Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,196
- 113,480
Uchaguzi ukiisha nitabadili jina na kujiita Chifu Ngabu.....kama nikivunja katiba msinishitaki....
wajameni hivi hawa watu wa kyela wamerogwa? haono kwamba ni fedheha na aibu kwa kabila zima la wanyakyusa kumtunukua kiwete heshima hii? kwa lipi jema aliloifanyia tanzania? kuwalinda mafisadi?
uchifu hata kama ni symbolic siyo peremende! wanyakyusa na viongozi wenu msitutie aibu. hili ni doa kubwa. sasa inabidi mkae, mkishamaliza kunyoosheana vidole, muweke criteria na sifa ambazo mtu anatakiwa awenazo ili mumtunuku huo uchifu. la sivyo mtaishi kuwatunuku wasanii!!
Kwa hiyo Wanyakyusa (akina Mtanzania) wamekubali Mwangupuli (Kikwete) kuwa Chifu wao!!!!............my God!........i don't want to believe this......kwi kwi kwi kwi kwi
Original story ndiyo hiyo uliyoiweka wewe au? Maana nimerudia tena kusoma na hakuna sehemu inayoonyesha huyo anayemvika magwanda Kikwete kuwa ni chifu of sort unless umefikia hiyo conclusion kwa sababu na yeye kavaa hiyo migwanda.... Sana sana kilichosemwa ni kwamba Chifu Mwangupili (Kikwete) alikuwa ni babu wa Chifu Magombe Mwakusya ambaye "alikuwa" chifu wa eneo la Kyela......
nyerere alifuta uchifu upande mmoja lakini upande wa pili yeye aliendelea kumtii na kumtambua chifu wa kabila lake..chifu wanzagi....,hata chifu wanzagi alipokufa ni yeye aliyeongoza kumsimika chifu wa sasa wa wazanaki chifu japhet wanzagi.....anayesimamia mila na tambiko za wazanaki...
uamuzi wa kufuta uchifu ulikuwa wa kisiasa ...lakini umuhimu wa machifu upoo...wangeweza kuwaondolea tu authorative powers na wakawaacha na title na jukumu la kusimamia mila na tamaduni za kabila husika.....kwa namna moja ingesaidia kusimamia maadili ya taifa iwapo machifu wangetumika vema.....
hivi kuna chifu mmoja alikuwa anaitwa MWAMI THERESA wa kigoma .....mbona hatusikii hata traces zake????..nasikia she was very powerful!!
wajameni hivi hawa watu wa kyela wamerogwa? haono kwamba ni fedheha na aibu kwa kabila zima la wanyakyusa kumtunukua kiwete heshima hii? kwa lipi jema aliloifanyia tanzania? kuwalinda mafisadi?
uchifu hata kama ni symbolic siyo peremende! wanyakyusa na viongozi wenu msitutie aibu. hili ni doa kubwa. sasa inabidi mkae, mkishamaliza kunyoosheana vidole, muweke criteria na sifa ambazo mtu anatakiwa awenazo ili mumtunuku huo uchifu. la sivyo mtaishi kuwatunuku wasanii!!
Hawa wazee wanajikomba kwa rais angalau awape hata ujumbe wa nyumba kumi kumi...
kwi !kwi !kwi !kwi !kwi!
Mwanakijiji,
kwanza hilo jina, spelling zake ni MWANKUPILI, ile baada ya 'n' ni 'k' sio 'g', ndivyo linavyoandikwa kule Kyela.
Pili, nadhani haina shida yoyote hicho cheo, ni masifa tu ambayo kimsingi ni 'unafiki' tu, nina uhakika hao wanyakyusa hawamaanishi wanachosema kwa kumpa JK uchifu huo. Tena hatokani na nasaba ya chifu Mwankupili, kwa ujumla hakuna alichopewa.
Tatu, msishangae sasa hivi kwani bado hajapewa 'vyeo' vyote ambavyo 'lobbyists' huwapa watawala. Bado hajapewa degree za heshima, ukaazi wa heshima, kuwa 'mwanaukoo' (ati hata Mkapa ni 'mwanaukoo' wa Nyerere, na kwenye urithi alipewa ng'ombe!), na mengine mengi!
Mwacheni Chifu Mwankupili II afurahie 'title' yake mpya, bado nyingine zinakuja!
Mzee Mwanakijiji,
Hii hoja ya Uchifu na Katiba naona uiache pembeni maana hata ukichaaambua namna gani na kuwa kuna udhaifu, bado Mwankupuli II ataendelea kuwa Chifu wa kusadikika kule Kyela.
Ni sawa na yule Mgombea wa Urais wa chama cha Republican Yohana Makene anavyokosa hoja kumbomoa Obama.
Lets be like Obama, tuonyeshe udhaifu wa Kikwete na labda cha umuhimu kuwa siku alipobatizwa kuwa Mwankupuli, alitoa kebehi, dharau na kuudanganya umma. Tukimpiga nyundo kwa hilo, basi kama Yohana Makene anavyochechemea kwenye mchakato wa Uchaguzi, ndivyo Mwankupuli atakavyo dorora!
Kwa Mtanzania na Ogah, add Kithuku,
Je Kyela ndio makao makuu ya Mwankupuli wa kwanza? ina maana Rungwe, Mbeya mjini, Mbeya vijijini na wilaya nyingine na WanyaChusa wake walikuwa chini ya Kyela?
KUna mtu kauliza, je Mwakipesile ndio kawatia dole kwatika jicho Mwandosya na Mwakyembe? Je Kasyupa wa Kyela alitumika vipi hapa kutoa hii nishani ya juu ya WanyaChusa?
Ni sawa na yule Mgombea wa Urais wa chama cha Republican Yohana Makene anavyokosa hoja kumbomoa Obama.
Lets be like Obama ...Tukimpiga nyundo kwa hilo, basi kama Yohana Makene anavyochechemea kwenye mchakato wa Uchaguzi, ndivyo Mwankupuli atakavyo dorora!
Una assume kwamba kila mtu hapa anamwelekeo kama wako katika upande uliouchagua wewe katika uchaguzi huo. Unapotuma madongo au utani wa kumchamba mgombea fulani hakikisha wote unaoongea nao ni kondoo wa kundi hilo hilo moja na wewe. Unless kama unampigia kampeni mtu wako. Na hata hapo pia, ukijichanganya sehemu sehemu na siasa zisizotakiwa unaweza ukasubiriwa na walevi kichakani na mawe!