Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,844
Chenge amesomewa mashtaka matatu likiwepo la kusababisha vifo vya watu wawili.
Ni kwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Emirius Mchaura.
Mwendesha Mashtaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi David Mafimbo.
Chenge anadaiwa kufanya makosa hayo Machi 27 mwaka huu majira ya 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selasie, karume eneo la Osterbay, Kinondoni.
Mafimbo: Katika shitaka la kwanza Chenge unashitakiwa kwa kusababisha kifo kupitia uendeshaji wa kizembe katika barabara ya umma, na maelezo ya kosa ni kwamba ukiwaunaendesha gari yenye Namba T. 513 ACE Toyota Hilux Double Cabin uliendesha gari hiyo kizembe na kushindwa kuchukuwa tahadhari kama inavyotakiwa huku ukiendesha upande wa kulia zaidi uliigonga Bajaji yenye namba T 736 AXC, kweli au si kweli?.
Chenge: Si kweli.
Mafimbo: Katika shitaka la pili, Chenge unashitakiwa kwa kusababisha vifo vya watu wawili, na maelezo ya kosa ni kwamba mnamo Machi 27 mwaka huu majira ya 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selasie, karume Osterbay wilaya ya Kinondoni ukiendesha gari bila kuchukuwa taadhari uliigonga Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili Victoria Gorge na Beatrice Constantini, kweli au si kweli?
Chenge: Si kweli.
Mafimbo : Shitaka la Tatu ni kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa bajaji, jibu kweli au si kweli?
Chenge: Si kweli.
Baada ya Chenge kukana mashtaka yake yote ASP Mafimbo alimweleza Hakimu Mchauru kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Definately majibu hapo yatakuwa si kweli. Kuendesha gari kizembe maana yake nini? kuendesha ni kuendesha tu. Huwezi kuhusisha neno uzembe liwe sawa na kuendesha (mfano) ukiwa umelewa!
Kwani hawakupima umbali wa michubuko ya breki kukadiria gari ilikuwa inakwenda mwendo gani? au hawawezi kutathmini mbonyeo wa gari husika na ki Bajaj kujua the force of an impact?
...shitaka la kukimbia eneo la tukio halikuhusishwa?
aaarrgghh, haya bana...wanasheria na sheria zao.