Cheti cha ndoa cha Serikali kinagharimu kiasi gani kukipata?

KingPower

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
1,098
1,745
Wakuu poleni na majukumu,

Hivi Cheti cha ndoa cha serikalini kina gharama ya Tsh ngapi hadi kukipata?

Hata Kwa experience ya uko ulipo

Natanguliza shukrani zenu za dhati
 
Kuna gharama za kuandikisha,alafu kuna malipo ndipo ufunge ndoa na kupata cheti malipo haya kama utafunga ndani ya siku 21 ofini kwa mkuu wa wilaya gharama ni 50,000/= na kama ni nje ya ofisi ya mkuu wa wilaya gharama zinazidi hapo kutokana ma mahitaji yako.
Kuandikisha Ni Bure, Sijaona Gharama Zozote Kwa Uzoefu Wangu
Kwani Mnatangaza Redioni Ama Kanisani, Msikitini, Kwa DC
 
Ninachojua Ambacho Kipo Bayana
Mkienda Kuandikisha Ndoa Ni Bure Ila Taratibu Zipo
Lazima Itangazwe Siku 21,Iwapo Kuna Pingamizi La Haki

Siku 21 Kama Kwa DC Utakuta Tangazo Kwenye Mbao
Kama Kanisani Kila Jumapili Itatangazwa Na Huwa Ni Bure

KWA Kanisa Siku 21 Zikiisha Inafungwa Haraka

Gharama Yaweza Kuwa Kubwa Kama Mtapeleka Matangazo Kwenye Radio, Gazeti, Television Ama Kwenye Blogs
 
Mkuu natamani hata niende wilaya nyingine

Hii wilaya ya hapa Tanga mjini
Ninachojua Ambacho Kipo Bayana
Mkienda Kuandikisha Ndoa Ni Bure Ila Taratibu Zipo
Lazima Itangazwe Siku 21,Iwapo Kuna Pingamizi La Haki

Siku 21 Kama Kwa DC Utakuta Tangazo Kwenye Mbao
Kama Kanisani Kila Jumapili Itatangazwa Na Huwa Ni Bure

KWA Kanisa Siku 21 Zikiisha Inafungwa Haraka

Gharama Yaweza Kuwa Kubwa Kama Mtapeleka Matangazo Kwenye Radio, Gazeti, Television Ama Kwenye Blogs
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom