Chezea wazanzibar nyieeee. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chezea wazanzibar nyieeee.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bikra, Jul 16, 2012.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  SISI Wazanzibari ngoma yetu ya "KIBATI" tushaicheza toka 2010, na ndio imewafanya Watanganyika kuja na MZIMU wa katiba mpya. Mabadiliko ya 10 ya KATIBA YA ZANZIBAR yamewafanya sasa waamshe ngoma yao ya kimasai, sasa wacha tuangalie wanavyocheza huku wakikoseana mikuki...... ha ha ha ha ha.


  Kilichokuwa kikifanywa na UAMSHO, wenyewe wenye lugha wanakiita ‘Negotiating from a strong Opposition’ Mara hii lazima muone joto ya jiwe watu wa upande wa pili (Watanganyika); mambo ndio kwanza yanaanza mushaanza kupatwa na baridi. HATA BADO MWISHO MTATAFUNANA WENYEWE.


  Sisi tunawaambia….......
  ZANZIBAR KWANZA.....na Uzanzibar ndio FAGHARI YETU.


  Niliwaambia siku za nyuma humu, UAMSHO ni chombo tu cha usafirishaii na imepewa kazi ya kufunga chapter ya mwanzo ya ZANZIBAR MPYA na kufungua ya pili ya KUDAI "SOVEREIGNTY" ya ZANZIBAR kama Taifa na katika kutekeleza majukumu yake kuna STEPS za kupitia na hakuna wa kuwazuiya Zanzibar. WAZANZIBAR NI WATAALAMU WA FANI YA SIASA njooonii mjifunze nyinyi watu..


  Sasa tumewatia Tanganyika kwenywe "micrometer gauge'' TUNAWATAZAMA KWA MAKINI, tunawasaidia kutunga katiba ya tanganyika tukimaliza mtakwenda wenyewe NEW YORK kushusha lile tambara la MUUNGANO.


  CHEZEA WAZANZIBAR NYIEEEE.


  Toa maoni yako.....kwa kujenga HOJA
   
 2. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Du kumbe UROJO nao ni kilevi?
   
 3. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,186
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  KAMA MTU ALIYEROPOKA VILE. Wajipange upya maana VIONGOZI WA NCHI Wametoa ONYO kwao


  Dr-SHEIN- Muungano hautavunjika nitautetea na Wakiwaita kwenye maandamano Msiende

  SHAMSI VUAI NAHODHA- Muungano hutovunjika na ninaupenda sana
   
 4. m

  msitu wa pande Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijajua kama ni ngonjera au ni mashairi ya taarabu.hila najua tu Wazanzibari hawapatani na viroba, vinawalewesha kupitiliza!
   
 5. Isalia

  Isalia JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 950
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Wao ni kama nani people power ndio itakayo sema hata mubaraka hakupenda kuundoka madarakani misri wakati ndio unaosema leteni jeshi lote la huko tanganyika lakini ukweli utacmama. 'Z'bar kwanza'
   
 6. jobe ayoub

  jobe ayoub JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 206
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
   
 7. jobe ayoub

  jobe ayoub JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 206
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  sasa hapa utachangia nini kama si upuzi tu..
  kwa hiyo kujitenga we unaona ni dili..
  watu wanawaza vitu vya msingi,we pumba tu..

  kwanza muungano unatusaidia nini wakati mmekua kama kupe!!
  wazushi nyie,mtakula jeuri yenu na ulojo yenu
   
 8. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot]Zitto Kabwe : Muundo wa Muungano: Serikali Tatu, Moja, Mbili? Zote [/FONT]
  [FONT=&quot]Mwalimu Azaveli Lwaitama ni mwalimu na mlezi wangu nje ya darasa. Alipokuwa Katibu wa Umoja wa Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mimi nilikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Idara ya Uchumi. Nilikuwa nashinda kwenye Ofisi ya UDASA tukijadiliana kuhusu Umajumui wa Afrika (Pan-Africanism), Ujamaa na harakati za kulinda haki za watu. Ilikuwa
  ni nadra kwa mwanafunzi wa uchumi kuwa karibu na mwalimu wa lugha na mnadharia mkubwa. Wanafunzi wa uchumi tulikuwa tunajidai na kujivuna. Tulikuwa tunajiona bora sana maana darasa letu halikuwa linazidi watu 40 na kwa kweli wote hawamalizi. Darasa langu tulimaliza wanafunzi 25 tu kati ya 40 tulioanza. Mwalimu Lwaitama ni mpenzi mkubwa wa Muungano
  kama nilivyo mimi. Tumeapa kuulinda kwa namna yeyote ile. Yeye alikuwa mhafidhina (conservative) sana akitaka Muungano wa muundo huu aliouacha Mwalimu Nyerere. Mimi nataka kuulinda kwa kuufanyia marekebisho makubwa sana ya kimuundo. Hatukuwa tunakubaliana.

  Wiki iliyopita Mwalimu Lwaitama kaandika kuhusu muundo wa Muungano katika makala zake za kila wiki katika gazeti la kimombo la The Citizen. Amebadili msimamo. Ameona sasa muundo wa Muungano ulivyo sio endelevu. Ametoa mapendekezo niliyoyatoa siku za nyuma katika mazungumzo yetu ingawa yeye bado anayasema kwa shingo upande. Lwaitama
  sasa anataka Serikali mbili zilizonyumbuliwa. Anapendekeza Waziri Mkuu wa Muungano mwenye nguvu za za kitendaji. Nampongeza kwa kuboresha mawazo yake.

  Hata hivyo bado Mwalimu wangu na Watanzania wengi wamejikita katika mjadala wa Serikali ngapi. Idadi ya Serikali inaonekana kama ndio dawa ya kero za Muungano. Ni kweli Wazanzibari wanataka uhuru zaidi na wengine hawataki kabisa Muungano. Unawalalia. Unawanyima uhuru wa kuamua baadhi ya mambo yao na japo halisemwi unawanyima wanasiasa wa Zanzibar mamlaka ya masuala mengine ambayo yangewafanya wajilimbikizie
  madaraka.

  Huku bara napo kuna watu, tena wanaongezeka kwa kasi kweli kweli, wakitaka Tanganyika yao. Tena wengi vijana. Demografia zetu zinaonyesha kwamba Watanganyika waliozaliwa Tanganyika ni takribani asilimia 12 tu ya Watanzania. Asilimia 70 ya Watanzania wamezaliwa
  wakati Muungano umeshasherehekea miaka 15 ya kuzaliwa kwake. Lakini wanataka Tanganyika yao. Wamechoshwa na kelele za Wazanzibari. Hawawataki Wazanzibari kujaa kwenye Bunge la Muungano wakati wapo kiduchu sana. Wanasiasa nao, japo hawasemi waziwazi wanataka wawe na mamlaka zaidi bila kulazimika kushauriana na wanasiasa wa Zanzibar. Linapokuja suala la wagombea Urais ndio kabisa wanakereka kutafuta mgombea mwenza kutoka Zanzibar. Wachambuzi wa historia za kisiasa siku wakiamua kufanya tafiti watachoka na roho zao watakapoona aina za wagombea wenza ambao wagombea Urais huteua, hasa kutoka sisi vyama vya upinzani.

  Kimsingi idadi ya wapinga Muungano inazidi kuongezeka siku hata siku. Ukiwauliza kwa nini hawataki Muungano wanasema aah, basi tu. Kama ni Mzanzibari atasema Tanganyika wanatutawala. Kama ni Mtanganyika
  atasema Wazanzibari wamezidi kelele, tunataka Tanganyika yetu. Sisi ‘Unionists’ (Wanamuungano) nao hatuna majibu ya kuridhisha sana na ya kukonga nyoyo. Isipokuwa tu, Muungano huu ni wa aina yake Afrika na Duniani. Ni alama pekee ya kuonyesha Mwafrika kupinga mipaka ya kikoloni. Sasa hili haliwaingii kichwani ‘secessionists’ (Wanautengano) na hatuna la kuwasaidia. Lakini ni lazima tuurekebishe Muungano huu. Ulivyo sasa utavunjika tu. Kuulinda Muungano ni kuufanyia marekebisho makubwa. Mwalimu Lwaitama kaliona
  hilo. Pendekezo lake liboreshwe sasa. Sio rahisi sana.

  Sasa tufanyeje? Serikali moja itaimeza Zanzibar. Serikali Tatu ni gharama kuendesha na Serikali mbili zimeimeza Tanganyika na watu wanataka Tanganyika yao na zinainyima uhuru Zanzibar na watu wanataka wawe huru zaidi. Mfumo wa Serikali ngapi na kadhalika ni moja ya mikakati ya wanasiasa katika kusaka vyeo. Sisemi sio halali kujadili lakini kiukweli mfumo gani wa Muungano hautaongeza fungu la dagaa kwa mwananchi wa Kagongo au sinia la ubwabwa kwa mwananchi wa Mkanyageni. Waingereza wana msemo ‘unataka kula keki yako na kubaki nayo’, basi tuwe na Serikali zote.

  Nimeanza na Mwalimu Azaveli Lwaitama. Naboresha hoja yake kwa kurudia niliyowahi kuyasema huko nyuma kuhusu muundo wa Muungano. Tuwe na Dola Moja tu. Ndio, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wala sio Shirikisho la Tanzania (kwanza litatuondoa kwenye kiti chetu kule Umoja wa Mataifa maana kwa jina letu sisi tunakaa katikati ya Uingereza na
  Marekani. Katikakati ya mabwana wakubwa, labda ndio maana wanatupa misaada sana, unajuaje?). Tuwe na Rais mmoja tu mwenye mamlaka kamili ya Asasi za Dola – Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Uhamiaji, Sera za Fedha na jukumu la jumla la kusimamia ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Achaguliwe na Watanzania wote wa pande zote mbili za
  Muungano kwa kupata zaidi ya nusu ya kura za pande zote za Muungano. Tuachane na mambo ya Mgombea Mwenza. Tumejaribu tumeona hana maana zaidi ya kutembea na mikasi tu.

  Zanzibar iwe na Waziri Mkuu Mtendaji kwa masuala yote ambayo sio ya Muungano. Tanganyika iwe na Waziri Mkuu Mtendaji kwa masuala yote ambayo sio ya Muungano. Hawa watateuliwa na Rais wa Muungano kutoka chama chenye Wawakilishi wengi katika Baraza la Wawakilishi Tanganyika na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Wote watakuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa utaratibu kwamba iwapo Rais anatoka Zanzibar,
  basi Waziri Mkuu wa Tanganyika atakuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na wa
  Zanzibar atakuwa Makamu wa Pili wa Rais. Kule kule kwenye misingi haswa ya Muungano. Hawa wataongoza Mabaraza yao ya Mawaziri na watakuwa na nguvu ya kuteua na kufukuza Mawaziri wanavyotaka. Hawatakuwa Wabunge katika Bunge la Muungano.

  Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye Wajumbe wasiozidi 101 pamoja na Rais wa Bunge la Muungano. Wabunge wa Muungano watatoka kwenye mikoa (au Majimbo kama sera ya Majimbo itakubalika). Kwa utaratibu wa sasa kila mkoa utachagua wabunge 2 mmoja mwanamke mmoja mwanaume kwenda Bunge la Muungano. Wajumbe wa Ziada watatokana na uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata kwenye kura za Rais wa Muungano. Idadi hii
  yaweza kupunguzwa na hata kuwa na Wabunge 51 tu akiwemo Rais wa Bunge la Muungano ambapo kwa mikoa ya sasa kila mkoa utachagua Mbunge 1 na wengine watokane na uwiano. Rais wa masuala ya Muungano atakuwa Mkuu wa Shughuli za Serikali katika Bunge la Muungano na Rais kwa mwaka mara moja atahutubia Baraza la Taifa (Wabunge wa Bunge la Muungano na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka kila upande wa Muungano). Wazungu wanaita hotuba hii ‘State of the Union’ (Hali ya Taifa) na wengine huita ‘Queen’s Speech’ (Hotuba ya Malkia).

  Mkuu wa nchi mmoja, Dola moja ya Jamhuri ya Muungano. Serikali mbili na kila upande una Serikali yake yenye mamlaka kamili ya maisha ya watu wao ya kila siku. Haya matatu pamoja na Serikali ndogo ya Muungano. Lakini tutakuwa tumepata kila kitu labda. Wenye kutaka Uhuru
  mpaka Zanzibar watapata. Wenye kutaka Tanganyika watapata na wenye kutaka Muungano kama Dola yenye nguvu watapata. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 9. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Viboko haramu - niliwamiss sana.....
   
 10. Dogo1

  Dogo1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,102
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Wote wanaoshabikia kuvunja muungano sio wazanzibari wala watanganyika, wanajijua wenyewe ni kina nani, wanatoka wapi na wana-ajenda zipi juu umoja na muingiliano wa watu wa visiwa vya zanzibar na tanganyika. Kuweni macho!
   
 11. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi si mzanzibari wala mtanganyika....ni mnyaturu halisi mtajijua wenyewe mlioungana, eti wazanzibari ooh watanganyika, ndo watu gani hawa. Nyerere alisema hakuna uzanzibari wala utanganyika bila yauzanzibari na utanganyika. Usipoelewa falsafa hii utapata shida sana
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Bora ngonjera inamruhusu mtu kuvuta pumzi
   
 13. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  yakhe...mwigulu anakuja huko kuzima hiyo kitu atiiii
   
 14. papason

  papason JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Na hasa ule wa mkaanga chips maarufu amijei mdebwedo!
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Karikenye

  Wewe pekee ndio umachangia vema thread hii..

  Swali PM wa zanzibar anachaguliwa na Rais wa JMT?? (aisee hiyo itakuwa shida kwa wazenj)

  Kama idea yako itakubalika inabidi "Rais wa JMT" uwe kwa mzunguko yaani every 10yrs lazima rais atoke zanzibar au Tanganyika

  Otherwise wazanzibar hawataweza kutoa rais wa JMT bila utaratibu huo; na hapa wazenj hawatakubali hujuma hizo.
   
 16. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hivi wazanzibar wanaamini wanaweza kuendesha maisha yao bila kuitegemea bara...wanajidanganya :wacko:
   
 17. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Wzzbar kizunguzungu: yule senior citizen jana kalalama kunyimwa kutibiwa india kwa fedha za tanganyika japo hajawahi kutindikiwa kitu. Huyu naye anajidai kuwa wao hodari wakati wenzie bado wapo kambi ya dadab wakidai pemba hapakaliki, huku wengine wamejichimbia Mbagala wakiapa kuto ngolewa hata kwa grader. Ama kweli zzbar ni zaidi ya wenyenayo wanavyoijua.
   
 18. G

  GWAMWAJA Member

  #18
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du sijui kama mtabaki salama! mkumbukeni mwl. jk nje ya muungano no. znz but pemba and unguja. mtakuja upya kama refuge
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Na mkate na mboga mboga...kaaazi kweli kweli. Si muuvunje muungani tujue moja.
   
 20. Imam Yussuf Shamsi

  Imam Yussuf Shamsi Member

  #20
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nchi zote zinategemeana na hasa zikiwa jirani,utegemezi wa znz kwa tanganyika mimi siuoni, maana hakuna mnachowapatia bure. Kama kuna kinachotolewa bure ni sehemu ya kujikosha tu juu ya zulma mnazowatendea.
   
Loading...