barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,863
Asilimia 56 ya wakazi wa mkoa wa Dodoma wamedumaa kiakili kufuatia kukosekana kwa chakula hali inayotajwa kuchangia pia wakazi wa mkoa huo kuwa ombaomba.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Gallawa anasema pamoja na mkoa huo kuongoza katika uchaguzi Mkuu mwaka jana lakini umekuwa nyuma sana katika huduma za jamii zikiwemo Lishe, Elimu na Maabara.
Hivi karibuni mkoa huu umeripotiwa kukumbwa na njaa kali hasa katika wilaya ya Chamwino kata ya Majereko ambapo wakazi wake walilazimika kutumia wadudu aina ya viwavi jeshi kama chakula.
Katika kikao cha Halmashauri kuu ya Mkoa huu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkuu wa Mkoa huu luteni Mstaafu Chiku Galllawa amethibitisha hali hiyo.
Chanzo: ITV