Chifu Wanzagi: Viongozi wamemsaliti Nyerere

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
MSEMAJI wa familia ya Nyerere, Chifu Japhet Wanzagi amesema wanasikitishwa kuona viongozi wengi wa serikali wameacha mstari wa uadilifu aliochora hayati Mwalimu Julius Nyerere na badala yake kunyakua rasilimali za nchi kwa maslahi yao binafsi.

Chifu Wanzagi, ambaye pia ni askofu wa Kanisa la Last Church of God, alisema kutokana na mabadiliko hayo, viongozi wa nchi wanaendesha nchi ndivyo isivyo.

Kutokana na hali hiyo, amewashauri viongozi wa nchi kutumia kipindi hiki cha kuelekea katika kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Baba wa Taifa, kutafakari ni jambo lipi wanaweza kujisifu kwamba wamefanya kumuenzi mwasisi huyo.

"Ukiangalia hali ilivyo sasa pengo la Baba wa Taifa lipo, hayupo mtu wa kukemea maovu yanayofanywa na viongozi hawa. Wapo baadhi wanaweza kusema wanajaribu, lakini walio wengi hawaangalii wana wajibu gani kwa wananchi.

"Kibaya zaidi ni kulindana, watu wanafanya makosa, wana tuhuma nyingi, lakini bado wako ofisini. Enzi za Mwalimu Nyerere wasingevumiliwa, angewatoa. Hakuwa anamwacha mtu anayetuhumiwa kuendelea kukalia ofisi wakati anachunguzwa. Hali ya sasa inasikitisha sana," alisema Chifu Wanzagi katika mahojiano yaliyofanyika hivi karibuni nyumbani kwake Butiama, Musoma Vijijini.

Chifu Wanzagi aliwashauri viongozi wa nchi kufuata nyao za Mwalimu Nyerere kwani wanaposikiliza hotuba zake ambazo alikuwa akizitoa wakati nchi inapata uhuru, hazijachuja na kwamba viongozi wajaribu kufuata nyao hizo.

Badala ya kufuata nyayo na mstari wa uadilifu, viongozi wa sasa wanashindana kunyakua rasilimali zilizotunzwa na Mwalimu kwa miaka mingi bila kujali. "Huku ndiko kumuenzi kweli Baba wa Taifa? alihoji, Chifu Wazangi.

Alisema kutoka na hali hiyo, wakati wa kuelekea katika kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, viongozi wakae chini na kutafakari kauli zao na jambo gani zuri la kujisifu walilolifanya katika kumuenzi Baba wa Taifa.

Naye Joseph Muhunda Nyerere, ambaye ni mdogo wa Mwalimu Nyerere, alisema wanashukuru kupata wageni watakaokwenda Butiama kwa ajili ya kumbukumbu hiyo, na kwamba watawapokea kwa ukarimu, lakini amewataka wapime wanafuata vipi misingi aliyoacha Mwalimu Nyerere.

"Mwalimu alikuwa hapendi kujipendelea, kujikweza wala kujilimbikizia mali, aliwajali watu wote,"alisema. Alisema anapoangalia sasa miaka 10 tangu mwasisi huyo wa taifa afariki dunia, pengo lipo katika familia na katika nchi. "Sauti yake inaporudiwa kila siku inatusababishia majonzi, unaona kabisa kwamba pengo lipo,"alisema Nyerere.

 
Chifu wanzagi naona umepitwa na wakati. hakika duniya kila siku inabadilika na hata JKN alilifahamu hilo na ndio miongoni mwa vyama vingi vya siasa.

Lazima Chief Wanzagi sasa utafute umaarufu binafsi na sio wa wenzako.Unganisha nguvu zako na ukemee na sio kutumia ujiko kwa wengine.
 
Chief alimegewa sehemu kwa niaba ya ukoo wa mwl huko mbugani naye akaiuza na kuwazika pesa wanaukoo wengine. Naye ni mmoja kati ya waliomsaliti Nyerere!
 
Lakini amesema ukweli hapa na ndio maana leo kuna Vacuum ya uongozi ya Tanzania
 
Back
Top Bottom