Chiligati Apata Wakati Mgumu Maswa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chiligati Apata Wakati Mgumu Maswa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Feb 4, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  HALI si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu, baada ya viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho wilayani humo kutakiwa kuachia ngazi kutokana na kuendeleza migogoro ya mara kwa mara na kukidhoofisha.

  Hayo yamejitokeza juzi katika kikao cha Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo kilichohudhuriwa pia na viongozi wa ngazi za juu wa Mkoa wa Shinyanga chini ya Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Kapteni John Chiligati, kilichofanyika katika ukumbi ofisi za chama hicho, mjini Maswa.

  Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao, zilisema kuwa Chiligati ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, alitaka kufahamu kilichosababisha wakakosa viti vya ubunge katika majimbo ya Maswa Mashariki na Maswa Magharibi katika uchaguzi mkuu uliopita.

  Ndipo aliposimama Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Maswa, Jeremiah Shigalla na kueleza kwamba kulikuwa na usaliti uliofanywa na baadhi ya watendaji wa chama hicho na wanachama kwa kukiunga mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hususan Katibu wa UWT wilayani humo, Nuru Mselemo na hivyo kupendekeza atimuliwe.

  Pia waliendelea kumtupia lawama Mselemo kuwa ndiye anaendeleza migogoro ndani ya chama hicho ambaye anatuhumiwa kuchakachua jina la Pili Lameck, katika nafasi ya udiwani wa viti maalum ambaye alishindwa kupata nafasi hiyo licha ya kuongoza kwa kupata kura nyingi katika mkutano mkuu wa UWT wilayani humo.

  Wakati tuhuma hizo zikielekezwa kwa Katibu huyo wa UWT baadhi ya wajumbe walipinga maelezo hayo akiwemo Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Bakari Mbonde, ambaye alieleza wazi kuwa migogoro ndani ya chama hicho wilayani humo, inasababishwa na Mwenyekiti wa CCM, Peter Bunyongoli, pamoja na Katibu Mwenezi, Jeremiah Shigala, hivyo kupendekeza waondolewe.

  “Baada ya kumtuhumu kwa muda mrefu Mselemu, wajumbe wengine tulikataa kwani tunajua chanzo cha wananchi na wanachama kukichukia chama chetu ni hawa viongozi wawili wa wilaya ambao ni Mwenyekiti, Bunyongoli na Katibu Mwenezi, Shigala,” alisema mzee Bonde.

  Walisema viongozi hao wamekigeuza chama kama kikundi cha watu binafsi, jambo ambalo limezua mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hata kushindwa kufanya kazi na makatibu wa CCM wanaoletwa wilayani humo.

  Hata hivyo Chiligati alipata wakati mgumu kujibu sababu hizo, lakini aliahidi kwamba angeyachukua mapendekezo hayo na kuyafikisha katika ngazi ya taifa.

  Katika hatua nyingine, Chiligati alishindwa kuhutubia mkutano wa hadhara uliondaliwa na chama hicho katika viwanja wa MADECO kutokana na wananchi kutohudhuria mkutano huo.

  Chiligati ambaye alipaswa kuhutubia mkutano huo majira ya saa 10:00 jioni kulingana na matangazo yaliyokuwa yakitolewa kupitia vipaza sauti kwenye gari lililozunguka mitaa yote ya mji wa Maswa, hakuna watu waliojitokeza kuhudhuria.

  Ilipofika majira ya saa 11.56 jioni ambapo mwandishi wa habari hizi alikuwepo katika viwanja hivyo, kulikuwa na watu wanne tu wakiwa eneo la mkutano, huku wakilalamika kutokuwa na taarifa ya mkutano huo..

  Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja alipotafutwa kuzungumzia kitendo cha Chiligati kutofika eneo la mkutano alisema kuwa walipata taarifa ya misiba mitatu, hivyo watu hawakuweza kuhudhuria, ndiyo maana waliahirisha.

  Source: Tanzania Daima ya leo ukurasa wa tano
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Chiligati hauwezi moto wa wasaliti waliomo ndani ya chama,na akumbuke kuwa chama huanguka kutokana na viongozi na wanachama ndani ya chama kuchaguliwa viongozi na ccm taifa
  kwa hiyo ni vizuri chama cha mapinduzi kuanza kubadilika ktk mitazamo yao na ikiwezekana waanze na kumwenguwa makamba na akifuatiwa na chiligati mwenyewe na hizo nafasi zishikwe na wasomi walioiva kisiasa na sio kipropaganda

  msema ukweliiii hapendwiiii daimaaaa:clap2:
   
 3. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mzimu wa damu walioimwaga arusha,kuiba mali za wanyonge+wiz wa kula ndivyo vinawasumbua na wataendelea kutaabika,nawashauli wana ccm wahame mapema kabla aza haijawakuta
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Asomaye na afahamu!
  Hawa jamaa hawajaelewa bado kuwa hawatakiwi na mtu eeh?...sijui wanasubiri waone dalili gani!
  How come unategemea uwaone watu mkutanoni, wakati gia yako ya kawaida ni kwenda wakati wa kampeni na Tisheti na kofia?...
  Ukitaka kuwahutubia kikawaida ni lazima pia ulete tisheti na kapelo!...mwosha huoshwa!
   
 5. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakimaliza kutimuana huko wakatimuane na Mwanza na Musoma......wao wakishindwa kwny kura wanashikana uchawi eti wanahujumiwa au eti tumewakopesha wapinzani jimbo!....wanafikiri wananchi wa leo ni wale wale wa enzi za uhuru!
   
 6. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mshaanza kugawanyika wenyewe, safi sana :clap2: !!!
   
 7. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu?
   
 8. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hili ni fundisho. Safi sana watu wa maswa.:clap2:
   
 9. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nani yuko tayari kusimama juani kuskiliza porojo, huku hana uhakika wa kunywa hata chai, maana bei ya sukari sasa inamnyima mtu wa chini kunywa chai.
  watatafuta sababu nyingi sana lakini ule mwisho waja.
  Hakuna ca misiba wala nini.
   
 10. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa umenimaliza
   
 11. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Siku hizi wasukuma wameelimika wasifikirie ni wale mamami wa wazamani kwamba unampeleka lupango ukimsalimia anakwambia ndoho tabu wakati anaenda kunyea debe bado ndugu zetu wa kusini kama lindi na mtwara nao wanatakiwa wapewe elimu ya people power ili wawatose wapiga porojo kama kina chiligati na Makamba:sad::embarrassed::embarrassed:
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Lakini mimi nina wasiwasi na hii story kidogo. yaani gari lizunguke siku nzima kuhamasisha watu waje kwenye mkutano halafu kwenye uwanja kuwe na muziki wasipatikane hata wale ambao wamezoea kushangaa?
   
 13. Mazee

  Mazee Senior Member

  #13
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 6, 2007
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wadau wa Shinyanga Hizi Khabari zina ukweli ndani yake,,,,
  verification please..............
   
Loading...