Chifu Mwangupili wa Unyakyusa na Ibara 29:3,4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chifu Mwangupili wa Unyakyusa na Ibara 29:3,4

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 14, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na Mwandishi Maalum, (Habari Leo)
  Kyela, Mbeya

  [​IMG]

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi Oktoba 11, 2008) ametawazwa kuwa chifu wa Kabila la Wanyakyusa na amepewa jina rasmi la Chifu Mwangupili.
  Rais amepewa heshima hiyo na wazee wa Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya, kwenye Uwanja wa Michezo wa mji wa Kyela wakati alipotembelea wilaya hiyo akiwa katika siku ya tatu ya ziara ya Mkoa huo.

  Tangazo la Rais Kikwete kuwa Chifu Mwangupili limetolewa kwenye Uwanja wa Michezo wa Kyela mbele ya maelfu ya wananchi ambako pia alivalishwa wazi rasmi la kichifu na kupewa zana nyingine kukamilisha heshima hiyo.

  Wazee wa Wilaya hiyo wamesema kuwa wameamua kumpa heshima hiyo Rais Kikwete kwa sababu ya uhodari wa utawala wake na kwamba Chifu Mwangupili alikuwa babu wa Chifu Magombe Mwakyusa ambaye alikuwa chifu wa eneo la Kyela.

  Akizungumza mara baada ya kuwa ametawazwa kuwa chifu wa kabila hilo, Rais Kikwete amewashukuru wazee na wakazi wote wa wilaya hiyo kwa uamuzi wake wa kumtunukia heshima ya kuitwa Chifu Mwangupili.

  Baada ya hapo, ametumia muda wa kutosha kuelezea utekelezaji wa ahadi za Serikali zake kitaifa na katika wilaya ya Kenya katika maeneo ya elimu, afya, miundombinu na hasa ujenzi wa barabara, uwezeshaji wa wananchi.

  Kwa mara nyingine amesisitiza kuwa Serikali Kuu imekuwa inatoa fedha nyingine kwa serikali za mitaa kwa ajili ya maendeleo, lakini mara nyingine fedha hizo zimekuwa hazisimamiwi vizuri na madiwani.

  Amesisitiza kuwa ni wajibu wa madiwani kusimamia vizuri fedha hizo ili matunda ya fedha hizo yaonekane katika mabadiliko ya maisha ya wananchi iwe kwa njia ya elimu, afya ama hata miundombinu.

  Wilaya ya Kyela imepewa sh bilioni 12 kwa ajili ya kuendeleza miradi mbali mbali wilayani humo kwa mwaka huu.

  "Kama ninavyosema kila mara, tunatoa fedha nyingi mno kuliko wakati mwingine wowote tokea tupate uhuru, lakini lazima matumizi ya fedha hizi yasimamiwe na madiwani ambao ndiyo wabunge wetu kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa."

  Mapema akipokea taarifa ya wilaya hiyo ya Kyela, Rais Kikwete amewaonya wakazi wa wilaya hiyo kuvusha dawa kutoka Tanzania na kuzipeleka kwa jamaa zao katika nchi jirani ya Malawi.

  Kwenye taarifa hiyo iliyotolewa katika eneo la mpakani kabisa mwa Tanzania na Malawi la Kasumulu, ilielezwa kuwa hospitali za wilaya hiyo zimekuwa zinakabiliwa na matatizo makubwa ya sekya ya afya ikiwa ni pamoja na ukosefu wa dawa za kutosha kiasi cha kwamba baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo wamekuwa wakitafuta huduma za afya katika wilaya jirani ya Rungwe.
  "Naambiwa sasa tatizo limepatiwa ufumbuzi, lakini pia naambiwa kuwa mmekuwa mnachukua dawa katika hospitali zetu na kuzipeleka kwa jamaa zenu Malawi.

  "Hapa tunayo matatizo makubwa ya afya. Tunalo tatizo kubwa la malaria. Msipeleke dawa hizo kule nchi jirani ya Malawi. Hawa wajomba wenu kama wanataka kutibiwa wavusheni mpaka na kuwaleta huku," amesema na kuongeza:
  "Watu wa ajabu nyie. Dawa mnapeleka Malawi, halafu nyie mnakwenda Rungwe kutibiwa. Kweli ujanja mwingi huondoa maarufu."

  My Take:
  Ibara ya 29:3,4 ya Katiba yetu inasema hivi:
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Oct 14, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Lakini hii si ni symbolic tu....Kwani atakuwa mtawala halali atakayetumia uchifu wake huo aliopewa kutawala? Ataondoka hapo na kurudi Ikulu na kuvua hiyo mitambara aliyovaa kichwani, hilo limkuki litawekwa stoo, atavaa suti yake ya Brooks Brothers halafu huyo atapanda G5 yake kwenda kiwanja....
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Nafahamu wanachoashiria lakini sicho wanachosema; Katiba haina utata, soma hicho kipengele cha pili. Najaribu kukumbuka mahali ambapo Nyerere alikuwa anakubali kuvikwa mavazi haya ya uchifu, inawezekana ilikuwepo lakini nimetafuta sana picha sijaziona.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Oct 14, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani wanachosema ni uchifu utakaokuwa na authoritative powers na sio huu wa kuvikwa migwanda kwenye sherehe halafu mkimaliza hakuna atakayekumbuka tena kuwa wewe ni chifu wa sehemu fulani. Mbona Fundikira aliendelea kuwa na hiyo title ya uchifu hata wakati wa Nyerere. Labda basi wangeweka wazi kwenye katiba kuwa hata uchifu wa ishara ni marufuku.
   
 5. M

  Mchelea Mwana Member

  #5
  Oct 14, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Katiba imeweka wazi kabisa kuwa:

  (3) Raia yoyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki,
  hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi
  wake.
  (4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo
  maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi
  ya nasaba, jadi au urithi.

  Kimsingi kwangu siyo huo uchifu wa ishara wa mtu asiye na nasaba au urithi wa uchifu; kwangu ni hilo la watu ambao wanatambulishwa katika jamii kuwa ni machifu kutokana na nasaba zao au urithi wao. Kikatiba watu hao hawapo na ni makosa kwa kiongozi wa serikali kuwatambua hivyo au kuwatambulisha hivyo.

  Lakini Katiba katika hilo halina utata kuwa inasema "hakutakuwa"... sasa mbona wapo?
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mzee Mwanakijiji,

  Mbona Nyerere alishavaa sana hayo manguo ya jadi? Binafsi nilishaona picha za Nyerere mara nyingi tu akivishwa hayo manguo.

  Kitu ambacho sikumbuki ni kama yalikuwa ya kijadi au kichifu.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Oct 14, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mimi nikianza kujiita Chifu Nyani na baadhi ya watu wakaanza kuniita hivyo na nika design vazi langu mwenyewe na kila sehemu nitakayoenda watu watakuwa wakiniita Chifu Nyani McCain nitakuwa nimevunja katiba?

  Halafu kwenye hiyo habari sijaona chifu yeyote yule. Wamesema ni wazee ndio waliompa hicho cheo.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Oct 14, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Who cares anyway? Watu wanataka na kujali maisha bora na sio ku-mind migwanda na mitambara anayovaa au kuvalishwa kiongozi fulani kwenye hafla ambaye baada ya hafla atarudi nyumbani na kumpa hiyo kitambara housebirl au houseboy kupigia deki. Come on people......
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Oct 14, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,018
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,

  ..kwa kweli hapa tulipofika Kikwete inabidi abadili jina sasa.

  ..tena nadhani jina Mwangupili linamfaa.

  ..Raisi ameharibu kwelikweli. inabidi aanze upya.

  ..kutuhakikishia kwamba ameachana uzembe na tarbia zake za zamani, na pia kutupa imani mpya, inabidi abadili jina.

  NB:
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwenye origina story huyo anayemvika hayo magwanda ni Chifu of sort..
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nyani, it matters a lot.

  Unajua kwanini wamarekani walikataa George Washington asiwe mfalme wa aina fulani na Katiba yao (kama ya kwetu) inamkataza Mmarekani yeyote yule kupokea cheo chochote kinachotolewa kwa kurithishana.
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Oct 14, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Original story ndiyo hiyo uliyoiweka wewe au? Maana nimerudia tena kusoma na hakuna sehemu inayoonyesha huyo anayemvika magwanda Kikwete kuwa ni chifu of sort unless umefikia hiyo conclusion kwa sababu na yeye kavaa hiyo migwanda.... Sana sana kilichosemwa ni kwamba Chifu Mwangupili (Kikwete) alikuwa ni babu wa Chifu Magombe Mwakusya ambaye "alikuwa" chifu wa eneo la Kyela......
   
 15. Companero

  Companero Platinum Member

  #15
  Oct 14, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu hii ukiipeleka mahakamani utashindwa kesi kufuatana na misingi ya tafsiri ya sheria katika korti. Ibara ya 29(4) inasema "ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo...". Hakuna sheria hapo iliyotoa haki, hadhi au cheo maalum kwa Mwangulupi. Pia Ibara ya 29(3) inasema "...kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi wake". Hapo Mwangulupi hakupewa uchifu kwa misingi ya nasaba yake ya Uafrika, jadi yake ya Kikwere au urithi wake wa Kichifu. Kesi imefungwa.
   
 16. O

  Ogah JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo Wanyakyusa (akina Mtanzania) wamekubali Mwangupuli (Kikwete) kuwa Chifu wao!!!!............my God!........i don't want to believe this......kwi kwi kwi kwi kwi
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ......and this is very interesting.........

  eeeeehhhhh!!!......kwi kwi kwi kwi kwi
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Oct 14, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  So it matters because the Americans didn't want to?

  My point is this: kisheria machifu hawatambuliwi na hawana mamlaka yoyote yale. Lakini kama watu wa sehemu fulani wakiamua kukuita wewe Mwanakijiji Chifu Mwanakijiji kuna ubaya gani? Haina maana utakuwa unatawala watu na haina maana watoto wako watarithi hicho cheo na hata na wao wakiamua kujiita Chifu Mwanakijiji Jr.....hey what's wrong with that?
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Oct 14, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  We utamuweza Mwanakijiji.....
  Yaani hata hii anataka kuishikia bango....naona kaboreka leo...
   
 20. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwi kwi kwi!!!!!
   
Loading...