametawaliwa na majini. Washairi pia wa maeneo hayo waliamini kuwa na majini. Kwamba wanapopata mawazo au utunzi kichwani ni majini ndiyo yenye kuweza na kusukuma kuweza kuyatamka maneno hayo. Mfano wa mshahiri maarufu aliyeamini hilo ni Hassan ibn Thabit wa Madina ambaye baadae alikuja kuwa Muislam. Hivyo kwa fikra za awali Muḥammad alihisi labda naye amevamiwa na majini na kuwa mwenye Majin, (Majnu). Hili lilimtisha pamoja na sababu nyingine wamiliki wa majini hakuwapenda na aliamini ni waongo. Kazi ngumu aliyoiona mbele yake ni kutofautisha Quran na Mashairi mengine ya kiarabu. Alipokuwa pangoni aliona kiumbe kingine ambaye baadae alikuja jua ni Malkia Jibril (Gabriel).

Katika Uislam, malkia jibril ni anatambulika kama mzimu mtakatifu ambao Mungu kupitia yeye Mungu anawasiliana na wanadamu. Huyu hakuwa malaika wa kawaida, bali mwenye nguvu ambaye haiwezekani kumkimbia. Muhammad alipata hisia za utukufu na woga kwa Jibril, ambapo mitume wa kiyahudi hali hii waniitwa Kaddosh, upande unaotisha wa Mungu [Numinous]. Hali hii ya uoga baada ya kukutana na Jibril Mitume wa kiyahudi nao walidai kuipitia, lakini tofauti na Muḥammad, kwake ilikuwa ni hali ambayo hakuwa na maandalizi nayo wala mila za kumfunza nini cha kufanya. Muhamad jambo pekee aliloweza ni kukimbilia kwa mkewe, Khadija.

Akiwa katika hali ya woga na kutetemeka, Muhamad alimlilia Khadija na kulala mapajani mwake na kumwambia, 'nifunike, nifunike' Akimtaka amkingine dhidi ya uwepo wa utakatifu. Alipotulia, Muḥammad alimuuliza Khadija kama amekuwa Majnun. Khadija akamsihi na kumuambia, haiwezi kuwa hivyo kwani yeye Muhamad ni mtu mwema, mwenye kusaidia masikini na wenye shida, na mwenye kupambana kila siku kuhakikisha kuwa jamii ya waarabu inakuwa na mila nzuri na zenye kupendeza. Khadija alimsihi wamuone Waraqa ibn Nawfal, binamu yake Khadija ambaye wakati huo alikuwa ni Mkristo na alikuwa na uwezo ujuzi wa kusoma na kutafsiri maandiko. Waraqa alimuambia kwa uhakika kuwa alichopokea na ufunuo mtakatifu kutoka kwa Mungu wa Moses na mitume wake, Na amekuwa mjumbe mtakatifu kwa jamii ya waarabu. Baada ya miaka kadhaa Muhamad aliamini kuwa ilikuwa ni sahihi sasa akaanza rasmi kuwahubiria Wakureshi, maandiko katika lugha yao wenyewe [kiarabu].

Tofauti na Torah, ambayo Moses alishushiwa yote kwa mara moja kwenye Mlima Sinai, Muhamad alishushiwa Quran kidogo kidogo, Mstari kwa mstari, neno kwa neno, kwa muda wa miaka 23. Muhamad anasema ufunuo wote kwa kwe haukua rahisi, mara zote alihisi kuwa roho inaacha mwili. Anasema ufunuo huo wa maneno haukuwa mwepesi na rahisi wakati wote, kuna nyakati hakuelewa alichoambiwa, Na kuhitaji jitihada kubwa kutoka kwa jibril kuweza kumuelewa. Mara zote Muhamad anasema alikuwa akisistizwa asitamke wala kueleza maneno hadi aelewe maana kusudiwa na maelekezo hayo ya Mungu. Kama ilivyo kazi zote za ubunifu, kupokea Quran ilikuwa ni kazi inayochosha akili na mwili sana. Ndivyo alivyopitia Muhamad, kuna nyakati alikuwa kama ni mtu aliyepoteza fahamu.

Kwa hiyo, Kazi ya Mapokeo ya Quran kwa Muhamad ilikuwa ni pevu, si tu alikuwa akitengeneza Na kufanyia kazi ufumbuzi wa kisiasa wa matatizo ya jamii yake, bali pia alikuwa akiunda andiko ambalo Limedumu miaka yote. Aliamini kuwa alikuwa akiweka maneno ya Mungu katika Quran ambayo ni nguzo muhimu kwa uislam kama ilivyokuwa neno katika Ukristo. Kupitia Quran ambapo kuna sura kadhaa zimemuelezea, Muḥammad amekuwa ndiye mtume aliyeelezewa zaidi na kuonekana ni jinsi gani dira yale ilivyobadilika na kuwa ni ya ulimwengu wote. Alipewa ufunuo kidogo kidogo kadri matukio mbalimbali yalivyokuwa yakitokea. Quran tunayoisoma leo, haikuwa katika mtiririko huu, kwani alikuwa akiteremshiwa bila utaratibu kufuatana na mambo yanayatokea. Na yeye kwa kuwa alikuwa hajui kusoma wala kuandika, alipokuwa akifunuliwa basi alikuwa akiyatamka maneno hayo na watu aliokuwa nao waliyahifadhi maneno hayo mioyoni na waliokuwa wakijua kuandika walikuwa wakiyaandika maneno hayo. Miaka takribani 20 baada ya kifo chake, ndipo yalikusanywa maandiko yote na kutengeneza kitabu kimoja.

Waliokusanya mwanzo, walipanga Sura ndefu mwanzo ma fupi fupi mwishoni. Mpangilio huu licha ya ukosoaji, haukua na shida yoyote kimantiki sababj Koran sio masimulizi au hoja ambazo zinahitaji mfululizo wa upangaji mawazo, bali ni maandiko yaliyogusa matukio/mazingira mbalimbali kama uwepo wa Mungu kwenye maisha ya kila siku, maisha ya mitume na siku ya hukumu.

Wakati Muhamad alipoanza kuhubiri Quran, hakua na ufahamu mpana wala mawazo kuwa anaeneza dini ya ulimwengu, bali alikuwa akiwaeleza wakureshi dini iliyokuwepo muda wote ya Mungu mmoja. Na mpango wake awali haukuwa kuhubiri katika makabila mengine ya kiarabu, bali maka na viunga vyake tu. Muhamad hakuwa na mamlaka yoyote kisiasa, hivyo yeye kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwaonya wakureshi juu ya mienendo yao. Alikuwa muonyaji [Nadhir]. Wala hakuwa na wajibu wa kuwathibitishia juu ya uwepo wa Mungu, kwani tayari jamii ile ilikuwa inatambua uwepo wa al-Lah kwa miaka Mungu. Mungu huo al-Lah, waliamini ndiye muumba wa mbingu na ardhi na waliamini ndiye Mungu huyo huyo anayeabudiwa na Wakristo na wayahudi. Ingawa tatizo kubwa kwa Muhamad ni kuwa, uwepo wa al-Lah ulikuwa ukichukuliwa poa na waarabu.

Kama ambavyo Mungu anasema kwenye sura za mwanzo za Quran:

Waulize nani aliyeumba Mbingu na ardhi, jua na mwezi na zikatii sheria zake, hakika wengi watakujibu al-Lah | waulize nani aliyeteremsha mvua na kuleta uhai dunia wakati haukuwepo, hakika watakujibu al-Lah.

Kilichomsumbus Muḥammad ni kuwa wakureshi hawakuwa na fikra na mawazo ya muktadha huo. Mungu amewaumba kutokana na tone la manii, hivyo kama alivyosema kwenye Quran wanamtegemea yeye katika maisha yao, lakini wao wanajiona wanaweza kujitegemea kwa kila kitu (Istaqa). Na hawakujali kabisa chochote kuhusu jamii nzima na kuishi kwa maadili. Kufuatana na hili, sura za kwanza katika Koran ziliwasisitiza wakureshi kuuona ukarimu wa Mungu juu yao wakati wote. Na pia wakati wote ambao licha ya mafanikio yao, bado Mungu anaahidi kuwapa mema zaidi na wautii utegemezi wao kwa Mungu.

[Mara nyingi] mwandamu hujiangamiza mwenyewe: kwa ubishi wake huukataa ukweli!
[Mwanadamu huwaza?] Ni kutoka kwenye kitu gani Mungu amemuumba?

Kutoka kwenye tone la manii ndio amemuumba, na ndiye amepanga asili yake na kuwa rahisu yeye kuishi; na mwisho yeye ndiye huamua mwisho wake na kumpeleka kaburini; na kisha, kwa utashi wake humrudishia uhai.

Lakini mwanadamu bado hajatimiza kile anachofurahia,
Acha mwanadamu, afikirie chanzo cha chakula chake; ni kwa vipi tumeleta mvua, na kwa vipi imepelekea nafaka kumea, kwa ajili ya mwanadamu na wanyama kula.]


Hivyo suala la uwepo wa Mungu sio la mjadala kwenye Koran. Bali asiyeamini, kafir bi na 'mat al-Lah, siye mtu asiye amini Mungu, bali ni yule asiyetambua ukuu na fadhili za Mungu. Hivyo Koran haikuwa inawafundisha wakureshi kitu kipya. Ilikuwa ni ukumbusho wa mambo yote yaliyopo. Ndio maana maneno kama 'Je, hamjaona' ama 'Je, hamjafiria' yametumika sana kwenye Koran. Hii maana yake, Quran haikuwa ikitoa maamrisho bali ilikuwa ikifanya mazungumzo na wakureshi. Iliwakumbusha mfano, Kaaba[eneo ambalo watu wa maka mwa miaka mingi waliliona kama ni takatifu], nyumba ya al-Lah, kuwa ndiyo kitovu chao cha mafanikio ambapo kwa maana nyingine ni deni lao kwa Mungu.

Wakureshi walikuwa na mazoea ya kufanya ibada huku wakizunguka madhabahu, lakini waliweka mbele utajiri wao Hivyo wakasahau utamaduni huu wa kale wa kuzunguka madhabahu yao. Walitakiwa wazisome alama za Mungu (Ayat) za ukarimu wa Mungu na ukuu wake kwenye dunia. Na kama watashindwa kuiga ukarimu wa Mungu katika maisha yao ya kila siki, basi watakuwa wamepoteza Muunganiko wao na maumbile ya dunia. Waliomfuata Muḥammad, aliwapa mafunzo ya kuwa wanainama chini wakati wa kusali (salat) mara mbili kwa siku. Kitendo hiki cha kuinama na kutii, kitawafanya wakureshi wawe na fikra na mioyo ya kuyabadilisha maisha yao kuwa wanyenyekevu. Hivyo kitendo hiki cha kuinama na kutii kilichokuwa kinafanywa na waliomuamini Muḥammad, Kuashiria kuacha kutii utajiri wao na kumtii al-Lah, ndicho kikawamsingi wa waislam. Kwa maana ya watu wanaojikabidhi kwa Muumba wa dunia (al-Lah).

Kitendo hiki cha kuinama na kusali, kiliwashtua wakureshi na kukerwa kwani kabila lao lilokuwa huru, na lenye ufahari, liliona ni kitendo sawa na utumwa. Hivyo waislam hao walianza kusali kwa siri. Mapokeo haya ya wakureshi yalimpa picha halisi ya jamii yake ilivyo. Tafsiri halisi ya uislam ilimaanisha wajibu wa jamii kutengeneza jamii iliyo sawa na yenye kusaidia wenye shida. Ujumbe wa kiimani wa uislam ni kuwa si sahihi kujilimbikizia mali na ni vyema kuwasaidia wenye shida kupitia zaka Na kusali sala ambazo ndio nguzo za uislam.

Tutaendelea na sehemu ya tatu wakati mwingine.
Kazi yangu ni moja tu!
safuher

Usisahau kumtag brother Zurri(Sijui anatumia Zurri ipi hata sijui nimtag vipi!)
 
Ingekuwa simple sana unazaliwa tu automatically unamjua Mungu next time Mungu akija kuumba watu uko mbele alifanyie kazi hili jambo.

Maana mabilion ya watu wamekufa pasipo kumjua yeye kama lengo lake katuumba tumuabudu,iwe tu automatically unazaliwa unajua kila kitu kuusu yeye.
 
SEHEMU YA III- MIGONGANO YA UISLAM & DINI ZINGINE ZA KIKURESHI.

Katika miaka ya mwanzo ya harakati zake Muhamad, uislam ulipata waumini wengi ambao walikuwa ni vijana walioumizwa na ubepari wa maka, makundi yaliyokandamizwa kama wanawake na watumwa na koo dhaifu. Ilionekana kuwa, karibu maka yote ingesilimu na kuifuata dini iliyofanyiwa mabadiliko ya al-Lah.

Matajiri na watawala wengi wa maka hawakuwa na shida na dini hiyo, hadi pale Muhamad alipowataka waumini waache kuabudu miungu ya kipagani. Miaka mitatu ya mwanzo ya mahuburi ya Muhamad hakujishughulisha na kusisitiza imani ya Mungu mmoja (al-Lah), hivyo wakazi wengi wa maka waliamini kuwa wangeweza kuendelea kuabudu miungu yao kwa pamoja na al-Lah (Mungu mkuu) kama walivyofanya siku zote. Lakiní alipoanza kuhubiri uharamu wa miungu mingine, alipoteza wafuasi wengi, na uislam adui na kundi la wachache wanaowindwa kuuawa.

Kama ilivyokuwa ukristo wa mwanzo, waislam walichukuliwa kuwa ni wasio Muamini Mungu, kundi ambalo kwa jamii lilionekana kuwa ni tishio. Jamii ya wakureshi ambao 'uumjini' ndio ulikuwa ukiingia, ujio wa uislam ilikuwa ni mgongano wa dhahiri wa kijamii na maisha ya Muhamad mwenyewe yalionekana kuwa hatarini.

Katika jamii ya warabu wa Hijjaz (saudi), kati ya Miungu mitatu, miungu ya al-Lat(Mungu wa kike) na al-Uzza(Aliye Mkuu) ilikuwa ikihusudiwa na jamii hiyo. Al-lat madhabahu yake yalikuwa katika eneo la Taif na Al-Uzza ilikuwa Nakhlah[yote kwa ujumla ilikuwa kusini mwa maka] na Mungu wa tatu, Aliyeitwa Manat (Mungu wa hatma) madhabahu yake yalikuwa Mji wa Qudayd, Pwani ya bahari ya shamu. Miungu huu haikuwa na 'ukamilifu' na iliitwa banat al -Lah (watoto wa kike wa Mungu). Waarabu walikuwa wakitumia neno banat kuonesha uhusiano uliopo kati ya mungu huyo na kazi yake fulani aliyo na nguvu ya kuitenda. Hivyo wanapotumia Banat al-dahr(ni mungu mwenye uwezo wa kuamua hatma). Walipokuwa kuwa wakitumia Banat al-Lah walimaanisha Mwenye Uungu.

Miungu yote hii, kwenye madhabahu, haikuwa na masanamu maalumu bali ni mawe makubwa yaliyosimamishwa. Mawe haya ni mithili ya yaliyokuwepo wakati wa wakanani wa kale, hivyo waarabu waliyatumia kwa ajili ya kuabudia. Kama ambavyo ilivyokuwa kwa kaaba, taif, Nakhlah na Qudayd maeneo haya yalikuwa na umuhimu mkubwa kiimani kwa waarabu. Mababu wa mababu zao waliabudu maeneo hayo na waliamini kuwapa hisia za uponyaji. Uwepo wa Miungu hii ulimpa mivutano na wakureshi, lakini kamwe hakutaka kukubaliana na miungu hii mingi. Jambo kuu Muhamad ambalo alipingana na wakureshi ni kuabudu miungu. Mahubiri yake yote ilikuwa ni msisitizo wa kuachana na miungu yote na kuwa na utii kwa Mungu mmoja (al-Lah) pekee. Kama ilivyosemwa kwenye Sura ya 109 ya Quran; Sema: Enyi makafiri. Siabudu mnacho kiabudu, Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. Wala sitaabudu mnacho abudu. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.

Hivyo waislamu watakuwa na utii kwa Allah tu na si kitu wala mila zingine zozote. Kuamini miungu mingine yoyote ilikuwa ni Shirk, dhambi kuu kuliko yoyote kwenye uislam. Wakureshi walisisitizwa kuacha kuabudu mali au utajiri na matajiri na miungu kwani haina nguvu kama al-Lah naye ndiye muweza wa kuwapa kila kitu. Kama ambavyo iliteremshwa kwenye Sura ya 112 ya Quran (Ikhlas) Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee; Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. Muhamad alijua kuwa Imani ya mungu mmoja itatibu ukabila. Hivyo ingeweza kuunganisha jamii na mtu mmoja mmoja. Wakati Wakristo wanasilimu na kuwa waislam, Muhamad hakuwashawishi wajiunge na uislam labda kwa hiari yake mwenyewe. Muhamad mwenyewe aliamini kuwa Wakristo na wayahudi wao tayari walishafunuliwa dini zao halali kwa ajili yao. Kwa Muhamad, ujio wa Uislam hakuwa kwa ajili ya kufuta dini zingine na matendo ya mitume wengine bali ni muendelezo wa dini kwa mwanadamu.

Koran inafunza kuwa Mungu ametuma mitume katika kila kundi la watu hapa duniani na mtume wake. Kama ambavyo imesemwa kwenye Quran (sura ya 2, Al Baqar};
Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.

Hivyo Quran, imewataja mitume ambao walikuwa wakijulikana kwa waarabu kama Abraham, Nuhu, Musa na pia Yesu, waliokuwa wakijulikana na waarabu kuwa ni mtume wa wakristo. Pia inawataja mitume wa kale wa kiarabu kama Hud na Salih ambao walitumwa kwa jamii za kale za kiarabu za Midian na Thamood.
 
SEHEMU YA IV- CHANZO CHA KIBLA KUWA MAKA.

Baada ya mikwaruzano ndani ya wakureshi juu ya Uislam na kuabudu mungu mmoja, maisha ya waislam na Muhamad mwenyewe yakawa hatarini. Watumwa na waliochwa huru waliuliwa wakati mwingine na ukoo wake Muḥammad mwenyewe wa Hashim (Hashemites). Waarabu wa kipagani wa Yathrib (ambapo baadae waislam wakaja uita Madina), waliwakaribisha wakaishi kule. Wayathrib ni jamii iliyokuwa imevurugika kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na walikuwa kwenye mtanziko mkubwa wa kijamii. Hivyo waliona Uislam kuwa ungewapa muelekeo mpya kiimani na kisiasa. Hivyo waliuhitaji Uislam. Katika jiji hili la Yathrib wayahudi walikuwa ni jamii yenye watu wengi na walikuwa wameshaanza wazoesha wenyeji pale juu ya kuabudu Mungu mmoja. Hii maana yake Muhamad asingepata kazi kuwashawishi juu ya Mungu mmoja kama ilivyokuwa kwa wakureshi. Mwaka 623, Muhamad na familia zipatazo 70 ziliondoka kwenda kuhamia Yathrib (Hijjra).

Baada ya misukosuko ya wakureshi, Muhamad aliona haja ya kushirikiana na jamii ambayo imeshajiimarisha zaidi, hivyo aliusogeza karibu zaidi uarabu na uyahudi. Aliwashawishi waislam kufanya ibada ya funga katika siku takatifu ya wayahudi (Yom Kippur), aliwaagiza wasali mara tatu kwa siku kama wafanyavyo wayahudi (badala ya mbili kama walivyokuwa wakifanya), aliwaruhusu kuoa wanawake wa kiyahudi na kufuata baadhi ya mafundisho/sheria za kiyahudi, Na pia waislam walipaswa kusali kuelekea[Kibla] Jerusalem kama walivyofanya wayahudi. Hivyo wayahudi wa Yathrib (madina) waliiwapokea na kuishi nao vizuri waislam. Lakini baadae waliwageuka na kuanza uadui.

Wayahudi walikuwa na sababu kuu ya kisiasa ya kuwageuka waislam. Walitishika na uwepo wao kwa kuona maslahi yao yako hatarini kutoka kwa waislam hawa wakuja. Wayahudi walianza kumpiga Muhamad na mafundisho yake na kuna nyakati walimdhihaki kuwa iweje mtume wa Mungu anashindwa kujua farasi wake yuko wapi pindi akipotea. Kugeukwa na wayahudi kulimfanya Muhamad avunjike sana moyo na hata kufikiria mara mbili juu ya uelekeo wake kiimani. Lakini si wayahudi wote waliomchukia. Wapo waliompenda na kumpa maandiko ya kiyahudi na kuweza kujisomea. Katika kujisomea maandiko ya kiyahudi ndiko alikojifunza mengi. Kwa mara ya kwanza Muhamad alijifunza mtiririko wa mitume wa kiyahudi na kikristo. Kinyume na alivyokuwa akidhani, alijua kwua wayahudi na Wakristo ni watu wasio dini moja na wasiolewana. Katika mafunzo ya wayahudi aligundua pia, wayahudi wenyewe ni watu walioitwa 'wasio imani' sababu waligeuka na kuabudu sanamu la ng'ombe. Kupitia marafiki wa kiyahudi, Muhamad alijifunza kwenye maandiko yao kisa na Abraham, Isaac na Ismael. Kwenye biblia kisa hiki kinaelezwa kuwa Abrahamu alizaa na kijakazj wake kijana aliyeitwa Ismaili. Baadae mkewe Sarah alizaa kijana aliyeitwa Isaac. Sarah aliamua kumfukuza Haga na mkewe. Mungu kumpa faraja Abarahm alimuahidi Abraham kuwa mwanaye Ismail atakuwa baba wa taifa kubwa. Waarabu pia wana upande wao wa kisa hiki kilichokuwepo miaka mingi kabla ya Muhamad. Wao wanasema kuwa Abarahm aliwaacha Hagar na Ismaili kwenye bonde la mtoto zamzam lililopo Maka na kuwaacha chini ya ulinzi wa Mungu. Maji haya ya zamzam ndiyo yalimnusuru Ismaili na kiu. Baadae Abraham alipoenda watembelea hapo maka, ndipo walipojenga hekalu la Mungu, kaaba. Hivyo kwa waarabu ismail ndio baba wa taifa lao kama ilivyo ismaili kwa wayahudi. Muhamad aliona njia nzuri ya kisa hiki na ufahamu wa waarabu juu ya Kaaba iliyopo Maka, na kuamua kuufanya rasmi uislam uendane na mizizi ya wahenga wa kiarabu. Hivyo hadi kufikia mwaka 624 ilikuwa dhahiri kuwa wayahudi wa madina walikuwa ni maadui wa kudumu wa Muhamad, hivyo January 624 alitangaza rasmi uhuru wa dini mpya ya al-Lah (Uislam). Kutimiza hili aliwaamrisha waislam wabadili kibla kutoka Jerusalem na waelekee Maka. Kubadili kwa kibla ndio linaloitwa tukio la kibunifu zaidi la Muhamad kwenye uislam. Kwani hapa aliufanya Uislam kuwa dini huru kutoka kwenye Ukristo na Uyahudi na wanajimilikisha kwa Mungu, kama alivyofanya abraham alipojenga nyumba yake takatifu ya kaaba pale maka.

Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina.

Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake
 
Kuna kitu najiuliza kuhusu idadi ya sala kwa waislamu,nataka kujua sala ni mara tano kwa siku au mara mbili kwa siku? , manake ktk sehemu yako ya PILI ya mada hii umeeleza kusali mara mbili na pia kuna aya kwenye Quran zinaongelea kuhusu kumsujudia mola mara mbili.
 
Kabla ya kiza kuingia nilijua wazi kuwa wale waarabu wa tandale na magomeni wenye ngozi nyeusi, pua pana, nywele ngumu na lips pana watakuja kujambia hii mada

Hiyo ni kwasababu wengi wao wameshashiba kahawa na kashata

Wabillah Tawfiq
 
Kuna kitu najiuliza kuhusu idadi ya sala kwa waislamu,nataka kujua sala ni mara tano kwa siku au mara mbili kwa siku? , manake ktk sehemu yako ya PILI ya mada hii umeeleza kusali mara mbili na pia kuna aya kwenye Quran zinaongelea kuhusu kumsujudia mola mara mbili.
Mwanzoni zilikuwa mbili. Baadae katika kuwaridhisha/kuwashawishi/kutafuta kukubalika kwa wayahudi waliompokea Madina, Muhamad aliamrisha ziwe tatu kuendana nao. Sasa zilifikaje tano. Tuendelee na usomaji hapa.
 
Kuna kitu najiuliza kuhusu idadi ya sala kwa waislamu,nataka kujua sala ni mara tano kwa siku au mara mbili kwa siku? , manake ktk sehemu yako ya PILI ya mada hii umeeleza kusali mara mbili na pia kuna aya kwenye Quran zinaongelea kuhusu kumsujudia mola mara mbili.
Uzi hujaisha mkuu,
Teundelee kufuatilia
 
Ingekuwa simple sana unazaliwa tu automatically unamjua Mungu next time Mungu akija kuumba watu uko mbele alifanyie kazi hili jambo.

