Chiligati Watanzania siyo mabwege!-Lusekelo blog | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chiligati Watanzania siyo mabwege!-Lusekelo blog

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Nov 1, 2009.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Chiligati Watanzania siyo mabwege!

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati amesema kitendo cha Rais Jakaya Kikwete, kutoa ardhi kwa wawekezaji si kuiuza nchi badala yake ni kukuza uchumi kupitia kilimo.
  [​IMG]
  Chiligati amesema kuwa kitendo hicho hakiwezi kuwa ni kuuza nchi, kwa sababu wawekezaji wanakodishwa mashamba na wala hawamilikishwi, hivyo wakiondoka hawaondoki nayo.

  Si kweli hata kidogo na ninadhani Bwana Chiligati anajua hiyo ni danganya toto. Mimi naona Chiligati, ambaye ni mkuu wa propaganda wa CCM anacheza na msamiati.

  Kukodishwa maelfu ya ardhi ya Tanzania kwa miaka 99 ni nini, kama siyo kuuza? Ikipita miaka hiyo, huo mkodisho utaendelea – kwa miaka mingine 99. Ni nini hiyo? Na WaTanzania ambao watakuwa vitukuu na vilembwe wa watawala wa leo, na ambao wengi wanaishi vijijini, wataenda wapi? Sidhani kama wote watakuwa mawaziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi au marais.

  Kwa mtu yeyote anayeifikiria na kuipenda nchi yetu, atagundua kuwa huu ni ubinafsi mbaya sana. Kwa nini tunafikiria kama kuku? Maana yake kuku anaangalia njaa yake pale pale.Akishiba basi umetoka hiyo. Kesho itajijua yenyewe.

  Wakati wa uhuru, miaka arobaini na iliyopita, Tanganyika ilikuwa na wananchi 12 milioni. Leo tupo 45 milioni. Wamezidi watu 30 na, milioni. Tukianza kuuza ardhi (mimi naona ni uhaini tu) na baada ta miaka 99 utakuwa na watu 70 milioni. Je,utawaweka wapi? Nchi yetu itakuwa ni ya manamba tu? Na waTanzania hawatakubali hiyo – zitapigwa tu!

  Ukiangalia historia kidogo watawala waliota, baada ya kuambiwa na wakoloni mambo-leo, kuwa bila Tanzania kubinafsisha viwanda vyetu hatuwezi kuendela. Tumebinafsisha, tena kwa bei chee, na sasa tumebaki tunang’aa macho.

  Juisi za embe na mananasi ‘zinatengenezwa’ nchini Saudi Arabia. Watanzania hawawezi kusindika juisi hizo. Nguo nzuri za pamba inayolimwa Shinyanga ‘zinatengenezwa’ Dubai. Watanzania hawawezi kushona nguo za pamba. Matusi hayo kwa Tanzania Bwana Chiligati! Inaonekana kuwa Watanzania hatuwezi kufanya lo lote.

  Sasa anasema, na hiyo ni sauti ya watawala wetu, kuwa nchi yetu bila kuwa na wawekezaji katika kilimo cha mashamba makubwa haiwezi kuendelea. Huu utumbo tutaendelea kusikia mpaka lini? Hizi fikira tegemezi za watawala wetu zitaendedea mpaka lini?

  Kujidharau gani huko kwa watawala, na kudharau waTanzania wenzao kuwa hawawezi kulima mpunga na ngano. Mpunga ni mpunga na ngano ni ngano. Kuna watumwa wa kimawazo (inferiority complex) ambao wanafikiria kuwa waarabu au wakorea wakilima mpunga unakuwa mzuri kuliko ule unaolimwa na mmatumbi huko Ifakara. Mtu mweupe akisema, hata upumbavu gani, anasikilizwa sana na watumwa hao wanaowahusudu watu weupe.

  Haya tusaidiane – tunapata maendeleo gani kutoa ardhi yetu kwa wakoloni ambao watawala wanawaita wawekezaji. Tunapata nini kutoka kwenye kashfa ya Loliondo. Eti shule moja na kiwanja cha ndege. Ni lini wamasai wa Loliondo waliiambia serikali kuwa wanataka kiwanja cha ndege?
  Tuambiwe faida tanayoipata au tutakayo ipata kwa kinadi ardhi yetu. Jamani kama hamna la kufanya, basi kuleni maraha tu. Lakini ardhi yetu muiache. Kama mtu hana la kufanya basi akae anywe chai. Siyo lazima aanze kuota cha kufanya. Ardhi yetu muiache!
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kuacha kulima kwa miaka 99, nakulima kwa kutumia jembe la mkono linakusaidia nini? wacha wapewe wakulima wakubwa wakiwemo wazalendo ofcourse...issue ni sera na implementation hilo la kutumia rasilimali ikiwemo ardhi haina kweri hata kidogo..lol
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hata Kariakoo sasa hivi wawekezaji wamekodisha viwanja na wanashusha majengo ya ghorofa... Inapendeza kufikiria hivyo na hata kuyaona majengo yamesimama lakini ukweli ni kwamba majengo hayo hayamsaidii mwananchi wa kawaida wala mazingira.. Kariakoo hakuna sewerage system, hakuna elevators, hivyo taka watu hutupa toka ghorofa ya 6, hakuna parking space, Residencial area yote imegeuzwa kuwa maduka na storage warehouses..huwezi panga nyumba ya Kariakoo ikiwa kipato chako ni cha kati (middleclass) kwa sababu kodi ni kubwa sana..

  Kifupi maendeleo ya Kariakoo, ni sawa sawa kabisa na maendeleo yanayotegemewa toka ktk Kilimo cha kukodisha ardhi kwa wageni...
   
 4. The Flycatcher

  The Flycatcher Member

  #4
  Nov 2, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaleyale ya kwa Bob Mugabe!
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160

  Tumempa ridha ya kusema hivyo, sio kosa lake ni kosa letu wenyewe, tusingempa ridhaa asingekuwa na forum ya kusema hivyo.

  Angalia hiyo red, umekosea kidogo hesabu, wakati wa uhuru tulikuwa 12,000,000 40 years later tuko 40,000,000 maana yake ni increase mara mbili na nusu katika miaka arobaini hivyo kwa miaka 99 population itakuwa 160,000,000 na zaidi. Na ardhi yetu haiongezeki iko vilevile na global warming inazidi kutuaffect jamani tuache utani.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwa maana rahisi kichwa cha habari cha thread ni kinyume cha hali halisi. Ni kwamba kweli sisi ni mabwege (at least wale walio-vote for him) na ndio maana imekula na itaendelea kula kwetu.
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  You couldn't have said better as you cant complain on a self inflicted injury
   
 8. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mkuu hapo umenena, huyu jamaa pamoja na wenzake akina Makalla, Komba, Makamba, Tambwe etc wanatuona sisi mabwege na ndio maana wanapata confidence ya kuongea chochote. Remember one time Mkuchika alisema hizi kelele za mjini tu lakn vijijini hakuna gazeti wala TV na wao wataendelea kuwa madarakabi milele. Uchaguzi wa juzi wa local government they swoop almost over 90 percent kwa nini wasituone MABWEGE!?
   
 9. A

  August JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  je baada ya lease kwisha , je tutamlipa ili aondoke kwa kuwekeza miundo mbinu , mazao ya kudumu kama miti , majengo etc au itakuwaje? tumia akili kaka, hapo kariakoo mfano, watu wengi lease yao iliisha wale waliokuwa na vibanda vya chini? je serikali ilichukua ardhi yao na kuiuza upya au wao wenyewe ndio wanawauzia hao wawekezaji? na hapo huyo mtu alikuwa na kajengo kadogo hivyo kununuliwa ilikuwa rahisi, sembuse huyo mwekezaji ambaye ataongeza dhamani maradufu, huo uwezo tutakuwa nao, si tutamwambia mzee bora yaishe tu we ongeza 999 years more ilimradi unalipa kodi na kutoa ajira kwa akina maganga na mkude, naona tutakuwa na jamuhuri ya wakorea ndani ya tanzania hapo baadae, we angalia maeneo ya Indira Gandhi, Asia Street, etc si ni kukaribia kuwa ni jamuhuria ya india ndani ya bongo, nao hao ni wachache tu, lakini tunaona wanavyo ichezea serikali yetu kama wao ndio milioni 30. maana ukipita maeneo hayo ni wao na maduka yao na mahali pakuabudia yao, makta zao , shule zao, mabenki yao, kukwepa kodi wao, mahospitali yao ukumbi mikubwa yao diamond jubilee na karimjee, yaani hapa inabidi tumshukuru mwalimu, maana sehemu hizi tusingekuwa tuna pita, chiligati na marafiki zake wangekuwa wanaenda kula biriani na kuuza nchi tu na watu wake. angalia hata wakati ule sisal estates zilikuwa za akina nani? angalia morogoro mjini inatawaliwa na nani?
  hivyo hii mikataba unatakiwa uangalie na mambo mengine, eg huyo mwekezaji baada ya miaka 10 au hiyo 99 atakuwa ni raia watanzania au hatakuwa? je nguvu yake ya kiuchumi itatudhuru vipi? kwa kumalizia inaweza kuleta hali kama ya zimbabwe maana hii inaitwa settlers economy, ambapo leo hii wale ma-settler wameleteleza zimbabwe kubsanwa na uingereza, sasa fikiria sisi tukibanwa tukawekewa vikwazo na korea huko mbeleni, macho yatatutoka kama mjusi anavyo banwa kwenye mlango.
  na ukumbuke mikataba ya madini ilianza hivi hivi, oh! itatoa ajira 200, sijui watalipa mrahaba, watalipa kodi blah blah kibao, leo hii hata hiyo kodi haionekani tunaunda tume baada ya tume hapo ni kwenye dhahabu, na tanzanite wakasema watafanya branding, sijui watai-process hapa sio india tena , yameishia wapi? mpaka balozi wa sa awambie jamani madini yawanufaishe wananchi. mimi ukiniambia angalau tumlete meneja wa shamba toka ulaya or what ever tumpe mshahara atufanyi kazi nitakubaliana. hata tumlipe 10,000,000 hata 20millioni pm na nauli ya kwenda kwao kila mwaka nitakubali na sio kutoa ardhi kwa mwekezaji. na tumpa nyenzo nitakuelewa.
   
 10. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Lusekelo, waTanzania ni mabwege.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  August,
  Mkuu nimekusikia sana yaani uko loud and clear!.. yaani hadi leo hatujajifunza kabisa.. mashirika kibao yanauzwa pindi muda unapokaribia kwisha na wageni hujisajili upya kwa miaka mingine 99. Ni mchezo unachezwa sana nchini hasa ktk ardhi. Hiyo miaka 99 nani kati yetu atakuwa hai?.. Hivi kweli hatufikirii kizazi cha kesho jamani kuwaachia nchi ya Upangaji..Nyumba za msajili zilikuwa za serikali leo hii ni wapangaji ndio wanaouza kwa marklet rate (bila kuweka senti yao) wakati serikali ikiambulia punje za pato zima la mpangaji.

  Hata Zimbabwe kiasili ardhi ilikodishwa kwa wazungu (settlers) kisha hawa hawa wakaja miliki ardhi hiyo baada ya nchi kujitenga na kuundwa kwa Rhodesia..
  Who knows 50 years from now historia inaweza badilika kabisa..Hao hao wawekezaji wanaweza kuwa na nguvu kiasi kwamba wakamnunua hata rais wa nchi (jambo ambalo lawezekana kabisa) na huyo rais akapitisha sheria ya kumiliki ardhi kwa wale wote wenye ardhi hizo.

  Mtanznaia leo anapangisha ardhi kwa shida na ndivyo ilivyotokea ktk nchi zote zilizotawaliwa. Tofauti na wenzetu, wao WAZAWA ndio waliwezeshwa kuwa wakulima kwani mkulima sii mwenye jembe ila mkulima ni yule mwenye ardhi... Tofauti ya msingi huu wa kiuchumi ndio maana hawa viuongozi wanafikiria kuwa mkulima ni yule mwenye jembe la kisasa na fedha pasipo kuthamini ardhi.. Kama kweli huyo mkulima wa Arabuni au Ulaya ni mkulima kweli kwa nini asiende kulima jangwani! ARDHI ndio tafsiri ya uhuru na watu wa nchi zote.
   
Loading...