Cheo kimoja kati ya Waziri Mkuu au Makamu wa Rais kifutwe

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Habari wandugu. Ukifuatilia nchi nyingi utaona kuwa zina mmoja, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais na si wote.

Na nchi nyingi zenye mawaziri wakuu ni zile za kifalme, wakati Jamhuri nyingi zina Makamu wa Rais. Na zingine zikiongozwa na waziri mkuu pekee, Rais akiwa ni ceremonial tu.

Na hata ukiangalia kiutendaji utaona kuwa makamu wa Rais huwa yupoyupo tu, haeleweki anafanya nini.

Ni wakati sasa tufute cheo kimoja, cha wazicha Waziri Mkuu au Makamu wa Rais.
 
Kimsingi cheo cha makamu wa rais hakina kazi yoyote zaidi ya kuwa supersub wa rais aliyepo madarakani.

Waziri Mkuu anatakiwa apewe mamlaka kamili ya kuunda na kuongoza serikali na endapo ikitokea rais akashindwa kuendelea kufanya majukumu yake spika wa bunge au jaji mkuu akaimu nafasi ya rais na kuitisha uchaguzi ndani ya miezi sita, jiwe gizani hilo.
 
Habari wandugu. Ukifuatilia nchi nyingi utaona kuwa zina mmoja, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais na si wote.

Na nchi nyingi zenye mawaziri wakuu ni zile za kifalme, wakati Jamhuri nyingi zina Makamu wa Rais. Na zingine zikiongozwa na waziri mkuu pekee, Rais akiwa ni ceremonial tu.

Na hata ukiangalia kiutendaji utaona kuwa makamu wa Rais huwa yupoyupo tu, haeleweki anafanya nini.

Ni wakati sasa tufute cheo kimoja, cha wazicha Waziri Mkuu au Makamu wa Rais.
... kwa Katiba hii vp kazi yake #1 ni kusubiri rais afe ili achukue nafasi! Hiyo ndio kazi yake ya msingi; kazi ya ajabu kabisa!
 
Ebu fikiri nnje ya boksi, laiti kama Mama Samia asingekuwa Makamu wa Raisi Hayati JPM, unadhani angekula shavu la kuwa Raisi kama hivi sasa?

Na kwanini hiyo nafasi ya umakamu ifutwe ngazi ya Uraisi tu ilihali Wakuu/Mabosi sekta zingine kwa vitengo mbali mbali zibaki kuwa na Makamu wake?
 
Makamu wa Rais ni mchezaji wa akiba kama ilivyotokea. Waziri Mkuu yeye hujibu maswali ya papo kwa papo Bungeni siku ya Alhamisi japo muda mrefu anakuwa jimboni kwake kama ilivyokuwa Geita.
 
Ebu fikiri nnje ya boksi, laiti kama Mama Samia asingekuwa Makamu wa Raisi Hayati JPM, unadhani angekula shavu la kuwa Raisi kama hivi sasa?

Na kwanini hiyo nafasi ya umakamu ifutwe ngazi ya Uraisi tu ilihali Wakuu/Mabosi sekta zingine kwa vitengo mbali mbali zibaki kuwa na Makamu wake?
Vyeo vya kufutwa nchi hii ni vingi sana.
 
Kuna haja Katiba pendekezwa,ije na pendekezo la kuunganisha au kufuata nafasi moja, ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi na hakina tija kwa taifa.
 
Habari wandugu. Ukifuatilia nchi nyingi utaona kuwa zina mmoja, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais na si wote.

Na nchi nyingi zenye mawaziri wakuu ni zile za kifalme, wakati Jamhuri nyingi zina Makamu wa Rais. Na zingine zikiongozwa na waziri mkuu pekee, Rais akiwa ni ceremonial tu.

Na hata ukiangalia kiutendaji utaona kuwa makamu wa Rais huwa yupoyupo tu, haeleweki anafanya nini.

Ni wakati sasa tufute cheo kimoja, cha wazicha Waziri Mkuu au Makamu wa Rais.
Nchi iwe moja na serikali moja kwa mchanganuo huu
1. Rais wa muungano atoke sehemu moja wapo ya Tanzania bara au Tanzania Zanzibar
2. Makamu wa rais akitokea Zanzibar awe pia rais wa Zanzibar
3.Rais wa JMT akitokea Zanzibar, cheo cha makamu wa rais kutokea Tanzania bara kifutwe na badala yake Waziri mkuu awe mtendaji wa serikali na makamu wa rais pia
4. Rais wa JMT akitokea Tanzania Zanzibar, mtendaji wa serikali ya visiwani awe Waziri kiongozi (vyeo vya makamu wa kwanza na pili vifutwe)
5. Zuwekwe sera za Taifa ambazo chama chochote kinachoshika dola zifuate na mtindo wa kujinasibu na ilani za vyama vya sisa ufutwe na kuweka mjumuisho wa mawazo yote mbadala na kukabidhiwa kwa kiongozi atakayeshinda kwenye uchaguzi
6. Baadhi ya watanzania bara wajumuishwe kwenye serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kama wanavyopewa wa kutoka Zanzibar kwa kushika nyadhifa kubwa serikalini na mashirika ya umma bila upendeleo
7. Kikwazo cha mtanzania bara kumiliki ardhi uondolewe
 
Sijui hata kwanini tulivyotoka kwenye makamu wa rais wawili (mmojawapo anakua pia waziri mkuu) enzi za kina malechela tukamtenganisha Rais wa zanzibar na kutenganisha makamu wa rais na uwaziri mkuu??

Cc Pohamba JokaKuu
 
Habari wandugu. Ukifuatilia nchi nyingi utaona kuwa zina mmoja, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais na si wote.

Na nchi nyingi zenye mawaziri wakuu ni zile za kifalme, wakati Jamhuri nyingi zina Makamu wa Rais. Na zingine zikiongozwa na waziri mkuu pekee, Rais akiwa ni ceremonial tu.

Na hata ukiangalia kiutendaji utaona kuwa makamu wa Rais huwa yupoyupo tu, haeleweki anafanya nini.

Ni wakati sasa tufute cheo kimoja, cha wazicha Waziri Mkuu au Makamu wa Rais.
Ili iwaje wakati unaona hata Kenya wanataka kukirudisha cheo cha PM.
 
Nchi iwe moja na serikali moja kwa mchanganuo huu
1. Rais wa muungano atoke sehemu moja wapo ya Tanzania bara au Tanzania Zanzibar
2. Makamu wa rais akitokea Zanzibar awe pia rais wa Zanzibar
3.Rais wa JMT akitokea Zanzibar, cheo cha makamu wa rais kutokea Tanzania bara kifutwe na badala yake Waziri mkuu awe mtendaji wa serikali na makamu wa rais pia
4. Rais wa JMT akitokea Tanzania Zanzibar, mtendaji wa serikali ya visiwani awe Waziri kiongozi (vyeo vya makamu wa kwanza na pili vifutwe)
5. Zuwekwe sera za Taifa ambazo chama chochote kinachoshika dola zifuate na mtindo wa kujinasibu na ilani za vyama vya sisa ufutwe na kuweka mjumuisho wa mawazo yote mbadala na kukabidhiwa kwa kiongozi atakayeshinda kwenye uchaguzi
6. Baadhi ya watanzania bara wajumuishwe kwenye serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kama wanavyopewa wa kutoka Zanzibar kwa kushika nyadhifa kubwa serikalini na mashirika ya umma bila upendeleo
7. Kikwazo cha mtanzania bara kumiliki ardhi uondolewe
Kwani Tume ya Warioba ilipendekeza nini?
 
CHEO cha Makamu wa Rais Kiko kulinda Zaidi Muungano...Na ile zanzibar bila kuwa nayo kuna kasheshe..Bora tukomae nao.Ila siku hizi Mpango hasiskiki kabisaaa.
 
Upo sahihi mkuu,km Leo hii tusingekuwa na cheo Cha makamu rais inamaana makamu wa Sasa angeendelea kuwa waziri wetu wa fedha kuliko huyu wa sasa
 
Back
Top Bottom