Chikawe alia na utapeli wa vigogo katika kujaza fomu za mali......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chikawe alia na utapeli wa vigogo katika kujaza fomu za mali.........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 4, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,981
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Vigogo waongo, Waziri aagiza wabanwe
  Imeandikwa na Namsembaeli Mduma; Tarehe: 4th December 2010

  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe ameishukia Sekretarieti ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, akidai imeshindwa kutumia mamlaka iliyonayo kuwabana vigogo wa serikali wanaojihusisha na rushwa, ufisadi na wanaodanganya juu ya mali walizonazo.

  Chikawe alitoa madai hayo mazito alipozungumza na wafanyakazi wa sekretarieti hiyo, Dar es Salaam jana, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kuifanya katika taasisi zilizo chini ya ofisi yake hiyo inayoshughulikia utawala bora.

  Waziri Chikawe alisema, viongozi wengi wanaojaza fomu za maadili ya viongozi wa umma wanadanganya kuhusu mali zao kwa lengo la kuficha ukweli kitendo alichosema kinapaswa kuchukulia hatua za kisheria mara moja.

  Alisema pamoja na kudanganya, lakini pia wapo viongozi wa umma wanajihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi, lakini hakuna hatua zozote wanazochukuliwa, hatua inayopotosha dhana nzima ya utawala bora.

  Aliitaka sekretarieti hiyo kubadilika mara moja kiutendaji na kufanya uchunguzi wa kina juu ya maadili ya viongozi hao ili kuwafichua na kuwachukulia hatua za kisheria wale watakaobainika kudanganya juu ya mali walizonazo, kuhusika na rushwa au ufisadi.

  Chikawe alisema uwezo wa kiutendaji iliyoonesha sekretarieti hiyo ni sawa na asilimia nne ya kazi nzima wanayotakiwa kuifanya, hatua ambayo haikidhi kuudhihirishia umma kwamba ipo makini katika kusimamia maadili ya viongozi.

  Kwa mujibu wa Chikawe, umefika wakati kwa sekretarieti hiyo kutambua umuhimu wake kwa umma, na hivyo kuwajibika kwa kuzingatia malengo yaliyosababisha kuwepo kwake.

  Alisema, sekretarieti hiyo inawajibika pia kuzifundisha, kuzielekeza na kuziagiza taasisi nyingine, kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kushughulikia masuala yanayohusu rushwa na ufisadi badala ya kuziacha taasisi hizo kufanya kazi zipendavyo.

  Alisema ingawa sheria iliyoanzisha sekretarieti hiyo haina meno ya kutosha katika kuwaadhibu viongozi wanaokiuka maadili ya umma, lakini hiyo haiwezi kuchukuliwa kama sababu ya kuwaacha kuendelea kukiuka maadili ya umma bila kuchukuliwa hatua kwani sekretarieti hiyo inaweza kuziagiza taasisi zake ikiwemo Takukuru kuwafikisha viongozi hao mahakamani kwa kutumia sheria zao.

  “Natambua umuhimu wa sekretarieti hii na jambo hili nitalipa umuhimu mkubwa ili kuhakikisha tunaandaa utaratibu wa kuifikisha sheria hii bungeni kwa ajili ya kuongezwa makali ili itoe mamlaka ya kuwawajibisha viongozi wasio waadilifu kwa lengo la kukuza na kulinda utawala bora nchini.

  “Ifikie mahali muiite Takukuru na kuiagiza ichunguze viongozi fulani mtakaokuwa na mashaka na maelezo yao wanayoyatoa katika fomu za maadili ya viongozi, taasisi hiyo itazifanyia kazi zaidi na kuwafikisha mahakamani watakaobainika kusema uongo pale inapobidi, vinginevyo, ufisadi na rushwa havitakoma,” alisema.

