Chiku Abwao mbunge wa CHADEMA afyatuka uchaguzi wa udiwani manispaa ya songea

Mar 23, 2012
64
13
Na Stephano Mango, Songea

WANANCHI wametakiwa kuwa makini katika kuzisikiliza sera na ilani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ili waweze kuchukua hatua stahiki katika Uchaguzi mdogo wa madiwani na ubunge jimbo la Arumeru Mashariki unaotarajiwa kufanyika aprili mosi mwaka huu.


Wito huo ulitolewa jana na Mbunge wa Vitimaalum na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwalo wakati akihutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni wa kuziba nafasi wazi ya udiwani Kata ya Lizaboni Manispaa ya Songea

Abwalo alisema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndicho chama imara ambacho kimesimamisha wagombea wanaokubalika na wenye uwezo mkubwa wa kuielezea na kuitekeleza kwa kivitendo ilani yake ya uchaguzi na sera za chama hicho.

Alisema muda uliobaki unawatosha wananchi kutafakari kwa umakini na kuchukua hatua madhubuti ya kuwachagua wagombea wa CHADEMA ili wawe viongozi katika nafasi za ubunge, udiwani na urais kwa maslahi ya Watanzania wote.


Alisema Chedema ndicho chama chenye dhamira ya kweli ya kuwakomboa Watanzania wote katika lindi la umasikini, ujinga na maradhi hivyo wananchi kuweni makini sana na uchaguzi huu mdogo kwani Chama cha Mapinduzi hakina jambo jipya watakalowafanyia wananchi kwasababu kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaongoza bila kuleta tija.

Alisema kuwa wapiga kura wanatakiwa kuwa makini katika kuwatambua wagombea ambao watakuwa na uwezo wa kusema na kutenda mara watakapochaguliwa hivyo ni vyema kufahamu sifa na matendo ya kila mgombea ili siku ya uchaguzi waweze kufanya maamuzi sahihi.

Alisema uchaguzi huu mdogo ni wa muhimu sana kwani ni uchaguzi wa kuwakataa kikamilifu wagombea mafisadi, walaghai na watoa rushwa hivyo wananchi mnawajibika kuwachagua viongozi wenye uadilifu mkubwa ambapo wagombea hao wanapatikana katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Alisema kura yako ina thamani kubwa sana katika maisha ya watanzania na iwapo mkiipoteza kwa kuchagua kiongozi kwa ushabiki mjue mmepoteza fursa ya kupata barabara, maji, hospitali na huduma nyinginezo muhimu za kijamii.

Aliongeza kuwa CCM imeshindwa kuwakomboa Watanzania katika lindi la umaskini, maradhi na ujinga katika kipindi chote cha miaka 50 ya uhuru hivyo katika uchaguzi huu ni vema Watanzania wakaacha ushabiki usio na faida ambao mwisho wa siku ni kuongezeka kwa ugumu wa maisha.

Awali Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime alisema kuwa wazee nchini wanatakiwa kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chenye malengo ya kuleta ukombozi kutoka mikononi mwa Chama cha Mapinduzi ambacho kimewanyonya watanzania kwa muda mrefu na kuwafanya maskini

Fuime alisema kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi imeshindwa kuwajali wananchi ,wakiwemo wazee kwa muda mrefu kwa kushindwa kuwapatia huduma stahiki za jamii na kuwasababishia kuona maisha ya uzeeni kama ni hatari ambayo inapaswa kuogopwa

Alisema kuwa katika nchi nyingine wazee wanaheshimika na wanapewa huduma za jamii bure ikiwemo matibabu na pensheni kwa wazee bila kujali kuwa ulifanya kazi serikali kwani mchango walioutoa katika ujenzi wa taifa walipokuwa vijana unatosha kuwaenzi wanapokuwa wazee

Alieleza kuwa Serikali imeshindwa kuwaheshimu watanzania kutokana na matendo yao katili dhidi ya wananchi kutokana na kuwapandishia gharama za maisha kila kukicha,kushindwa kutekeleza ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania,kuwatoza kodi nyingi huku wakishindwa kutoa huduma stahiki kulingana na kodi zinazotozwa kwa wananchi

“Ili kufanya mabadiliko katika nchi hii ni lazima wananchi waamue kuchukua hatua za kuzisikiliza sera za Chadema na kujiunga nacho ili kuweza kuleta ukombozi stahiki mara uchaguzi wa Serikali za Vijiji,Mitaa na katika uchaguzi mkuu wa Madiwani,Wabunge na Urais muda utakapofika”alisema Fuime

Alisema kuwa ukimya wa wananchi ndio unaowapa kiburi viongozi wanaotokana na Ccm hivyo ili kuonyesha thamani ya mpiga kura katika nchi hii tumieni Chadema kama fursa stahiki ili kuweza kupata viongozi makini katika kufuatilia raslimali za umma kwa maendeleo ya wote

Alieleza zaidi kuwa kutokana na ukiburi wa viongozi wa Serikali kwa kutoogopa nguvu ya umma wanaendelea kuwadhurumu wananchi kwa kuwakandamiza katika mambo mengi na kuwafanya wananchi kuwa na maumivu makali ya maisha na kushindwa kuwa na uhakika wa kuishi kesho kwani kila kukicha ni afadhari ya ugumu wa maisha uliokuwepo jana

Naye mgombea Udiwani kupitia Chadema Alanus Mlongo akiomba kura kwa wananchi alisema kuwa mara atakapochaguliwa atashirikiana na wananchi wa Kata hiyo ili kusaidiana kuleta maendeleo stahiki na kwamba atatumia maarifa na mbinu zake kwa ajili ya kuleta maendeleo katika kata hiyo.

”Ninachowaomba wananchi wa Kata ya Lizaboni mnipe kura zote Aprili Mosi mwaka huu. Hakika dhamira yangu ni kuwasaidia na haitabadilika kamwe, maana wananchi wenyewe wananifahamu uwajibikaji wangu katika jamii nilipokuwa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ”,alisema. Mlongo

Pia, aliwaasa wananchi wa eneo hilo, kutodanganyika na maneno yanayotolewa na wapinzani wake, kwa kuwa maneno si vitendo na kwa muda mrefu wameshindwa kutimiza ahadi yao kutokana na dhamira zao kuwa mbaya katika kuwatumikia wananchi
 
  • Thanks
Reactions: GIB
Tanx kwa info, mapambano yanaendelea na tarh 1 ndio siku ya kuwaonesha magamba kuwa haturidhiki na uongoz wao.
 
Asante Mango, wewe mwanahabari siku nyingi ulikuwa wapi kujiunga JF siku zote, karibu sana!!!
 
Namkubali sana Chiku Ni shupavu na mpiganaji kweli kweli nafikiri anfaa sana kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA.
 
kila la her Stephano Mango natumai utaendelea kutujuza yanayojiri mpaka tar 1, thanx a lot brother.
 
Back
Top Bottom