Chichijima Incident: Rais wa 41 wa Marekani, George Bush alivyonusurika kuliwa na wanajeshi wa Ki-Japan

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,878
1,849
Dunia ina mambo siyo kidogo. Wakati ambao unahisi upo kwenye nyakati ngumu kuna wenzako mikiki wanayopitia ni mara mia ya hiyo ya kwako!!

Kwanza siku hizi, kizazi cha millenials, tuna raha. Vita vita tunazisikia na kuzisoma kwenye vitabu tu na bado inaogopesha!! Embu waza kash kash za zamani - kuanzia adhabu na maisha kwa ujumla ya enzi hizo. Kama kuna watu wanatakiwa kulaumu na kulia lia "maisha ni magumu" basi ni watu wa miaka hio.

Miaka ambayo dunia ilikua na viumbe primitive. Civilization haikuwepo hata... Ubabe ndio ulitawala. Afadhali siku hizi tunalindwa na visheria na elimu ya hapa na pale... La sivyo mambo yangekuwa si mambo!!

Naam!

Miaka ya 1940's ndiyo vita ya pili ya dunia ilianza na kuisha. Hakukuwa na mshindi ila kulikuwa na waliokuwa na hasara chache/nyingi baada ya vita hii kufika tamati.

Baada ya vita hii kuisha, Japan ni moja kati ya nchi ambayo iliongoza kwa kuvunja sheria za vita kutokana na vitendo vyake vya zaidi ya unyama dhidi ya maadui zake.

Ndio, sheria za makosa ya vita. Sio wewe tu, hata mimi nilishangaa kusikia kuna sheria ya makosa ya vita. Yaani vita ina sheria zake pia, inafurahisha sana hii. Nyie mnapigana ndio lakini kuna sheria zinazolinda vita yenu hio. Na kwa atakaekiuka adhabu yake mara nyingi huwa ni kifo (death) au kifungo cha muda mrefu (long term confinement) kutoka mzima hapa ni nadra sana.

Basi Japan ilikuwa kati ya nchi kinara kwa kuvunja sheria hizo za vita. Askari wa kijapani walikuwa hawana huruma.

Baadhi ya mambo waliyofanya ni ubakaji na uuaji wa kikatili. Kula nyama za binadamu wenzao (cannibalism) hasa wafungwa na mateka kwao ilikua jambo la kawaida. Waliamini kufanya hivyo ni jambo zuri kwa Mungu na linawaongezea nguvu na inaweza kuwa kama dawa ya tumbo pia.

Kama unafikiri walikuwa wanakula nyama ya watu waliokufa umekosea. Ilikua ni nyama freshi - Mtu aliye hai alikuwa anakatwa kipande kimoja baada ya kingine (amputation.) Kwa mfano leo wangekata paja tu, kesho mkono hivo hivo mpaka victim afariki. Unaweza kuona ni mateso kiasi gani, hawa mateka/wafungwa, walikuwa wanakutana nayo...

Baadhi ya Askari wa kijapani wamewahi kukiri kuwa serikali ya Japan(kwa kipindi hicho) ilikuwa na mkono wake kwenye matukio hayo, kwa faida za watu binafsi na faida za nchi.

Hata hivyo, kuanzia miaka ya 1950's baadhi ya viongozi wa kiserikali wamekuwa wakiomba radhi kwa vitendo hivyo vya serikali zilizopita lakini pia wapo wengine ambao wamekuwa wakipinga vikali shutuma hizo wakidai ni UONGO. Moja ya shutuma ikiwa ni ile ya kuteka wanawake na kuwatumia kama vyombo vya starehe (sex slaves.)

Naam!.. Dunia ina mambo kweli kweli.! Hebu turudi kwenye mada yetu sasa

Mwaka 1941, Miaka miwili tangu vita vya pili vya dunia vianze tokea mwaka 1939, George H. W Bush, akiwa na miaka 18..... Japan, Kupitia jeshi lake la anga ilifanya shambulio la ghafla katika bandari ya pearl marekani. Shambulio hili lilikuwa ni kama onyo kwa marekani kuacha kuingilia maamuzi ya kijeshi yanayopangwa kusinimashariki mwa Asia.!

Kwa sababu hio, jina lake lilikua ni moja kati ya majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga na kozi ya miezi 10 ya mafunzo ya kijeshi ya jeshi la anga Marekani.

Jukumu hilo lilimulazimu kukatisha masomo yake chuoni, na kwenda kwa ajili ya kulitumikia taifa lake.

Mafunzoni alionesha umahiri na juhudi. Akawekwa kwenye mission ndogo ndogo za hapa na pale na hata alipowafurahisha wakubwa, akapewa majukumu makubwa zaidi.

Wakati huu marekani ilikwisha jiunga na vita vya pili vya dunia (WWII) na kutokana na mashambulizi ya bandari ya pearl, ilipofika mwaka 1944 mwishoni kiliundwa kikosi maalumu kitakachofanya oparesheni dhidi ya wajapani, huko visiwa vya bonin, takribani maili 700 kutokea kusini mwa Tokyo.

Kwenye kikosi cha jeshi la anga kilichokuwa na watu tisa, Bush alikuwa mmoja wao. Alikabidhiwa ndege ya kivita, yeye na wenzake.
Walipo kuwa kwenye anga ya Japan walishambuliwa ghafla na wenzake nane wakaanguka hapo. Kwa bahati nzuri ndege yake ilienda kutuwa mbali kidogo na sehemu ambayo wenzake waliangukia.

Huko alikutana wanajeshi wenzake wa kimarekani ndiyo ikawa pona pona yake...

Inasemekana baada ya wanajeshi wa anga waliokuwa na Bush kuanguka, waliwekwa chini ya jeshi la kijapani lisilokuwa na huruma. Waliteswa na kupigwa lakini kubwa zaidi ni kwamba wanne (4) kati yao walikatwa kipande kimoja kimoja na kuliwa na wengine wanne (4) kuteswa mpaka kufa...

Basi baada ya vita hii kuisha sheria za makosa ya vita zilifuata mkondo wake na mwaka 1947, kati ya wa Japan 30 waliopatwa na hatia, watano (Matoba, Tachibana, Mori, Yoshii na Teruki) walihukumiwa kunyongwa mpaka kufa.!

Kwa kuwa zamani hakukuwa na sheria iliyotambua cannibalism kama kosa, watuhumiwa hawa, walihukimiwa kwa kosa la kuua na kuinyima maiti haki ya kuzikwa kwa heshima.!

Kwa upande wa Bush, Alirudi akaendelea na masomo. Baada ya kuhitimu akaanza biashara ya mafuta iliyompa kipato kikubwa hadi kumiliki kampuni mpaka hapo baadae akaingia kwenye siasa.

Mara ya kwanza aligombea u rais wa marekani mwaka 1964 na akaburuzwa mpaka alipojaribu tena bahati yake akashinda mwaka 1989 akitoka nafasi ya makamu wa rais na kuwa rais. alikaa madarakani kuanzia 1989 hadi 1993.

Kitendo cha kupona kwenye mkasa ule wa chichijima, alipoombwa aseme chochote, alisema "Kwanini nilitengwa na wenzangu nane wale. Hakika Mungu alikuwa na mpango nami.!"

Alifariki dunia mwaka 2018, November. Huyu ni baba yake na George Walker Bush( Rais wa 43 wa Marekani)

Somo: Kila gumu unalopitia lina faraja mbele yake. As long you're alive God has plans for you!! Mipango ya Mungu inaisha siku ukifa. Kama upo hai bado muda wa kukata tamaa.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom