Chiligati aonja machungu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Waziri Chiligati aonja machungu

2008-09-18 10:59:41
Na Richard Makore na Hellen Mwango

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kapteni John Chiligati, juzi jioni alijikuta katika wakati mgumu, baada ya wanakijiji cha Kwembe nje ya jiji la Dar es Salaam kuanza kumsomea vifungu vya sheria ya Ardhi na kumtaka asiwaone kama watu ambao hawajasoma.

Waziri Chiligati alikumbana na hali hiyo kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho, uliolenga kuwatangazia wanakijiji hao kwamba wanatakiwa kuhama ili kupisha ujenzi wa hospitali kubwa na Chuo cha Udaktari tawi la Muhimbili.

Baada ya Chiligati kutoa kauli kwamba wananchi watake wasitake watahama, ndipo mmoja wa wanakijiji hao aliposimama na karatasi na kuanza kumsomea Chiligati vifungu vya sheria vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza.

Mwanakijiji huyo aliyesoma vifungu hivyo, Baton Mwamboneke, alimfanya Waziri Chiligati kupigwa na butwaa na baada ya hapo wananchi wengi walinyanyuka kila mmoja akitaka kumuonyesha kwamba wao sio wajinga kama alivyodhani.

Kabla ya sakata hilo, baadhi ya wanakijiji walikuwa wamejiandaa kumsomea Waziri Chiligati vipande vya magazeti vilivyoandika kuhusu umuhimu wa serikali kushauriana na wananchi kabla ya kuwanyang\'anya ardhi yao.

Mwanakijiji mwingine, Rashid Athumani Makala, alimuuliza swali Waziri huyo kwamba yeye (Chiligati) ananenepa, lakini wao (wanakijiji) wanakonda na kuambiwa waondoke eneo hilo je, anataka waende wapi?

``Wewe bwana unataka twende wapi, mbona kuna mapori mengi ambayo hayakaliwi na watu, kwa nini serikali isiyachukue hayo?`` Makala alimuuliza Chiligati, ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza katika mkutano huo bila kumwogopa Waziri Chiligati na polisi waliokuwepo, mwanakijiji mwingine, Richard Munusi, alimuhoji Chiligati kwamba kama lengo ni kusogeza huduma za jamii kwa wananchi, mbona wao wanaondolewa?

Munusi alisema Serikali inatumia nguvu nyingi kuwaondoa wananchi katika maeneo ambayo tayari wameshayaendeleza na kuwa mazuri, lakini haiyahitaji mapori yaliyoko kwa ajili ya miradi inayodai ni ya wananchi.

Akijibu hoja zilizotolewa na wanakijiji hao, Waziri Chiligati alitoa majibu yalioonekana kuwakatisha tamaa wananchi hao kwa kuwaeleza kuwa watake wasitake wataondoka katika eneo hilo.

Alisisitiza kuwa cha msingi wanachotakiwa kujiuliza ni namna gani watakavyoondoka.

Alisema wanakijiji hao wanajidanganya na kusoma kwa mbwembewe kwa lugha ya Kiingereza vifungu vya sheria ya ardhi wakidhani hiyo itawasaidia wasiondolewe.

Aliwaambia kuwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania, ardhi ni mali ya Serikali na muda wowote ikihitajika kwa ajili ya kuweka miradi ya jamii inaichukua bila masharti yoyote.

Hata hivyo, wananchi hao walipinga kauli yake hali iliyozua zogo huku wakimuuliza nini maana ya Serikali.
Wanakijiji hao walioonekana kukatishwa tamaa na majibu ya Chiligati, walisema wanavyojua wao, Serikali ni wananchi na wananchi ndiyo wao sasa iweje Waziri huyo atumie ubabe na kauli za kuwakatisha tamaa katika zoezi la kuwaondoa katika maeneo yao.

Chiligati aliwasili katika eneo hilo juzi saa 9.45 alasiri na kuondoka saa 11.45 jioni baada ya mkutano huo na kuwaacha wanakijiji wakiwa wameduwaa kutokana na kukatishwa tamaa na majibu yake.

SOURCE: Nipashe
 
Siku moja niliwahi kumuambia mwalimu wangu wa general studies kipindi hicho nikiwa chuoni kuwa,"It's we with this corrupted mind who will be capable to live in this corrupted world called democratic world.Najua kwa wale walioishi katika enzi za chama kimoja kama hao wakina chiligati na ndugu yake makamba hawawezi kuyavumilia hayo.Ila ndo nawaonea huruma mana watu ndo wanazidi kuchanganyikiwa na huu mchanganyiko wa democracy
 
Jamani hivi hiki kijiji cha kwembe kiko sehemu gani? Mbona ardhi ambayo haikaliwi na watu ni nyingi tu, imejaa kila mahali, ukitoka bunju hapo hadi bagamoyo hakuna watu, ukitoka mbagala tu hapo mbele hakuna watu, kwa nini wasiendeleze maeneo hayo na badala yake wanakimbilia sehemu ambayo watu wanaishi?
 
How do we react to show this government idiots that we have our rights and they should respect that and not giving us orders like school kids ! in our country or they
think its theirs only ? or they believe they own us ?
 
Demokrasia, kama alivyosema Thomas Jefferson, inaweza kufanya kazi tu kama watu wameelimika. Naona watu wanawabana hawa plutocrats mpaka wanashindwa a logical argument wanaanza kutumia miguvu na ku invoke eminent domain.

And then we have the nerve to claim that we embrace the free market.
 
uzuri mmoja chini ya mwalimu nyerere watu walisoma na kwenda jeshini! akina makamba, kingunge na wengine wanaota zile zidumu fikra sahihi za kikwete. hawakujua hata julius alifahamu kwa kuelimisha watu, kuondoa ukabila alikuwa anaujua mwisho fika wa haya yote? mapunguani kama akina makamba watateseka sana na mfumo wao usiotelezeka
 
With the same guy (chilly-gati) at the frontline (vita vya magamba), ccm is very likely to lose their own battle!
 
Back
Top Bottom