Maana mabilion ya watu wamekufa pasipo kumjua yeye kama lengo lake katuumba tumuabudu,iwe tu automatically unazaliwa unajua kila kitu kuusu yeye.
Hii ndio maana ya kutupa akili ya kuchanganua mambo.
Wanyama ndio Wapo hivyo
 
Ukipata kitabu kinachoelezea chimbuko na evolution za imani na dini za kiafrika kichambue pia

Inaboa kuchambua na kujadili imani za kigeni kila siku
Naunga mkono hoja, maana kama Mungu alisema amewatuma wajumbe ktk kila jamii basi nasisi tuwatafute mitume yetu ya kiafrica
 
SEHEMU YA V

A. HIJJA

Mwaka 620 Muḥammad alifanikiwa kurudi nyumbani kwao, mji wa Madina na alipokelewa pasi na tabu yoyote. Mwaka 632 aliwatembelea waarabu wa Hajj waliokuwa wapagana na kusilimisha kuwa waislam. Kwa waarabu, kutembelea Hijja ilikuwa ni utamaduni wao wa miaka mingi kabla Muhamad na uislam haujaja. Ziara hii ya Muhamad, waislam waliipa hadhi na Muhamad kuamuru, kutembelea Hijja iwe ni nguzo ya 5 ya waislam wote.

Waislam wote wana wajibu, wakiwa na uwezo, kutembelea hijja mara moja kwa katika maisha yao. Tukio hili kwa waislam ni kumbukumbukwa Muhamad, lakini tukio hili linamkumbuka pia Abarahm, Hagar na Ismael. Lakini kwa uhalisia zaidi, mamia ya wanaoenda Hijja leo sio waarabu, lakini waislam hawa wamefanikiwa kuufanya Utamaduni wa kale wa waarabu kuwa ni wa kwao. Kama ambavyo wanavyokutana kaaba, waislam huhisi kuwa wametua mizigo yao yote na eneo hili hata kama ni maadui, hapa hawapaswi kukwaruzana.

B. HAKI ZA WANAWAKE.

Wakati wa Uhai wa Muhamad, moja ya kundi alilokuwa akiwapa kipaumbele sana ilikuwa ni wanawake. Katika jamii za waarabu, kabla ya Uislam (jahiliyyah), zilitawaliwa sana na mfumo dume. Wanawake walichukuliwa kama daraja la pili, vichanga wa kike waliuliwa, hawakua na haki ya kumiliki mali, na polygamism Na wanawake walipaswa kuishi kwa baba zao tu hadi watakapoolewa. Uislam ulipiga marufuku kuuliwa vichanga wa kike, iliwaruhusu wanawake kumiliki mali na haki ya talaka. Muhamad aliwapa msisitizo wanawake washiriki katika shughuli za jumuiya (ummah). Wanawake wa Madina mara nyingi walikuwa wakimkibilia Muhamad katika masuala mbalimbali yanapowatatiza. Mfano, walikuwa wakwikwazika kwanini Quran inawasemea wanaume tu hata pale wanawake wanapokuwa wamejiunga n Uislam. Kufuatia hili, Muḥammad aliteremshiwa sura maalum kwa ajili ya kuelezea masuala ya wanawake. Hadi Muhammad anakufa aliacha maandiko yanayosemea haki za wanawake. Lakini baada ya kifo chake, mfumo dume ulishika hatamu kwenye uislam.

So far, hayo ndio mazingira ambayo uislam ulianzia hadi kufa kwa Muhamad, muasisi wake. Sasa unapoutazama Uislam, upo sehemu kuu mbili. Moja ni Mazingira ya Uarabuni kabla ya Uislam hadi kuibuka kwa uislam wenyewe na Pili ni Uislam baada ya kifo cha Muhamad. Baada ya kifo cha Muhamad, mgogoro mkubwa ilikuwa ni nani awe kiongozi wa waislam. Wapo walioamini na walikuwa wengi kuwa aliyepaswa kuwa kiongozi ni Abu Bakar alikyekuwa ni mfuasi wa karibu wa mtume na baba mkwe, hawa walichagua anafaa kwa sababu ya sifa zake(hawa ndio waliitwa Wasuni). Na kundi la pili waliamini kuwa Kama Muhamad angekuwa hai, basi angemchagua Ali, aliyekuwa ni binamu yake. Hivyo, hadi Ali aliposhika uongozi wa uislam(Khalifa), baada ya viongozi watatu kupita, Ndipo baadhi ya waislam walimtambua kuwa ndio Khalifa wao wa Kwanza, hawa ndio washia. Kwa idadi wako wachache duniani. Kuna maelezo yanafaa sana kuwaelezea washia na wasuni, nitayaambatanisha hapa chini.
 
Back
Top Bottom