Cheo ni dhamana - Viongozi lindeni heshima ya future yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cheo ni dhamana - Viongozi lindeni heshima ya future yenu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 28, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Cheo ni dhamani, sitakitumia cheo changu au cha mtu mwingine kwa faida ya....
  Kuwa kiongozi ni dhamani kubwa aliyopewa kiongozi toka kwa raia waliomdhamini kuwaongoza. Ni wajibu wa kiongozi kulinda heshima hiyo kwa manufaa ya waliomchagua na kulinda heshima yake na future yake.

  Hali kwa sasa nchini inatisha na kuleta wasiwasi, si kwa Tanzania tu, ila nchi nyingi barani Afrika. Tangu nchi za kiafrika zipate uhuru viongozi wake hawaendani na wakati ambapo raia wanazidi kukomaa kidemokrasia na elimu ya maisha na ya kiraia kuzidi kushika kasi. Kasi ya uelewa wa raia inawapa taabu viongozi kwa vile wangali na ndoto za mfumo wa uongozi wa miaka 50 iliyopita nchi zilipopata uhuru.

  Kizazi cha walichokulia viongozi wa leo (informal education) ni kile ambacho mtoto huwezi kumwuliza kitu au kumdadisi baba kitu vinginevyo utaonekana huna adabu na kuchapwa bakora. Kizazi cha leo kimekulia zaidi katika mfumo wa formal education, mfumo ambao ni wa utandawazi unaofanya vijana wa leo waonekane kuwa wenye fikra pevu na wazi na wa kweli, na hawataki mfumo wa kuendesha mambo kwa siri.

  Tatizo hapa ni dhana ya viongozi wetu licha ya kuona ishara za nyakati na uelewa mkubwa wa wananchi katika masuala ya haki zao na wajibu wa viongozi kwa raia bado viongozi wamekuwa wazito wa kuwa wawazi na hoja za msingi zinapoibuliwa na wananchi viongozi wanabuni mbinu ya ububu katika masuala wanayowajibika kutolea ufafanuzi au kuridhia haki za wananchi. Kwa ububu wa viongozi haishangazi kuona kauli kinzania ndani ya viongozi wenyewe kwa vile ukimya hufumba mengi ambayo angepaswa kuyatolea ufafanuzi hadharani.

  Uongozi una hatima yake, na jinsi unavyoongoza wananchi na kulinda vema jina na heshima yako kwa wananchi waliowachagueni ndivyo viongozi wanavyojenga vema future ya hatima ya maisha yao katika jamii. Adhabu ya uongozi mbaya, au ujanja ujanja wa kujitwalia haki za msingi katika demokrasi inaweza viongozi kuwageukia kitanzi chao. Tumeshashuhudia viongozi wengi waliohujumu demokrasi na hatima yao inavyokuwa. Kama si kiboko cha Mungu basi kuna mengi ambayo yatakukosesha raha.

  Sifikirii kiongozi baada ya kuwatumikia vema raia wake aishie kupata adhabu toka kwa Mungu ya kuwa kipofu. Na pengine haipendezi badala ya kufurahia raha ya kupumzika baada ya kustaafu unaishia kuwa kiwete au kiziwi, yote hayo ni adhabu zinazoanzia hapa hapa duniani kwa wanaochezea haki za wananchi. Kuna mengi lakini tukumbuke haki za raia zikipotoshwa ni kitanzi cha viongozi, na hata kutoishi kwa amani katika maisha yao baada ya kustaafu maana amani imekosekana ndani ya mioyo yao na dhamira zitawasuta daima.
   
Loading...