Chenge kugombea Uspika kunastahili kukemewa hata kwa maandamano nchi nzima


M

Membensamba

Senior Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
157
Likes
0
Points
33
M

Membensamba

Senior Member
Joined Nov 4, 2010
157 0 33
Ndugu wanaJFs na watanzania wenzangu wote, kuna mambo ambayo mtu ukiyasikia unaweza kuyanyamazia kwa mshangao. Mengine mtu mwadilifu huwezi kamwe kuyanyamazia. Maana sio tu kuwa yanakera, yanachefusha roho. Swala la huyu bwana Chenge kuthubutu kuchukua form ya kugombea uspika kwa kweli linanifanya nitake kutapika utumbo.

Jamani uspika nio kazi ndogo. Bunge ni chombo kinachotuwakilisha wananchi katika kutunga sheria, kudhibiti mwenendo wa serikali ikiwa ni pamoja na kuiwajibisha. Ikumbukwe kuwa wenye nchi ni sisi wananchi, serikali ni watumishi wetu, tumewatuma, na kuwapa majukumu ya kulinda rasilimali zetu, na kutuongoza kufikia maendeleo hatua kwa hatua. Na Bunge limewekwa pale ili lihakikishe kuwa serikali tuliyoituma inafanya yale tunayoyataka kwa uadilifu wote. Ni kama ilivyo bodi ya wakurugenzi kwenye kampuni.

Sasa kama Bunge ni mdhibiti serikali na mkemeaji mkuu wa maovu au ubadhirifu wa serikali kwa niaba yetu, litaongozwaje na mtu ambaye mwenyewe ni fisadi wa kutupwa. Mwizi na mbadhirifu wa mali ya umma? Huyu Chenge si ndiye juzi tu aliyaita mamilioni yetu aliyoiba "vijisenti?" Huu mimi naona ni mpango wa makusudi wa kuwanyamazisha wapiga kelele dhidi ya ufisadi bungeni. Tusidanganyike kuwa eti kwa kuwa wako akina Lisu na wenzake Chenge atashindwa kuzuia kelele hizo. Kiongozi ni kiongozi tu, ukishampa hicho kiti usidhani unaweza kulazimisha mambo asiyoyataka yeye. Mmesahau kuwa Sita alilalamikiwa na chama chake kwa KURUHUSU mijadala iliyowaumbua? Ina maana kuwa alikuwa na uwezo wa kuizua. Spika asipokuruhusu bungeni huna la kufanya. Sio siri, Chenge hatakubali kamwe mafisadi wenzake wanyooshewe vidole.

Spika wa bunge ni askofu wa kisiasa. Haimpasi awe mtu anayelaumiwa, kwa kuwa yeye ni kiongozi wa chombo ambacho jukumu lake la msingi ni kudhibiti serikali na kuhakikisha kuwa inautumikia umma wa waTz. Huyu bwana HAFAI KABISA kuwa kiongozi wa chombo hiki.

Lakini kwa kuwa ccm yenyewe imeoza, inaweza kumpitisha tu, tena kwa shangwe, wakijua kuwa watapumua, wasibughubughudhiwe kwa ufisadi wao. Kwa hiyo waTz, kemeeni hili jambo kwa nguvu zote, ikibidi tutoke mitaani na mabango tukiandamana na kupinga CHENGE ASIWE SPIKA WA BUNGE LETU. CCM kumbukeni bunge sio lenu, hata kama mko wengi humo, BUNGE NI MALI WA WATANZANIA, ni chombo cha kazi SIO PANGO LA WANYANG'ANYI.
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,407
Likes
5,796
Points
280
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,407 5,796 280
CCM wamepata fundisho kubwa sana this time wasipoangalia watasababisha nchi iende kwa chadema 2015 najua JK hatakubali last term amabyo ameahidi tutamkumbuka aone shaghala bagala kama huo uozo!!!maana hata uwaziri jamaa alikataa kujiuzulu alipoulizwa na JK wakiwa ziarani....
 
Ringo Edmund

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2010
Messages
4,893
Likes
39
Points
0
Ringo Edmund

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined May 10, 2010
4,893 39 0
mimi nitasafiri hadi dodoma kwaajili ya kushuhudia makamanda wakiapishwa.ccm wakimpitisha chenge watatuulia palepale mjengoni.
mwizi ni mwizi tu.
 

Forum statistics

Threads 1,236,754
Members 475,220
Posts 29,267,790