Cheti cha ndoa cha Serikali kinagharimu kiasi gani kukipata?

Umepigwa nenda karipoti TAKUKURU hao watu wa vizazi na vifo mawilayani wanakula sana rushwa
kwanza ishu sio kupewa cheti cha ndoa, ni kufungishwa ndoa ya kiserikali.

Wanaopewa Vyeti ni zile taasisi za kidini ambazo kisheria zimeruhusiwa kufungisha ndoa ( makanisa na misikiti.)
Hao ndio wanapewa vyeti kwa ajili ya kwenda kuwapatia waumini wao wanaowafungisha ndoa kwa taratibu zao, nao hadi kupewa hivyo vyeti kuna taratibu na mlolongo mrefu sana wa kusajiliwa , kujaza fomu za maombi na kulipia na wanatakiwa kuripoti rita .

Makanisani siku hizi unaweza pewa cheti cha kanisa na cha serikali,
hata misikitini wanafanya hivyo ila hawa wanakuwa wagumu sana kutumia vyeti vya serikali.(ila tambua cheti cha kiserikali ndicho kinatambulika kwenye masuala ya kazi maofisini).

Raia kama Raia kama unataka kufungishwa ndoa ya kiserikali, unatakiwa kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya unapoishi ambapo kuna ofisi ndoo ya rita (zipo kwenye kila ofisi ya mkuu wa wilaya Tz).
Unatakia uwe na mwenza wako, ambapo mtaeleza dhumuni lenu la kutaka kufungishwa ndoa ya kiserikali,
Mtajazishwa fomu na kisha mtalipishwa Tsh 20,000/= siku hiyo hiyo na mtapewa risit ya malipo ya kiserikali.

Baada ya hapo yule msajili pale wilayani ataandaa tangazo la nyie kukusudia kufunga ndoa na atalibandika ubaoni, ili kama kuna mtu anakipingamizi na nyie kufuna ndoa aripoti apo kwake ndani ya wiki 3 mara nyingi ni ubao wa hapohapo ofisi ya mkuu wa wilaya na atakwambia urudi baada ya wiki 3,
Baada ya wiki 3 mkirudi pale ofisini kwake na risiti ile ya elfu 20 mliyolipia na kama kukiwa hakuna pingamizi ndipo mtapanga siku na muda siku iwe ya kazi na muda wa kazi (ukitaka ufungishwe wikiend au mida ambayo sio ya kazi unaweza ambiwa toa hela ya usumbufu) mfungishwe ndoa.
Siku hiyo iliyopangwa utatakiwa uje na huyo mke wako na wasimamizi 2 wa mume na mwanamke mnaweza pia kusindikizwa na nduguu wengine wengi tu mnafungishwa ndoa na kukabidiwa cheti chenu na hakuna gharama nyingine zaidi ya ile 20,000 mliyotoa.
Watu wanaopigwa ni wale mtu anaona wiki tatu ni nyingi kuna watu wanakurupuka unakuta anaishi na mtu labda mfanyakazi bila nyaraka yoyote ya ndoa ghafla amepewa uhamisho ndio anakurupuka anataka kuzuia uhamisho kwa kutumia cheti cha ndoa anakurupuka ofisi ya vizazi na vifo kutaka asaidiwe cheti kwa haraka ili kuzuia uhamisho, mkuu hapo kama huna koneksheni vizuri na watu wa hapo unaweza kupiwa hata laki 2, au hata milioni.
Ukiwa na koneksheni unasaidiwa tu kishkaji watu wanabackdate tangazo ila elfu 20,000 lazima uilipie na upewe risiti ya serikali

Mwingine anataka akafungishwe ndoa ukumbini au nyumbani kwake , hapo lazima uambiwe utoe hela ya usumbufu .

Mwisho. Kufungishwa ndoa ya kiserikali gharama yake ni 20,000/= na unapewa risiti ya serikali
Suala la kusema kupewa cheti cha ndoa cha kiserikali hilo suala halipo, kinachofanyika pale ni kufungishwa ndoa ya kiserikali ambapo kuna taratibu kabisa
Mfungisha ndoa (DAS) anawakalisha anawapa councelling ya maana ya ndoa , mnakula viapo vya ndoa na mnasaini hivyo viapo, kama mnapete za ndoa mnavalishana ,picha mnaruhusiwa kupiga kama kumbukumbu,hata vigelegele na mnamatarumbeta mnaruhusiwa ila msizidishe makelele manake pale ni ofisini na kuna shughuli nyingine zinaendelea na mwisho ndio mnasainishwa vyeti vya ndoa na kisha mnakabiziwa kila mtu chake.
Sio tu kupewa cheti cha ndoa kama unakwenda dukani unawaambia naomba kupatiwa cheti cha ndoa,unalipia na kupewa kama unanunua bidhaa flani
CHAP KWA HARAKA nikaoe sasa
 
Back
Top Bottom