Chiligati apasua mafisadi CCM asema Mwakani mwisho wa mafisadi dagaa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa na mbunge wa Manyoni Mashariki John Chiligati


Thursday, 12 May 2011 19:11 newsroom


* Mwakani mwisho wa mafisadi dagaa
* Asema CCM itabaki na waadilifu tu
NA BASHIR NKOROMO, SINGIDA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kitatumia uchaguzi mkuu wake kuwaengua viongozi wote wasio waadilifu na mafisadi. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika baadaye mwakani na kwamba, utatumika kusafisha masalia ya watuhumiwa wa ufisadi, ambao watakuwa bado hawajajiondoa. CCM imewataka watuhumiwa wa ufisadi kujiondoa wenyewe, vinginevyo nguvu itatumika wakati wa kikao cha NEC ya CCM, kinachotarajiwa kuketi Julai au Agosti, mwaka huu. Hata hivyo, CCM imesema kuwa ikilazimu kinaweza kuitisha mkutano wa dharura na kutekeleza agizo hilo kwa maslahi ya Chama na Watanzania kwa jumla. Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati, wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoani hapa katika Ukumbi wa
FDC, jana. Chiligati, ambaye alikuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi katika Sekretarieti iliyopita, alisema CCM imedhamiria kuwasafisha wanachama na viongozi wasio waadilifu. Alisema, hiyo ni miongoni mwa mikakati ya wazi iliyopitishwa na CCM mjini Dodoma, wakati ikiwa katika mchakato wa kujivua gamba kulikosababisha Kamati Kuu na Sekretarieti yote kujiuzulu na kuundwa mpya.
Chiligati alisisitiza kuwa watuhumiwa wa ufisadi ndani ya CCM wajitafakari wenyewe na kuchukua hatua, kinyume na hapo watang’olewa. Pia, alisema ikionekana muda wa kufikia kikao kingine cha NEC ni mbali, mkutano wa dharura unaweza kuitishwa ili hatua za haraka zichukuliwe ili kukiacha Chama kikiwa safi mbele ya jamii. Alisema CCM imedhamiria kuwa na wanachama na viongozi wenye maadili safi mbele ya jamii na ndiyo, msingi wa kujivua gamba ili kusafisha wachafu. “Hatutawavumilia wanachama na viongozi wachafu wanaotumia mgongo wa CCM na vyeo walivyonavyo ndani ya Chama na serikali kujilimbikizia mali,” alisema.
Alisema ili kufikia malengo hayo, NEC ilipitisha uamuzi wa kuwepo kamati maalum ya udhibiti ili kurejesha nidhamu ndani ya Chama na kwamba, itakuwa na jukumu la kuzuia mpasuko wakati wa uchaguzi. Kuhusu kura za maoni, alisema zitakuwa zikipigwa na wananchi mapema ili kupata muda wa kusikiliza malalamiko, rufani, uchaguzi uliopita CCM haikuwa na muda wa kutosha ndiyo sababu zilijitokeza kasoro nyingi.
Pia, alisema uchaguzi huo utakuwa na uchujaji wa awali, na kwamba si kila anayechukua fomu atagombea, kwani itakuwa nafasi moja kwa watu watatu, anayeshinda lazima apate nusu ya kura.
Katika hatua nyingine, Chiligati aliongeza kuwa CCM imepitisha utaratibu wa kutoruhusu mwanachama wake kuwa na vyeo vingi kiutendaji, kwani hali hiyo imesababisha kasoro nyingi.
Chiligati yupo mkoani hapa katika ziara ya kuitambulisha Sekretarieti mpya ya CCM, ambapo amefuatana na Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Juma Abdallah.
 
Sorry is he a minister ? Hope he's not coz I mix him and mkuchika..names and traits
 
Moja....mbili.....tano.....kumi wasikilizaji hii ni hatari kama mkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa taifa uko hivi kuna siku tunakoelekea watahutubia madereva wao.

 
huu ni mkutano au kikao? cz iyo idadi ya watu aingi akilini kwangu kama uwo ni mkutano
 


Rais Kikwete akimnadi Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi wa Richmond na kujilimbikizia mali



Rais Kikwete akimnadi Rostam Aziz (Kagoda) mtuhumiwa wa ufisadi wa Richmond na Dowans



Rais wa nyuma ya pazia Salma Kikwete akimandi Mzee wa vijisenti mtuhumiwa wa ufisadi wa Rada na ndege ya rais


Rais Kikwete akinmadi Amos Makala aliyetimuliwa kwa kutofaa kumshauri
 
ukiangalia kwa makini hiyo picha ya Chiligati akiwa Manyoni, sidhani kama hao wananchi walikuwa wakimsikiliza kwa makini, ingawe wengine wamevaa sare za CCM haimaanishi they are supporters, kuna babu ameshika kichwa nadhani anatafakari upupu unaosemwa hapo....
 
jamani jamani CCM mwogopeni Mungu na mjue Mungu hata siku moja halewi yaani mnapambana na mafisadi wakati rais na mwenyekiti wa CCM na mkewe wanawanadi mafisadi?? We Chiligati na Nape mbona mwapambana na ukuta?? Mmetumwa au mnataka mtolewe kafara??? Na wewe Chilly sause mbona watu unaowahutubia hawaonekani na waliopo hawana mpango wa kukusikiliza?? Pole baba Aibu
 
Ile singo ya siku 90 ime-expire, wanakuja na stori ya mwakani ndo wataondoa mafisadi...he!he!he! Kweli chama cha magamba hali ni mbaya
 
Siasa ngumu kweli kweli! Makeke yale yote ya siku tisini jamaa ameshindwa ku-garner support kubwa hata mashambani? Safari hii wenye mabasi wameogopa kunyofolewa magamba hawajatoa ofa ya kusomba waimbaji kwenye mikutano.
 
Ccm nao mipango yao ni kama ya Tanesco leo hili kesho lile hawaeleweki,wizi mtupu
 
Ccm nao mipango yao ni kama ya Tanesco leo hili kesho lile hawaeleweki,wizi mtupu kwani siku 90 zilipotelea wapi?,acheni kucheza na akili za Watanzania kila siku ujingaujinga tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom