Chimbuko la Uislam na Karen Armstrong

spensa_e

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
3,576
2,000
Kingine nikuelimishe kauli yako hii

"Jibu humu kumbuka hadith zote zipo kwenye kitabu kinaitwa sahih"

不不 Mkuu utanisamehe maana mpaka hapa nimeshaelewa level yako ya ufaham wa dini hii ya uislamu sorry no offence.

Kwanza si kweli kwamba "hadithi zote zipo kwenye kitabu kinaitwa sahihi 不不
(Sorry nimeshindwa kujizuia aisee) hakuna kitabu kinaitwa sahih .

Vitabu vya hadithi vinategemeana na madhhab unayoyaongelea mfano
Sunni islam wana vitabu hivi hapa sahih muslim, bukhari, sunnan ibn majah , na sunnan ibn taymiyya.

Ukija kwa shia islam wao wana kitabu kinaitwa "nahjul balagha" sasa sijui hicho sahih... Umekitoa wapi .

Ila umejitahidi aisee 不 you're wellcome nikimakiza kukujibu maswali yako yoote kama nilivyosema na mimi nina yangu machache.
Soma na uelewe nilijibu kwamba Hadith zote nilizo weka zimetoka kwenye kitabu ambacho tayari kinaitwa Sahih , Kuna sahih muslim na sahih Bukhari , so sikutegeme ule mchezo wenu mkizidiwa hoja mnasema Dhaif hadith
Hadith zote za Sunn ninazo maelfu ila za shia ndio sina
-ukinifundisha kuhusu hadith unapoteza muda tuendelee na mada , wewe utakuwa unazipata hadith , Koran na Tafsir
-Kuna aya za unyonyeshaji hazipo kwenye Koran baada ya Muhammad , nani kazifuta?
 

spensa_e

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
3,576
2,000
huyu ata icho kiswahili hakijui vizuri
"Muhandishi"? embu kwanza jifunze hii lugha ya taifa kbla ya kutukana Qur'an mna Qur'an ina maajabu yake kwaio usidhani kujua kwako kiarabu ndo ukaijua Qur'an we bdo ni mchanga sana kwenye kitabu hiki kitukufu
Halaf m naona huna hoja zaidi ya Ubishi mna ilo swali lko la 1st na 3rd m nilishakujibu kitambo tuu ila naona umekaza Fuvu we KAFIRI

Na ukifa kwenye UKAFIRI moto ni halali yako

N.b. M hua sikujibu mna huna hoja iliuo madhubuti zaidi ya Chuki zako
Hajawahi kujibu 1st na 3rd , ulijibu ukatoka nje ya swali ukaanza kuongelea allah anapo ongea kwa wingi (anaposema Sisi)
cha hajabu huwezi kujibu maswali ila unaweza kuandika maelezo ambayo hayaeleweki kama hayo hapo juu

rudi pangua hoja au kama umeshindwa sema Hadith ni Dhaif nifunge mada
  • Nani kafuta na wapi kwenye koran tunasoma zilifutwa, Muhammad kafa kaziacha
  • Aisha anasema allah alipunguza kunyonyesha mtu mzima kutoka mara 10 kwenda mara 5 na sio kufuta
Sahih-Muslim 1453e:
....I see in the face of Abu Hudhaifa (the signs of disgust) on account of entering of Salim (in the house), whereupon Allahs Messenger said Suckle him. She (Sahla bint Suhail) said: He has a beard. But he (again) said: Suckle him, ....
Verse zilikuwepo
Sahih Muslim 1452b
...There was revealed in the Holy Qur'an ten clear sucklings, and then five clear (sucklings).
Sahih Muslim 1452a
'A'isha (Allah be pleased with, her) reported that it had been revealed in the Holy Qur'an that ten clear sucklings make the marriage unlawful, then it was abrogated by five sucklings and Allah's Apostle (儱) died and it was before that time (found) in the Holy Qur'an (and recited by the Muslims).
 

Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,713
2,000
SEHEMU YA II - MAPOKEO YA QURAN.

Mapokeo ya Quran yalimfanya Muhamad ajihisi woga na hofu kubwa. Aliwaza kuwa labda naye amekuwa Kahin. Kahin ni watu katika jamii ya waarabu ambao waliokuwa ni waganga wa kienyeji waliaminika kuwa na majini yaliyowawezesha kupiga ramli na kuona yasiyoonekana. Katika jamii za waarabu waliamini kuwa Maeneo yao yenye matatizo yalikuwa yametawaliwa na majini. Washairi pia wa maeneo hayo waliamini kuwa na majini. Kwamba wanapopata mawazo au utunzi kichwani ni majini ndiyo yenye kuweza na kusukuma kuweza kuyatamka maneno hayo. Mfano wa mshahiri maarufu aliyeamini hilo ni Hassan ibn Thabit wa Madina ambaye baadae alikuja kuwa Muislam. Hivyo kwa fikra za awali Mu廎仟mmad alihisi labda naye amevamiwa na majini na kuwa mwenye Majin, (Majnu). Hili lilimtisha pamoja na sababu nyingine wamiliki wa majini hakuwapenda na aliamini ni waongo. Kazi ngumu aliyoiona mbele yake ni kutofautisha Quran na Mashairi mengine ya kiarabu. Alipokuwa pangoni aliona kiumbe kingine ambaye baadae alikuja jua ni Malkia Jibril (Gabriel).

Katika Uislam, malkia jibril ni anatambulika kama mzimu mtakatifu ambao Mungu kupitia yeye Mungu anawasiliana na wanadamu. Huyu hakuwa malaika wa kawaida, bali mwenye nguvu ambaye haiwezekani kumkimbia. Muhammad alipata hisia za utukufu na woga kwa Jibril, ambapo mitume wa kiyahudi hali hii waniitwa Kaddosh, upande unaotisha wa Mungu [Numinous]. Hali hii ya uoga baada ya kukutana na Jibril Mitume wa kiyahudi nao walidai kuipitia, lakini tofauti na Mu廎仟mmad, kwake ilikuwa ni hali ambayo hakuwa na maandalizi nayo wala mila za kumfunza nini cha kufanya. Muhamad jambo pekee aliloweza ni kukimbilia kwa mkewe, Khadija.

Akiwa katika hali ya woga na kutetemeka, Muhamad alimlilia Khadija na kulala mapajani mwake na kumwambia, 'nifunike, nifunike' Akimtaka amkingine dhidi ya uwepo wa utakatifu. Alipotulia, Mu廎仟mmad alimuuliza Khadija kama amekuwa Majnun. Khadija akamsihi na kumuambia, haiwezi kuwa hivyo kwani yeye Muhamad ni mtu mwema, mwenye kusaidia masikini na wenye shida, na mwenye kupambana kila siku kuhakikisha kuwa jamii ya waarabu inakuwa na mila nzuri na zenye kupendeza. Khadija alimsihi wamuone Waraqa ibn Nawfal, binamu yake Khadija ambaye wakati huo alikuwa ni Mkristo na alikuwa na uwezo ujuzi wa kusoma na kutafsiri maandiko. Waraqa alimuambia kwa uhakika kuwa alichopokea na ufunuo mtakatifu kutoka kwa Mungu wa Moses na mitume wake, Na amekuwa mjumbe mtakatifu kwa jamii ya waarabu. Baada ya miaka kadhaa Muhamad aliamini kuwa ilikuwa ni sahihi sasa akaanza rasmi kuwahubiria Wakureshi, maandiko katika lugha yao wenyewe [kiarabu].

Tofauti na Torah, ambayo Moses alishushiwa yote kwa mara moja kwenye Mlima Sinai, Muhamad alishushiwa Quran kidogo kidogo, Mstari kwa mstari, neno kwa neno, kwa muda wa miaka 23. Muhamad anasema ufunuo wote kwa kwe haukua rahisi, mara zote alihisi kuwa roho inaacha mwili. Anasema ufunuo huo wa maneno haukuwa mwepesi na rahisi wakati wote, kuna nyakati hakuelewa alichoambiwa, Na kuhitaji jitihada kubwa kutoka kwa jibril kuweza kumuelewa. Mara zote Muhamad anasema alikuwa akisistizwa asitamke wala kueleza maneno hadi aelewe maana kusudiwa na maelekezo hayo ya Mungu. Kama ilivyo kazi zote za ubunifu, kupokea Quran ilikuwa ni kazi inayochosha akili na mwili sana. Ndivyo alivyopitia Muhamad, kuna nyakati alikuwa kama ni mtu aliyepoteza fahamu.

Kwa hiyo, Kazi ya Mapokeo ya Quran kwa Muhamad ilikuwa ni pevu, si tu alikuwa akitengeneza Na kufanyia kazi ufumbuzi wa kisiasa wa matatizo ya jamii yake, bali pia alikuwa akiunda andiko ambalo Limedumu miaka yote. Aliamini kuwa alikuwa akiweka maneno ya Mungu katika Quran ambayo ni nguzo muhimu kwa uislam kama ilivyokuwa neno katika Ukristo. Kupitia Quran ambapo kuna sura kadhaa zimemuelezea, Mu廎仟mmad amekuwa ndiye mtume aliyeelezewa zaidi na kuonekana ni jinsi gani dira yale ilivyobadilika na kuwa ni ya ulimwengu wote. Alipewa ufunuo kidogo kidogo kadri matukio mbalimbali yalivyokuwa yakitokea. Quran tunayoisoma leo, haikuwa katika mtiririko huu, kwani alikuwa akiteremshiwa bila utaratibu kufuatana na mambo yanayatokea. Na yeye kwa kuwa alikuwa hajui kusoma wala kuandika, alipokuwa akifunuliwa basi alikuwa akiyatamka maneno hayo na watu aliokuwa nao waliyahifadhi maneno hayo mioyoni na waliokuwa wakijua kuandika walikuwa wakiyaandika maneno hayo. Miaka takribani 20 baada ya kifo chake, ndipo yalikusanywa maandiko yote na kutengeneza kitabu kimoja.

Waliokusanya mwanzo, walipanga Sura ndefu mwanzo ma fupi fupi mwishoni. Mpangilio huu licha ya ukosoaji, haukua na shida yoyote kimantiki sababj Koran sio masimulizi au hoja ambazo zinahitaji mfululizo wa upangaji mawazo, bali ni maandiko yaliyogusa matukio/mazingira mbalimbali kama uwepo wa Mungu kwenye maisha ya kila siku, maisha ya mitume na siku ya hukumu.

Wakati Muhamad alipoanza kuhubiri Quran, hakua na ufahamu mpana wala mawazo kuwa anaeneza dini ya ulimwengu, bali alikuwa akiwaeleza wakureshi dini iliyokuwepo muda wote ya Mungu mmoja. Na mpango wake awali haukuwa kuhubiri katika makabila mengine ya kiarabu, bali maka na viunga vyake tu. Muhamad hakuwa na mamlaka yoyote kisiasa, hivyo yeye kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwaonya wakureshi juu ya mienendo yao. Alikuwa muonyaji [Nadhir]. Wala hakuwa na wajibu wa kuwathibitishia juu ya uwepo wa Mungu, kwani tayari jamii ile ilikuwa inatambua uwepo wa al-Lah kwa miaka Mungu. Mungu huo al-Lah, waliamini ndiye muumba wa mbingu na ardhi na waliamini ndiye Mungu huyo huyo anayeabudiwa na Wakristo na wayahudi. Ingawa tatizo kubwa kwa Muhamad ni kuwa, uwepo wa al-Lah ulikuwa ukichukuliwa poa na waarabu.

Kama ambavyo Mungu anasema kwenye sura za mwanzo za Quran:

Waulize nani aliyeumba Mbingu na ardhi, jua na mwezi na zikatii sheria zake, hakika wengi watakujibu al-Lah | waulize nani aliyeteremsha mvua na kuleta uhai dunia wakati haukuwepo, hakika watakujibu al-Lah.

Kilichomsumbus Mu廎仟mmad ni kuwa wakureshi hawakuwa na fikra na mawazo ya muktadha huo. Mungu amewaumba kutokana na tone la manii, hivyo kama alivyosema kwenye Quran wanamtegemea yeye katika maisha yao, lakini wao wanajiona wanaweza kujitegemea kwa kila kitu (Istaqa). Na hawakujali kabisa chochote kuhusu jamii nzima na kuishi kwa maadili. Kufuatana na hili, sura za kwanza katika Koran ziliwasisitiza wakureshi kuuona ukarimu wa Mungu juu yao wakati wote. Na pia wakati wote ambao licha ya mafanikio yao, bado Mungu anaahidi kuwapa mema zaidi na wautii utegemezi wao kwa Mungu.

[Mara nyingi] mwandamu hujiangamiza mwenyewe: kwa ubishi wake huukataa ukweli!
[Mwanadamu huwaza?] Ni kutoka kwenye kitu gani Mungu amemuumba?

Kutoka kwenye tone la manii ndio amemuumba, na ndiye amepanga asili yake na kuwa rahisu yeye kuishi; na mwisho yeye ndiye huamua mwisho wake na kumpeleka kaburini; na kisha, kwa utashi wake humrudishia uhai.

Lakini mwanadamu bado hajatimiza kile anachofurahia,
Acha mwanadamu, afikirie chanzo cha chakula chake; ni kwa vipi tumeleta mvua, na kwa vipi imepelekea nafaka kumea, kwa ajili ya mwanadamu na wanyama kula.]


Hivyo suala la uwepo wa Mungu sio la mjadala kwenye Koran. Bali asiyeamini, kafir bi na 'mat al-Lah, siye mtu asiye amini Mungu, bali ni yule asiyetambua ukuu na fadhili za Mungu. Hivyo Koran haikuwa inawafundisha wakureshi kitu kipya. Ilikuwa ni ukumbusho wa mambo yote yaliyopo. Ndio maana maneno kama 'Je, hamjaona' ama 'Je, hamjafiria' yametumika sana kwenye Koran. Hii maana yake, Quran haikuwa ikitoa maamrisho bali ilikuwa ikifanya mazungumzo na wakureshi. Iliwakumbusha mfano, Kaaba[eneo ambalo watu wa maka mwa miaka mingi waliliona kama ni takatifu], nyumba ya al-Lah, kuwa ndiyo kitovu chao cha mafanikio ambapo kwa maana nyingine ni deni lao kwa Mungu.

Wakureshi walikuwa na mazoea ya kufanya ibada huku wakizunguka madhabahu, lakini waliweka mbele utajiri wao Hivyo wakasahau utamaduni huu wa kale wa kuzunguka madhabahu yao. Walitakiwa wazisome alama za Mungu (Ayat) za ukarimu wa Mungu na ukuu wake kwenye dunia. Na kama watashindwa kuiga ukarimu wa Mungu katika maisha yao ya kila siki, basi watakuwa wamepoteza Muunganiko wao na maumbile ya dunia. Waliomfuata Mu廎仟mmad, aliwapa mafunzo ya kuwa wanainama chini wakati wa kusali (salat) mara mbili kwa siku. Kitendo hiki cha kuinama na kutii, kitawafanya wakureshi wawe na fikra na mioyo ya kuyabadilisha maisha yao kuwa wanyenyekevu. Hivyo kitendo hiki cha kuinama na kutii kilichokuwa kinafanywa na waliomuamini Mu廎仟mmad, Kuashiria kuacha kutii utajiri wao na kumtii al-Lah, ndicho kikawamsingi wa waislam. Kwa maana ya watu wanaojikabidhi kwa Muumba wa dunia (al-Lah).

Kitendo hiki cha kuinama na kusali, kiliwashtua wakureshi na kukerwa kwani kabila lao lilokuwa huru, na lenye ufahari, liliona ni kitendo sawa na utumwa. Hivyo waislam hao walianza kusali kwa siri. Mapokeo haya ya wakureshi yalimpa picha halisi ya jamii yake ilivyo. Tafsiri halisi ya uislam ilimaanisha wajibu wa jamii kutengeneza jamii iliyo sawa na yenye kusaidia wenye shida. Ujumbe wa kiimani wa uislam ni kuwa si sahihi kujilimbikizia mali na ni vyema kuwasaidia wenye shida kupitia zaka Na kusali sala ambazo ndio nguzo za uislam.

Tutaendelea na sehemu ya tatu wakati mwingine.
Hii dini ni ya kikatili sana, inaleta maafa makubwa duniani, ona Msumbiji,Congo, Somalia, watu wameivamia hii dini kwa pupa
 

Consensus ad idem

JF-Expert Member
Jul 12, 2021
294
250
Hajawahi kujibu 1st na 3rd , ulijibu ukatoka nje ya swali ukaanza kuongelea allah anapo ongea kwa wingi (anaposema Sisi)
cha hajabu huwezi kujibu maswali ila unaweza kuandika maelezo ambayo hayaeleweki kama hayo hapo juu

rudi pangua hoja au kama umeshindwa sema Hadith ni Dhaif nifunge mada
  • Nani kafuta na wapi kwenye koran tunasoma zilifutwa, Muhammad kafa kaziacha
  • Aisha anasema allah alipunguza kunyonyesha mtu mzima kutoka mara 10 kwenda mara 5 na sio kufuta
Sahih-Muslim 1453e:
....I see in the face of Abu Hudhaifa (the signs of disgust) on account of entering of Salim (in the house), whereupon Allahs Messenger said Suckle him. She (Sahla bint Suhail) said: He has a beard. But he (again) said: Suckle him, ....
Verse zilikuwepo
Sahih Muslim 1452b
...There was revealed in the Holy Qur'an ten clear sucklings, and then five clear (sucklings).
Sahih Muslim 1452a
'A'isha (Allah be pleased with, her) reported that it had been revealed in the Holy Qur'an that ten clear sucklings make the marriage unlawful, then it was abrogated by five sucklings and Allah's Apostle (儱) died and it was before that time (found) in the Holy Qur'an (and recited by the Muslims).
 

spensa_e

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
3,576
2,000
huyu ata icho kiswahili hakijui vizuri
"Muhandishi"? embu kwanza jifunze hii lugha ya taifa kbla ya kutukana Qur'an mna Qur'an ina maajabu yake kwaio usidhani kujua kwako kiarabu ndo ukaijua Qur'an we bdo ni mchanga sana kwenye kitabu hiki kitukufu
Halaf m naona huna hoja zaidi ya Ubishi mna ilo swali lko la 1st na 3rd m nilishakujibu kitambo tuu ila naona umekaza Fuvu we KAFIRI

Na ukifa kwenye UKAFIRI moto ni halali yako

N.b. M hua sikujibu mna huna hoja iliuo madhubuti zaidi ya Chuki zako
  • Uncho sikitisha ni mtupu sana kwenye dini
  • Unasema mtu akifa na ukafiri moto ni Halali , na unampinga Allah na Muhammad
  • Allah kasema ata uwe mwema atakupeleka motoni na ata uwe kafir atakupeleka kwenye pepo yake
  • Ata mtoto mchanga akifa kama Allah alimpangia moto ni moto tu
  • .....And by Allah, a person among you (or a man) may do deeds of the people of the Fire till there is only a cubit or an arm-breadth distance between him and the Fire, but then that writing (which Allah has ordered the angel to write) precedes, and he does the deeds of the people of Paradise and enters it; and a man may do the deeds of the people of Paradise till there is only a cubit or two between him and Paradise, and then that writing precedes and he does the deeds of the people of the Fire and enters it." Sahih al-Bukhari 6594
 

Mubarridi

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
22,337
2,000
HiI Ni forum inajitegemea , inatakiwa uweke kipengele humu sio kumpa mtu Kazi akasome mavitabu , unachofanya ni kusumbua unae mjibu ILI wewe uonekane umejibu kumbe huna jibu , jibu kwa kuweka ushahidi hapa kinyume Cha hapo unao fanya ni utoto na kila mara nakwambia

Vitabu wameandika waislamu alafu wewe ndio unatumia kuwa ni majibu ya ukristo ,
Vitabu vina faharisi/Yaliyomo rejea kachague unachokitaka utakikuta usitafute pakutokea haya haya unayotuwekea humu yapo vitabuni,sasa soma vitabu usikimbie hoja.
 

Mubarridi

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
22,337
2,000
Hoja yangu nimeshaimaliza na nimeshathibitisha Allah anapoongea
1st person - yani Mimi au sisi (kujiongelea wewe ndio muhusika au nyinyi ndio wahusika)
3rd person -kuongelea mtu mwingine ambae sio wewe yani wao, yeye ,yakwao, aliye n.k (kuongelea mtu mwingine ndie muhusika au watu wengine ndio wahusika)
Mfano
Koran
1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi
2.Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo,....
Hakuna hoja hapo sababu unaenda kinyume na uhalisia na kuonyesha ya kuwa huijui Qur'aan na hili nimeliweka wazi tangu mwanzo.
 

Top leader

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
769
1,000
Hii dini ni ya kikatili sana, inaleta maafa makubwa duniani, ona Msumbiji,Congo, Somalia, watu wameivamia hii dini kwa pupa
mambwa kama nyie ndo wakuua kabisa mnadanganywa na vitabu vya juzi mbwa nyie .usislamu ni dini haki na ndo dini ya mwenyezi mungu
 

Mubarridi

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
22,337
2,000
Allah! ni muislam?
Hili ndiyo tatizo la kujadili mambo ukiwa hujui unajadili nini.

Umeuliza swali la uongo,sababu Allah hajengewi swali kwa mjengo huo.

Swali lako limeonyesha yafuatayo :

1. Hujui Uislamu ni nini ?
2. Humjui Allah ni nani ?

Hili tatizo kubwa sana.

Sasa nakwambia hivi "Tengeneza kiti chako kwanza kisha ndiyo ukipambe".
 

love life live life

JF-Expert Member
Sep 12, 2021
767
1,000
Hili ndiyo tatizo la kujadili mambo ukiwa hujui unajadili nini.

Umeuliza swali la uongo,sababu Allah hajengewi swali kwa mjengo huo.

Swali lako limeonyesha yafuatayo :

1. Hujui Uislamu ni nini ?
2. Humjui Allah ni nani ?

Hili tatizo kubwa sana.

Sasa nakwambia hivi "Tengeneza kiti chako kwanza kisha ndiyo ukipambe".
Allah simjui ndio na sitaki kumjua..
Na naelezea Allah kwa jinsi wafuasi wake mnavyo muelezea
Lakini kunawalakini juu uwezo wa Allah unapoishia inakuwaje
Allah anataka apiganiwe kwa jihadi kwanini asijipiganie mwenyewe?
Au mnalipa fadhila ya kuumbwa na Allah
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom