Chifu Butale: Chifu ni Sauti ya Mungu, Uchifu siyo Ushirikina au Uchawi bali ni Ukuhani na Utume

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,571
Mwenyekiti wa machifu wa Wasukuma Chifu Butale yuko mubashara Star tv akitolea ufafanuzi mjadala uliopamba moto nchini wa nafasi ya chifu katika taifa.

Chifu Butale anasema uchifu siyo ushirikina au uchawi bali uchifu ni uwakilishi wa mungu yaani ni utume na ukuhani.

Chifu Butale anasema yeye mwenyewe ni mkristo wa katoliki.

Updates;

Chifu Butale anasema kwa sasa kuna machifu 92 nchi nzima lakini idadi hiyo itaongezeka sana.

Chifu Butale anaiomba serikali iwe inawapa msaada pale wanapokuwa na uhitaji.

Chifu Butale ametabiri mtangazaji Benard James wa Star tv atateuliwa kuwa Mkuu wa mkoa.
 
Mwenyekiti wa machifu wa Wasukuma Chifu Butale yuko mubashara Star tv akitolea ufafanuzi mjadala uliopamba moto nchini wa nafasi ya chifu katika taifa...
Bwana Yesu alisema 'siku zinazokaribia mwisho kutaibuka watu wa aina aina na wengine watatumia jina langu nao watawapotosha watu wengi hata walio wema'. Take care!

Mtu hawi mtu wa Mungu kwa kudai ni Mkiristo au Mkatoliki au Muislamu. Kuna watu wengi wanaotaja jina la Mwenyezi Mungu na wanalitumia vibaya kwa kufanya uhalifu.

Kuna baadhi ya watu kabla ya kufanya uhalifu wanaomba na wakifanikiwa wanadai 'Mungu ndiye aliyewapa hayo mafanikio ya uovu'. Sisemi huyo chifu ni mwovu, ila ninachosema kuna watu wanaojificha kwenye kauli kama hizo kuwadanganya wanaoweza kudanganyika.
 
Maza anataka kutuletea hili balaa la Machief. Tusiwakubali. Waendelee vilevile kama zamani wakijijua wao na familia zao kuwa ni machifu.
 
Dini ni kichaka. Huwezi kupewa uchief kama wewe sio gwiji kwenye mambo ya giza. Chief ni mkuu anaetawala eneo husika katika ulimwengu wa giza, wachawi wanamipaka yao na tawala zao awaingiliani bila ruhusa yao ukitaka kupita kwenye anga yao ni lazima uwaombe ruhusa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom