Bikirembwe
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 250
- 7
Kama kuna alosikilia na kuona tukio la Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano anaweza kukubaliana nami kuwa Mama Asha alitoa hotuba nzuri ilogusia mambo muhimu ambayo Umoja wa Mataifa unashughulika nayo kwa sasa na mchango wa Tanzania katika hilo.
Nia ya thread hii si kuijadili hiyo hotuba ila ni tukio lililofata, pale Spika alipomkaribisha Mheshimiwa John Chilligati atoe shukrani kwa mgeni wao kwa niaba ya Serikali na Bunge - kama kawaida ilikuwa kumpongeza lakini naona kama waswahili wanavyosema kuwa viungo vinapokuwa vingi huharibu mchuzi na kwa maoni yangu ndio ilivyotokea, kwani katika kutaka kuzidisha sifa na kumhakikishia Mama Migiro kuwa Watanzania wanamuunga mkono alimtoa wasi wasi kuwa anaweza kutembea "kifua wazi" kwani Watanzania wako nyuma yake.
Sasa ninalotaka muchangie ni jee hiyo ni sifa au kashfa na kama ni kashfa au kukosea hakutakiwa kuomba radhi? au ndio kuwa msamiati wa kumradhi haupo tena katika jamii ya kitanzania?