Chenge kuhukumiwa leo.......

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,461
2,000
Chenge kuhukumiwa leo

Imeandikwa na Flora Mwakasala; Tarehe: 16th December 2010 @ 06:56 Imesomwa na watu: 3; Jumla ya maoni: 0

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, leo inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili inayomkabili aliyewahi kuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge.

Hukumu hiyo inayotarajiwa kusomwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kwey Rusema, inatokana na kukamilika kwa ushahidi uliotolewa kutoka pande zote mbili katika kesi hiyo iliyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi minane sasa.

Kwa mara ya kwanza, Chenge ambaye ni Mbunge wa Bariadi Magharibi mkoani Shinyanga, alifikishwa mahakamani hapo Machi 28, 2009 akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili, kuharibu pikipiki ya matairi matatu pamoja na kuendesha gari lisilokuwa na stika ya bima.

Katika moja ya ushahidi wake kortini, Chenge alidai shahidi wa tatu wa upande wa mashitaka ana ugomvi naye, akidai shahidi aliiambia Mahakama uongo kuwa gari aliyokuwa akiiendesha haikuwa na bima.

Awali, akitoa ushahidi wake Agosti 23, mwaka huu, shahidi huyo Raydon Njeje, ambaye ni mwajiriwa wa Kampuni ya Bima ya Phonex alidai stika hiyo yenye namba za usajili 1919156, inamilikiwa na Evarist Sesa.

Njeje alidai kuwa stika hiyo ni ya gari lenye namba za usajili T571 AKH aina ya RAV4 ya rangi nyeusi na siyo ya gari aina ya Toyota Hilux iliyosajiliwa kwa namba T 513 ACE. Gari hilo ndilo alilokuwa akiendesha Chenge wakati alipopata ajali iliyoua watu wawili.

Shahidi huyo alidai stika iliyokuwa katika gari la Chenge lililohusika katika ajali si mali ya gari hilo aina ya Hilux analolimiliki (Chenge), bali ni ya gari aina ya RAV4 na ilisajiliwa kwa jina la Evarist Sesa.

Awali ilidaiwa kuwa Machi 27, mwaka jana katika Barabara ya Haile Selassie Oysterbay, mshitakiwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux Pick up namba T513 ACE aliigonga pikipiki ya matairi matatu (bajaj) yenye namba T736 AXC na kusabisha vifo vya Beatrice Costantino na Vick George.
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,531
2,000
hakuna la maana hapa we utasikia tu anapigwa faini ya sh 40,000 basi kesi kwisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom