Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Ukweli ni kwamba cheo au madaraka humsababishia mtu mazingira ambayo ni rahisi sana kumbadilisha tabia. Kwa bahati mbaya, uwezekano wa cheo kumbadili mtu mwenye tabia nzuri kuwa mtu mbaya ni mkubwa wakati uwezekano wa kumbadili mtu mbaya kuwa mzuri ni kama haupo.
Ndio maana sisi wengine ijapokuwa hatueleweki kwa wepesi; tumekuwa tukishawishi kwamba ikiwa watanzania tunaamini juu ya Tanzania bora ya kesho, tunachotakiwa ni kushungulika zaidi na watu wa kawaida kuliko walioko madarakani. Msingi ni kwamba, ni rahisi kutengeneza watu wema wakiwa hawana cheo na siku wakipata cheo baadhi yao watabadilika kuwa watu wabaya lakini kwa kuwa tayari watakuwa ni wengi angalau kundi kubwa watabakia kuwa watu wema.
Lakini kama ukishindwa kujiadabisha au kumuaadabisha mtu akiwa hana cheo, uwezekano wa kuji/kum ‘Shape’ akiwa na cheo ni mdogo sana. Hii ni kwa sababu cheo humfanya mtu aangalie dunia na kujiangalia yeye mwenyewe kutokea kwenye ‘Angle’ ya tofauti kabisa.
Lakini pia suala la kujiuliza, kama tunafikiri sawasawa; kwa nini tusubiri kwamba eti tukishapata vyeo eti ndio tuanze kujifunza kuwa watu positive au ndio tuanze kuwafundisha waliopata kuwa watu positive?
Sasa hebu tujiulize maswali haya;
- Ni nani miongoni mwetu akipata cheo, na akawa na uhakika akitumia njia fulani atabaki na cheo chake kwa muda wote anaotaka bila yoyote kumfanya kitu, na akaacha kutumia njia hiyo eti tu kwa sababu anaamini sio ‘fair’?
- Hapo ulipo, ushawahi kufanya mambo mangapi ‘ya kiraia tu’ kusaidia wengine? Kama hujafanya au hufanyi, siku ukiwa kwenye ‘dilemma’ ya kuchagua kuwafanyia wengine wema wewe udhurike, au uwafanyie uovu upate maslahi, utachagua nini?
- Ni nani miongoni mwetu akipewa salio kidogo hawezi kukana anachoamini? Lakini kabla ya huko kote ni nani ambaye anaamini kitu fulani ambacho hakimsaidii yeye binafsi na yuko tayari kukutetea bila malipo?
- Ni nani ambaye yuko tayari kutumia akili, mwili na ikibidi mali kwa jambo lisilomnufaisha binafsi au bila malipo?
- Ni nani akipewa kazi ya kusimamia mabilioni ya pesa ambazo sio zake, na anajua hata akichukua bilioni chache hakuna wa kumfanya kitu, lakini ataacha kwa sababu tu anaamini kufanya hivyo sio ‘Fair’?
- Fikiria kama unakuta sasa hivi tu mtu hana cheo chochote ila anapenda kusikia habari za wengine kukwama au kudhalilika kuliko anavyopenda maendeleo yake mwenyewe, fikiria siku akiwa na cheo nini kitatokea?