Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,984
Salam wadau,
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari kuhusu zogo la wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini mwaka huu walivyokosa mikopo kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu(HESLB).
Bodi imejitetea kwamba sababu kubwa ya wanafunzi wengi kukosa mikopo ni ufinyu wa bajeti. Kwa hiyo katika bajeti ya mwaka 2011/2012 serikali haikutenga fungu la kutosha kwa ajili ya kukopesha wanafunzi. Na baadhi ya wanafunzi waliokosa mikopo wamekuwa wanahangaika kuonana na wahusika mbalimbali ili kuona kama wanaweza kufanikiwa kupata mikopo na hatimaye waweze kutimiza ndoto zao. Nimeambiwa wamefikisha ujumbe wao kwa raisi Kikwete naye amewaahidi kwamba suala lao linashughulikiwa, ingawa kwa upande wa pili waziri Kawambwa ameanza kupiga mkwara wa kuwafukuza vyuoni na kuwanyima mikopo wanafunzi wote watakaoshiriki kwa namna yoyote kugoma ama kuandamana kwa ajili ya kudai mikopo.
Wakati tukiendelea kuumiza vichwa ni jinsi gani tutaondokana na jinamizi la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, imekuja taarifa rasmi ya serikali kupitia kwa waziri wa mambo ya nje kwamba hatimaye BAE system wamekubali kuirudishia serikali ya Tanzania chenji ya rada kiasi cha pauni 29 milioni sawa na shilingi 70 bilioni za Tanzania. Kwakuwa tuna matatizo ya fedha za kukopesha watanzania waliodahiliwa katika taasisi zetu za elimu ya juu, nikadhani mojawapo ya matumizi mazuri ya fedha hizi itakuwa ni kuzielekeza bodi ya mikopo ili wanafunzi wote wenye uhitaji waweze kukopeshwa na hivyo kubaki na kazi moja tu ya kusoma. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuepusha migomo na maandamano yanayoweza kutokea kufuatia wanafunzi wengi kukosa mikopo na huku wakiwa na sifa stahiki za kupatiwa mikopo.
Naomba kutoa hoja, mawazo yenu tafadhali.