Chenge jiuzulu Uenyekiti wa Bunge kwa kashfa hii ya kuliibia taifa kupitia mikataba mibovu ya madini

Anderson Ndambo

Senior Member
Jun 3, 2017
152
207
*Chenge jiuzulu uenyekiti wa Bunge*

Kila mmoja anaweza kuwa na kumbukumbu zake binafsi kuhusu jina la mwanasiasa anayeitwa Andrew John Chenge (Mb). Binafsi kumbukumbu zangu zinalihusisha jina hilo na kashfa ya chenji ya rada.

Kwa upande wako unaweza kulihusisha jina hilo na kashfa hii ya mikataba dhaifu ya madini, na mwingine akalihusisha jina hilo na jeuri ya fedha, hasa pale alipodai kwamba dola zaidi ya bilioni moja alizoficha katka akaunti yake kule ughaibuni, visiwa vya Jersey nchini Uingereza ni vijisenti tu – huku akitambua Watanzania wengi wanakosa dawa hospitalini na huduma nyingine za kijamii kwa ujumla.

Nikukumbushe tu kuwa Chenge ni Mwanasheria wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa ameshika nafasi hiyo kuanzia mwaka 1993 hadi 2005.

Udhaifu wa mikataba ya madini uliowekwa wazi leo kupitia ripoti ya Kamati ya Profesa Usolo umeanika udhaifu wa Chenge kitaaluma katika usimamizi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ambapo mikataba husika imeanza kuingiwa akiwa Mwanasheria Mkuu.

Huyu Chenge ni mzoefu katika kashfa za kifisadi – kila mara jina lake limekuwa likichomoza, taja kashfa ya kampuni ya Meremeta – yumo, taja kashfa ya rada - yumo.

Itakumbukwa kuwa Aprili 20 mwaka 2008 alilazimika kujiuzulu baada ya kubainika amehifadhi dola za Marekani milioni moja (zaidi ya Tsh bilioni moja) katika akaunti ya Jersey zilizotokana na ununuzi wa rada ya kijeshi kati ya Tanzania na Shirika la BAE-Systems la Uingereza.

Wapelelezi wa kitengo cha Serious Fraud Office (nchini Uingereza) ndio waliobaini mchezo mchafu wa Chenge na maofisa wengine wa serikali ya Tanzania, wasiowaaminifu ambao kwa sasa hawana nafasi tena katika Serikali ya Rais John Pombe Magufuli.

Bado naendelea kutafakari nikijiuliza ni kwa namna gani uchunguzi wa Takukuru ulimsafisha Chenge katika kashfa hiyo ya chenji ya rada, lakini haya sitaki kuyazungumzia leo. Kazi ya leo ni moja tu, kumtaka Andrew Chenge ajiuzulu nafasi ya uenyekiti wa Bunge, kwa kuwa karibu kila kashfa kubwa nchini jina lake linaibuka.

Mbele ya Rais Magufuli, leo Chenge ametajwa kuwamo katika orodha ya miongoni mwa watakaohojiwa kuhusu kashfa hii ya mikataba inayonuka ya madini.

Huyu ni mtuhumiwa na kwa kweli mtuhumiwa hapaswi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi wa Bunge hadi uchunguzi dhidi yake utakapokamilika.AJIUZULU. Najua kwa jeuri yake ya fedha sambamba na jeuri ya kisomi isiyokuwa na tija kwa taifa, hawezi kujiuzulu ubunge kwa sababu aliwahi kugoma kufanya hivyo wakati ule wa kashfa ya chenji ya rada, sasa, angalau ajiuzulu uongozi wa taasisi nyeti, taasisi ya Bunge ambayo Spika Ndugai leo ameweka bayana kuwa Bunge litakuwa nyuma ya Rais Magufuli– likiunga mkono hatua zote za kizalendo anazochukua Rais Magufuli. CHENGE JIUZULU HUNA UHALALI KISIASA KUONGOZA VIKAO VYA BUNGE

By Mwananzengo
Bariadi
 
Kwa haya yanayotokea juu ya Chenge kuhusika na kashfa zote za nchi hii na afanywi lolote basi naamini kuna mengi anayajua na akiamua tu kuwa upande wa wanyonge basi watamtoa roho kabla ya kuweka wazi anayoyajua.. Ndio maana Chenge hatofanya hivyo kulinda uhai wake.
 
Hili halina mjadala, ajiuzulu fasta. Ikiwezekana na ubunge avuliwe plus kesi ya uhujumu uchumi. ili awe ndani wakati kesi inaendelea possibly kesi ichukue hata 10yrs.
 
Very disgusting figure. ..hafai hafai hafai. Aache kuwatumikia watu aende kujitumikia mwenyewe
 
Mara nyingi tu wenye akili zao walishapiga kelele kuhusu huyo mzee lkn team bashite waliwaona hamnazo, leo ndo kurudia kula matapishi.
 
“Utakuta mtu anajidai anajua, mimi namwangalia tu kwa sababu wakati mwingine hajai kwenye kiganja changu.” — Andrew Chenge, mnyamaa
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom