Chimbuko la mgogoro wa UKAWA jimbo la Mtama Lindi

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Awali wanachama wa CCM jimbo la Mtama kwa pamoja walikuwa wanamwunga mkono kada mzawa ndugu Selemani Mathew Kilowoko mtoto wa mstaafu wa jeshi la polisi.

Tangu mwanzo tulikuwa tunajua kwamba kada nguli wa chama tawala Mh. Napelepele atakuja kugombea jimbo kama TX (Kwa waliozaliwa zamani wanajua nini maana ya TX),hiyo haikuwasumbua sana wanachama wa CCM jimboni.

Kabla ya hapo mratibu mkuu wa kumleta TX agombanie jimbo la Mtama Lindi ni yeye mwenyewe Mbunge anayemaliza muda wake Mh. Membe na niwambie wazi wana bodi kwamba Mh. huyu alikuwa na uhakika wa 100% kwamba atafanikiwa kupewa ridhaa aliyopata Mh. Magufuri.Katika mashauriano Mh. Membe alipinga sana ndugu Selemani kupewa kijiti kwa kigezo cha elimu maana ndugu Selemani ni form four lakini Kilowoko ni wazaliwa wa hapa jimboni na babake Selemani amstaafu yuko hapa hapa jimboni.Wapo wanachama waliompinga Mh. Membe kwa kuona kama swala la elimu ni sababu ya kutompa ridhaa ndugu Selemani maana walisema Selemani anawazidi wabunge wengi wa CCM kielimu wakatoa mfano anawazidi Mh. Ngonyani( Pro.maji malefu), Mh Sanga (jah,people) na wengine.

Mh. Membe alisisitiza kwa kuwa yeye atakuwa Rais ni rahisi kumpa TX uwaziri kuliko Seleman akasema ni vigumu Jumanne kupata hata uenyekiti wa kamati.

Wajumbe wengine walimweleza waziri ugumu atakaopata TX kwenye kura za maoni maana TX hana hata ndugu hapa jimboni, ndugu zake wachache wako kijiji cha Makukwe Mahuta Tandahimba na wala hawamfahamu sana maana hata babayake alikuwa hafiki kijijini na msiba wa babayake TX ulikuwa kwenye nyumba ya mkuu wa mkoa Mh Yusuf Makamba yote yalizungumzwa.Waziri akasema hiyo yote haina shida.

Kilichotokea kumbe Mh. Membe na TX walikuwa na lao jambo maana wanachama waliisha kubaliana kwamba wampige chini TX kwenye kura za maoni na walimhakikishia kijana wao Jumanne ushindi.

Jimbo linawanachama hai wa CCM walioko kwenye leger ya katibu wasiozidi 6000,kwa kuwa kura huwa hawapigi wote basi mshindi halali angepata kama kura 4000 na zaidi kidogo (na ndizo alizopata Jumanne). Alichofanya TX Mh. Membe asijifanye hajui, TX alikuja na machapisho ya kura za wanachama hewa 12000, wanachama wa idadi hiyo hapa jimboni hamna, TX alifanikiwa kuziingiza kura hizo hewa kwenye masanduku kama vile ambavyo wenzie akina Gaudensia Kabaka na Malima Nyangwine ambavyo hawakufanikiwa kuingiza kura zao kwene msanduku wakakamatwa, TX alikuwa ana bahati tu hakukamatwa.

Baada ya matokeo hayo kutangazwa ikaonekana TX kapata 12000 na Jumanne 4000, jumla 16,000. Jimbo la Mtama halina wanachama idadi hiyo , matokeo hayo ndiyo ya mshindi wa ubunge uchaguzi mkuu subirini mtaona.

Ni wanachama wa CCM ndio waliomshinikiza Selemani atafute chama, wanachama wa CCM hawajui makubaliano ya UKAWA kwa sababu waliisha panga Jumanne akamate jimbo, hata kama TX asingecheza rafu zake Isihaka Mchinjita asingemweza Jumanne wa CCM.

Ndiyo maana alivyokuja Lowassa wakarudisha makadi ya TX yote , zile kadi waligawiwa wanachama wa CCM feki ili wampitishe TX pamoja na kadi alikuwa anawapa shs 20000, ndiyo zile hela alizokamatwa na TAKUKURU wote mliona.

Baada ya Seleman kujiunga na CHADEMA ndiye chaguo la wanachama wengi wa CCM,waliosababisha makubaliano ya UKAWA yavunjwe ni wanachi wa jimbo kwa machungu aliyofanyiwa kijana wao.

Kuna habari UKAWA kuna jambo wamkekubaliana hapa jimboni, ni vigumu maana majina yote yamepokelewa na NEC, ILA KIFUPI SELEMANI MATHEW KILOWOKO NDIYE ANAYEUNGWA MKONO.

source ni mimi mwenyewe niko jikoni,
 
Karibia majimbo yote waliyoshinda vyama vya upinzani 2010 yalikuwa na wagombea zaidi ya wawili, yaani wa CCM mmoja na wapinzani zaidi ya mmoja. Lakini vyama vya upinzani vilishinda bado

Majimbo ambayo CCM walishinda 2010, ambayo ukijumlisha kura za wapinzani wote zinazidi zile za mshindi wa CCM, ni machache sana ukilinganisha na yale wapinzani waliyoshinda.

Kwa mantiki hiyo, kwenye majimbo ambayo sidhani kama yanazidi 20 mwaka huu ambapo zaidi ya chama kimoja cha upinzani kina mgombea, bado wanaweza kushinda 12 au 13 kati yake.

Naomba vyama vya UKAWA viweke nguvu kwenye majimbo yote, na yapo majimbo zaidi ya 200 ambayo makubaliano ya UKAWA yanafanya kazi. Haya machache yasiturudishe nyuma, maanna kwa hakika wananchi wanajua nini kitaamuliwa.

Hebu chukulia kwa mfano Masasi, ambapo makubaliano ya UKAWA ni kuwa NLD wagombee, lakini wananchi wamemkataa mtu wa NLD na kumtaka wa CUF.

Najua maamuzi ya vikao vya UKAWA yalizingatia mawazo ya wananchi, lakini naamini yapo baadhi ya maeneo mawazo ya wananchi yamekuja kuonekana baadae kuwa tofauti... yaheshimiwe
 
Back
Top Bottom