Chiligati asikitishwa na kauli za Sitta

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Baadhi ya kauli hizo ni ile aliyoitoa wakati wa hafla ya uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Kanisa Katoliki Chang’ombe, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Sitta alisema ujasiri wake na maisha yake yanatokana na nguvu na ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Alisema nguvu hizo zimekuwa zikimwezesha kutekeleza wajibu wake kwa uhakika bila kuyumbishwa wala kuogopa kitu chochote.

Sitta ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akishambuliwa kwamba amewasaliti Watanzania kutokana na kuufunga mjadala wa kashfa ya Richmond, juzi akiwa mjini Songea, alikaririwa tena akisema alinusurika kuvuliwa uanachama CCM kutokana na ujasiri wake wa kusimamia ukweli.

Sitta alisema kauli kwamba alitaka kupokonywa kadi ya CCM kwenye vikao vya NEC mwaka jana na mwaka huu mjini Dodoma ni ya ukweli na kila mtu anajua. “Huo ni ukweli wenyewe, tatizo liko wapi? Maana kila mtu anajua, mimi sioni kama kuna siri hapa, na hili nitaendelea kulisema hata kama wenzangu hawataki,” alisema Sitta.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati, aliiambia Tanzania Daima jana kuwa, CCM imeshangazwa na kauli za Sitta wakati anapaswa kujiandaa kwa usuluhishi, alisema kwa kawaida vikao vya NEC na CC ni vya siri na mjumbe yeyote hapaswi kutoa siri za vikao hivyo.

“Ndugu yangu kweli nimemsikia, inasikitisha sana, lakini sina cha kusema na nakuomba uandike hivi kwamba Chiligati hana cha kusema kuhusu kauli za Sitta,” alisema Chiligati.

Akizungumzia kauli za Sitta, Msekwa kama ilivyokuwa kwa Chiligati, alisema hawezi kusema chochote kwani kamati yao ni ya CCM na inafanya kazi za CCM na si za CHADEMA. “Hii kamati ni ya CCM, si ya CHADEMA, ninyi watu wa CHADEMA mnaitakia nini? Hata kama Sitta anatoa kauli tata si kazi yetu, tuacheni jamani, mnaitakia nini CCM?” alilalama Msekwa

Source: Tanzania Daima

My take
Kamati ya Mwinyi itaweza kweli kuleta suluhisho ndani ya CCM na Msekwa alijuaje mwandishi aliyekuwa anamhoji ni wa Chadema?
 
Msekwa na Chilligati wote wameishiwa, hawana mpya. Mbona hawakukanusha habari zilizoandikwa magazetini mara baada ya kikao cha NEC cha mwaka jana na mwaka huu, ambapo magazeti karibu yote yaliandika habari za Sitta kutaka kupokonywa kadi yake na kwamba aliokolewa na JK.

The same comedian (Chilligati) baada ya kikao alitoka akijisifu kwamba Chama kitawashughulikia wale wote wanaojiita wapiganaji/wapambanaji wa ufisadi. Sasa leo anaona aibu kusema kusema ukweli?

Hawa jamaa huwa wanapenda kusema huko sirini na hawataki wananchi wajue nini kinatokea, halafu wakitoka kwenye vikao wanaanza kusema kupambana na ufisadi ni sera ya CCM na kumbe kulinda mafisadi ndo sera ya chama. Wakiumbuliwa ndo wanasema ooh hatuna cha kusema ila tumesikitishwa, mambo ya vikao vya NEC na CC ni siri, sasa kama ni siri, kwanini huwa wanaitisha Press Conference baada ya vikao kuisha? BS!
 
Mzee 6 hana lolote naye anapenda sana publicity aonekane ni mpiganaji.....hana jipya!
 
Masa

Hata mimi ananichanganya sana pamoja na wapiganaji wake! Ni lazima wachague kuwa moto au baridi lakini hawazezi kuwa vuguvugu.
 
Mzee 6 hana lolote naye anapenda sana publicity aonekane ni mpiganaji.....hana jipya!

Hali ni mbaya huko urambo, kwahiyo mzee wa watu anatafuta huruma kwa watanzania ili hata kama ikitokea ameshindwa ubunge kihalali, apate la kusema "Mapambano niliyokuwa nayaendesha na kuyasimamia ya vita dhidi ya mafisadi ndio wamesababisha nishindwe ubunge-si mmeona jinsi walivyopandikiza mtu wao na kutumia fedha haramu kuwaghiribu wapiga kura"

Na bado mwaka huu tutasikia mengi sana.
 
Hawa SSM wanashangaza umma wa watanzania. Hivi ni nani ambaye hadi leo hafahamu kuwa Mh. S. Sitta alitakiwa kupokonywa kadi ya uanachama ikimaanisha pia ni kuhitimisha uspika wake? Kwa nini wanamlazimisha Mh. Sitta afanya maamuzi ambayo ni kinyume na kanuni na taratibu za Bunge?? Sitta anafuata demokrasia kwa kuomba miongozo na taratibu za bunge, na kizuri zaidi ni mwanasheria. Hakuna kipindi ambacho kumekuwa na demokrasia Bungeni kama hiki cha Sitta. Ni mtu ambaye anelewa fika anachotakiwa kukifanya pale bungeni.

SSM ni vema wakae kimya tu, madhambi yao yatajitokeza moja baada ya jingine, hata kama action hazitachukuliwa maana wao ndio wameshika hatamu lakini angalao umma wa Watanzania wazalendo watapata habari a uozo wao. Keep it up Mzee Sitta. Hakuna cha kuomba msamaha fisadi yeyote. Kwanza mpatanishwe kwa kosa lipi au ugomvi upi?? Wewe ulikuwa unatekeleza wajibu wako kwa kuwapa wabunge demokrasia ya kujadili mijadala na kufikia muafaka. Wewe kazi yako pale ni moderation (kutoa miongozo, sheria, kanuni na taratibu) ya mijadala hiyo. Wasikuumizwe kichwa mzee wetu. Hata mimi ningekuwa mbunge ningekuwa upande wako. Long live Mzee Sitta.
 
Baadhi ya kauli hizo ni ile aliyoitoa wakati wa hafla ya uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Kanisa Katoliki Chang’ombe, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Sitta alisema ujasiri wake na maisha yake yanatokana na nguvu na ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Alisema nguvu hizo zimekuwa zikimwezesha kutekeleza wajibu wake kwa uhakika bila kuyumbishwa wala kuogopa kitu chochote.

Sitta ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akishambuliwa kwamba amewasaliti Watanzania kutokana na kuufunga mjadala wa kashfa ya Richmond, juzi akiwa mjini Songea, alikaririwa tena akisema alinusurika kuvuliwa uanachama CCM kutokana na ujasiri wake wa kusimamia ukweli.

Sitta alisema kauli kwamba alitaka kupokonywa kadi ya CCM kwenye vikao vya NEC mwaka jana na mwaka huu mjini Dodoma ni ya ukweli na kila mtu anajua. “Huo ni ukweli wenyewe, tatizo liko wapi? Maana kila mtu anajua, mimi sioni kama kuna siri hapa, na hili nitaendelea kulisema hata kama wenzangu hawataki,” alisema Sitta.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati, aliiambia Tanzania Daima jana kuwa, CCM imeshangazwa na kauli za Sitta wakati anapaswa kujiandaa kwa usuluhishi, alisema kwa kawaida vikao vya NEC na CC ni vya siri na mjumbe yeyote hapaswi kutoa siri za vikao hivyo.

“Ndugu yangu kweli nimemsikia, inasikitisha sana, lakini sina cha kusema na nakuomba uandike hivi kwamba Chiligati hana cha kusema kuhusu kauli za Sitta,” alisema Chiligati.

Akizungumzia kauli za Sitta, Msekwa kama ilivyokuwa kwa Chiligati, alisema hawezi kusema chochote kwani kamati yao ni ya CCM na inafanya kazi za CCM na si za CHADEMA. “Hii kamati ni ya CCM, si ya CHADEMA, ninyi watu wa CHADEMA mnaitakia nini? Hata kama Sitta anatoa kauli tata si kazi yetu, tuacheni jamani, mnaitakia nini CCM?” alilalama Msekwa

Source: Tanzania Daima

My take
Kamati ya Mwinyi itaweza kweli kuleta suluhisho ndani ya CCM na Msekwa alijuaje mwandishi aliyekuwa anamhoji ni wa Chadema?[/QUOTE]

Tanzania Daima ni La Chadema
 
mimi sasa hivi automatically nikiona habari yenye kichwa kinachomhusu SITTA siitilii manani kama zamani najua ni usanii tu
 
Sitta must know that "YOU CANNOT EAT YOUR CAKE AND STILL HAVE IT"
 
Wote wanajaribu tu kuwa karibu na keki ya taifa. Hakuna anayesukumwa na maslahi ya nchi maana muda wa kujipambanua baina ya mbomoa nchi na mjenga nchi ulishapita.

Lakini kipi kipya kilitegemewa? Wadanganyika bana hawaeshi kunishangaza.
 
Six katuwezaa sanaa kwa usaniii wakee.. huyoo jamaa anamtishaa nyau kupata publicity zaidii..

Akikumbuka sherehe yake ya ndoa kutimiza miaka 40 na mafanikio aliyopata kutokana na nafasi za uongozi ndani ya taasisi yao CCM kwa kulindana na mfumo unaochochea kulemaa mawazoo na kuabuduu nafsii binafsi zaidii kulikoo ummaa hana jipyaaa...

Kupititia Richmond saga tumewaelewaa vyema masilahi yao ndo muhimuuuu..
 
Tusubili uchaguzi mkuu ujao tuone wananchi watasema nini juu ya hao wote, akiwemo 6. Zingatia kwamba nguvu ya fedha ziwe chafu au la, imepunguzwa na rungu la sheria ya gharama za uchaguzi itakayosainiwa na mhe. siku si nyingi zijazo. Hivyo, matumaini aghalabu ya kupata viongozi na wawakilishi wasafi wa wananchi itaongozeka.
 
Hawa SSM wanashangaza umma wa watanzania. Hivi ni nani ambaye hadi leo hafahamu kuwa Mh. S. Sitta alitakiwa kupokonywa kadi ya uanachama ikimaanisha pia ni kuhitimisha uspika wake? Kwa nini wanamlazimisha Mh. Sitta afanya maamuzi ambayo ni kinyume na kanuni na taratibu za Bunge?? Sitta anafuata demokrasia kwa kuomba miongozo na taratibu za bunge, na kizuri zaidi ni mwanasheria. Hakuna kipindi ambacho kumekuwa na demokrasia Bungeni kama hiki cha Sitta. Ni mtu ambaye anelewa fika anachotakiwa kukifanya pale bungeni.

SSM ni vema wakae kimya tu, madhambi yao yatajitokeza moja baada ya jingine, hata kama action hazitachukuliwa maana wao ndio wameshika hatamu lakini angalao umma wa Watanzania wazalendo watapata habari a uozo wao. Keep it up Mzee Sitta. Hakuna cha kuomba msamaha fisadi yeyote. Kwanza mpatanishwe kwa kosa lipi au ugomvi upi?? Wewe ulikuwa unatekeleza wajibu wako kwa kuwapa wabunge demokrasia ya kujadili mijadala na kufikia muafaka. Wewe kazi yako pale ni moderation (kutoa miongozo, sheria, kanuni na taratibu) ya mijadala hiyo. Wasikuumizwe kichwa mzee wetu. Hata mimi ningekuwa mbunge ningekuwa upande wako. Long live Mzee Sitta.

Umelonga kitu watu walinganishe bunge la Msekwa na hili la Sitta tofauti ni kumbwa mno wakati ule Msekwa alikuwa akionyesha wazi u CCM na alikuwa hata hahoji hoja zinazoletwa bungeni kama anavyofanya Sitta ndiyo maana wana CCM wanamwona Sitta kama anawasaliti wakati anasimamia kanuni za bunge enzi za Msekwa nakumbuka hata sauti yake ilivyokuwa inatia kinyaa "wanaokataaa waseme hapana wanaokubali waseme ndiyoooo WAMEPITAAAA" upu*&^%%()&*)*zi
 
Jamani 6 anajitahidi sana, kupambana na Mafisaadi kunahitaji kujipanga mno! siyo kukurupuka kama alivyofanya Lyatonga Mrema kaishia kuwa kituko tu kwa watanzanaia.
6endelea Baba......
Kwanza 6alisema yeye anasimamia ukweli hakusema jambo lolote kuhusu kamati ya Mwinyi, sasa Chiligati yeye anaweweseka nini??
 
Back
Top Bottom