  Alisema, wapo viongozi wanaodanganya wakati wana chembechembe za wazi za rushwa na ufisadi, na kwamba ndio maana asilimia moja ya tatu ya bajeti za serikali za kila mwaka zinaishia kwenye rushwa na ufisadi wa viongozi wa umma.

  “Hili ni tatizo na kikwazo kwa utawala bora, nitatoa ushirikiano wa kutosha ili tulikomeshe, nipeni na mimi ushirikiano tulifanikishe kulimaliza,” alisema Chikawe.

  Jumla ya viongozi wa umma wanaojaza fomu hizo za maadili ya viongozi, kwa mujibu wa Waziri Chikawe ni 7,888 ambapo viongozi wa kisiasa wakiwemo mawaziri ni 4,018 na watendaji wengine wakiwemo Makatibu Wakuu ni 3,870.
   
 2. A

  August JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  yaani EL hakujaza vizuri form yake, sasa naona mpambano wa 2015 anaingia candidate mwingine, itakuwa vita ya lindi ntwara membe/chikawe vs mwandosya , elinino nk
   
 3. m

  matawi JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sawa Chikawe. Bado hatukufahamu vizuri tunasubiri kuona achievement zako maana kusema kila mtu anaweza. Katika hili tunasubiri wewe kama Waziri utatufanyia nini
   
 4. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Chini ya mfumo mbovu wa ccm I don't expect anything new! Time will tell
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,981
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Saturday December 04, 2010 Local News
  Big shots who cheat on wealth


  By DAILY NEWS Reporter, 3rd December 2010 @ 22:00, Total Comments: 0, Hits: 45

  MOST public officials cheat on declaring their assets and liabilities at Leadership Ethics Secretariat, hence defeating the whole exercise of mandating compulsory declaration of the wealth to strengthen good governance.

  The Minister of State in the President's Office (Good Governance), Mr Mathias Chikawe, warned such public officials and urged Ethics Secretariat to go an extra mile and investigate to establish if what such officials declared on their forms was actually what they were worth.

  Mr Chikawe who was appointed to the portfolio over a week ago, said it was high time cheating public officials were held accountable if the concept of good governance and rule of law was upheld.

  "You should reach a point where, if in doubt with certain public officials, you sanction Prevention and Combatting of Corruption Bureau (PCCB) to assist with investigations into their assets," Mr Chikawe told employees of the Ethics Secretariat, when formally defining the position of his ministry since taking over.

  The minister decried the Secretariat's poor performance in the past with only four per cent of cases that they questioned and conducted investigations, arguing that the public expected more from the institution that tracks public officials' conduct.

  "I know you have problems in executing your mandate, including legal shortfalls, but that should not be an excuse to perform so poorly," Chikawe pointed out.

  He pledged to champion taking a Bill to parliament seeking to give the Ethics Secretariat legal powers to investigate and prosecute public officials who are seen to be cheating, taking bribes and embezzling public funds.

  A third of the country's annual budget is lost through corruption and embezzlement and the minister warned culprits that it would no longer be business as usual because some people would be held accountable.

  "It is clear that where leadership ethics flop there is no good governance, therefore, assist us by safeguarding your working principles to meet your goals," Mr Chikawe emphasized.

  A record 7,888 public officials are required to fill property declaration forms out of which 4,018 are political leaders including ministers and 3,870 are senior government technocrats.
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wataje mpaka mapazia ya ofisi wanaodai ni yao!wezi wakubwa
   
 7. T

  Taso JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  huyu si alikuwa waziri wa sheria, kwa nini hakuwasukuma wanasheria wa serikali washitaki wakubwa kama yeye anavyodai Tume ya Maadili iwashinikize TAKUKURU?

  anaonyesha ana uelewa mdogo sana wa mambo ya rushwa anaposema apewe ushirikiano "tulimalize" swala hili, amalize rushwa? inakuonyesha kwamba picha aliyonayo ni ya tatizo dogo tu linaloweza kumalizwa kirahisi rahisi kwa kupeleka muswada bungeni tu
   
Loading...