Chiku Abwao Chadema aitikisa CCM Iringa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
DSCF7454.JPG
DSCF7486.JPG
DSCF7440.JPG
DSCF7464.JPG
DSCF7434.JPG
DSCF7430.JPG


Katibu wa chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo akimkaribisha mbunge Chiku Abwao leo
CHADEMA cha demokrasia na maendeleo (chadema) wilaya ya Iringa vijijini kimeanza kukibomoa chama cha mapinduzi (CCM ) baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi kata ya Luhota na mjumbe wa kamati ya utekelezaji CCM wilaya ya Iringa vijijini Sihuna Kapalampya kuhamia Chadema na kuwa mwenyekiti mpya wa Chadema kata ya Luhota .


Kapalampya amejiengua CCM na makada wengine wa chama hicho na kuanzisha ofisi ya mpya ya Chadema katika kata hiyo ya Luhota .


Kapalampya alisema kuwa sababu ya kukihama chama tawala ni kutokana na viongozi wa serikali ya CCM kwenye kata hiyo kuendelea kukumbatia vitendo vya ufisadi na kutafuna fedha za pembejeo za kilimo zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 12 ambazo wakulima wa kata hiyo hawakunufaika na pembejeo hizo zaidi ya viongozi wa serikali ya CCM .


Akiwapongeza viongozi waliochaguliwa na makada hao wa CCM waliojiunga na Chadema na kufungua ofisi ya kwanza na Chadema vijijini ,mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe.Chiku Abwao (Chadema) alisema kuwa wakati wa ukombozi wa kweli kwa watanzania umefika na kuwa hali ya wananchi wa vijijini kuanza kuichukia serikali ya CCM umeanza katika kata hiyo ya Luhota jimbo la Kalenga linaloongozwa na mbunge wake Dkt Wiliam Mgimwa (CCM).


Mbunge Abwao aliwataka wananchi wa vijijini kutokubali kutishwa na CCM na kuwataka kuendelea kukihama chama hicho cha CCM na kujiunga na Chadema chama chenye malengo ya kweli ya kuwakomboa watanzania.


Hata hivyo aliwataka wananchi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Chadema ili kuhakikisha kuwa Chadema kinaendelea kuwa na wanachama zaidi jimbo hilo na kuwa hivi sasa mkakati wa Chadema ni kuwa na nyumba 20 tofauti na CCM ambayo ina nyumba 10
 
Ha ha ha ha hao watu hata kumi (10) hawafiki wewe ndio unaita "kutikisa"?
 
Safi sana mama,Iringa tunakukubari,wamebaki watu wa kijijini tu kuelimika na wajinga wachache mjini,ila ukombozi umefika dhidi ya CHADEMA kuwakomboa wananchi
 
safi sana mpiganaji wetu mheshimiwa Chiku Agwao,endelea kukiimarisha chama huko vijijini.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom