Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Wana JF -- kuna habari kwamba yule Bwana wa Vijisenti, Andrew Chenge anashikiliwa na polisi kituo cha Oysterbay kwa kuua watu wawili kwa kugonga Bajaj. Habari zaidi bado hazijapatikana. Tafadhali fuatilieni habari hizi.

IMG_9219.JPG

Gari la Chenge lililosababisha ajali

IMG_9218.JPG

Bajaj iliyongongwa na Chenge na kusababisha vifo
 
Last edited by a moderator:
Habari zaidi zinasema hakuua kwa risasi, bali aligonga Bajaj na kuua watu wawili, na Kova ataongea na waandishi asubuhi hii saa 5.
 
Unategemea nini?

Nchi haina Uongozi.

Viongozi wote wanaogopana. Wote wanamaovu. ...

Hakuna wa kusimama na kukemea. Anaogopa watarudisha majibu!

SO?

Kila mtu ni kiongozi.

Polisi anasimama popote anaua!

Kila mtu ni mwana siasa...atafanya anachofanya..atafanywa nini? Kwani wao wamefanywa nini?

Kila mtu anaita vyombo vya habari ...anabwabwajika ..iwe hovyo au with sense. Kila mtu ni kiongozi...Tena ajiona wa kutukuka!!

Kila mtu ni kiongozi na kila mtu anaweza kuchukua sheria na kuitumia anvyotaka.Hakuna kkiogozi mwanye ujasiri wa Ukweli na haki..

Mkuu wa wilaya....Mwalimu mkuuu...Balozi....Kibaka....All is just hopelesss!!

Kwanini Chenge asifanye alivyofanya? Haswa Chenge? why not?

Ujeuri unaonyeshwa na wengine umefanyiwa nini? Kwani yeye hana jeuri? Kwani jeuri ya Kagoda imefanywa nini? Kwani jeuri ya mitambo ya umeme etc imefanywa nini?

Kwani yeye hana jeuri? Just shoot!!!!

Nchi imekuwa ya kuchezewa na kila mtu sasa!!!

Ni mpaka Viongozi watakapo ondoa DHIHAKA na USWAHIBA na kufanya kazi tuliyowapa ...ndipo tanzania itarudi kwenye mstari...vinginevyo....?...Unaweza kubunia!!!
 
Ah kumbe ajali!! Utamu wote ushapotea . Aksante anyway.

Alikuwa anaendesha yeye personally au driver?
 
Kesi ndogo hiyoo kwanza atasema sikuwa naendesha mimi.....atapelekwa driver dak 20 atatolewa mahakamani dhamanaa....baada mwezii anapigwa fine mchezo umeisha
 
Balaa zimeanza kumwandama.
Safari ndeeefu ya chenge ktk vyombo vya sheria itaanza sooon.
patience wakulu tuone yatakayojiri
 
ni kweli yuko kituoni oysterbay na waandishi wa habari kibao wako pale wanasubiri apelekwe kwa pilato.
 
haijulikani alikuwa katika mwendo gani wakati tukio hilo linatendeka na muda gani kama ni asubuhi hii ni njia gani hiyo inayopitisha magari ya kasi hivyo mpaka kusababusha maafa hayo -- lakini bado kuna suala la usalama wa abiria wanaobebwa na hizi majaj kwa siku za karibuni kumetokea habari nyingi za bajaj kugongwa au kuacha njia kutokana na ipepo mkali mfano mzuri ni ile njia ya afrikana kwenda whitesands na jangwani kule kila mara ni ajari za majaj na piki piki
 
Alikuwa anaendesha yeye mwenyewe. Ajali ilitokea jana usiku na aligonga bajaji kwa nyuma na kuiburuza umbali mrefu kidogo kiasi cha kuwezakupoteza maisha ya wasichana wawili. Anatarajiwa kufikishwa mahakama ya kinondoni.

Kesi yake inasubiri wakuu wa police kutokana na wadhifa wake serikalini. Ilikuwa saa tisa usiku wa kuamkia leo asubuhi.
 
Kama ni ajali, basi bahati mbaya. Ajali haina kinga. Sidhani kama ataweza kumgonga mtu kwa makusudi pamoja na jeuri aliyo nayo!! Tuwape pole wafiwa na kuwaombea furaha ya milele waliofariki. Hata Vijisenti tumpe pole kwa yaliyompata. Huo ndiyo uungwana.
 
Wajameni!!!
Sasa hapo mahakama ina kazi yule Mallya alikuwa hana leseni hakuna aliyemwona akiendesha gari lililomwua CHACHA Wangwe,,amekula mvua tatu. Vijisenti Mungu ana mpango mahsusi nae sasa anaitia serikali ya Mkwere majaribuni! SFO walisema amekula rushwa yeye na Dr. Idris Rashid! Kikwete akamwamuru DPP kijana wa Chenge Asiwashitaki sasa hili la ajali ni Mungu anataka angalau Chenge alale Keko kama ishara lakini e bwana wee ataachiwa tu . Hata marehemu Ditto aliyekuwa Mshenga wa JK alitolewa kwa mbinde lakini Sir God akamchukua!!!! Hizo Bajaji zimeruhusiwa na Bunge kwa shinikizo la mafisadi wa Kihindi zitachinja kinoma sijui wataongeza matuta. Kule Nigeria waliruhusu pikipiki jana niliona polisi wakizikamata kwani hawavai HELmets na zimewaua wanigeria kibao inakimbizana na HIV aids kwa kua !!wao badala ya kujenga barabara za juu kama Afrika kusini na ulaya wakaruhusu pikipiki ziwahishe watu ahera. Watanzania kwa kuiga rikshaw za kihindi tutakwisha. Hao madereva hata leseni hawana sasa sijui wataandika ubavuni wapi? Tungojee ya Vijisenti as they develop!!
 
Unategemea nini?

Nchi haina Uongozi.

Viongozi wote wanaogopana. Wote wanamaovu. ...

Hakuna wa kusimama na kukemea. Anaogopa watarudisha majibu!

SO?

Kila mtu ni kiongozi.

Polisi anasimama popote anaua!

Kila mtu ni mwana siasa...atafanya anachofanya..atafanywa nini? Kwani wao wamefanywa nini?

Kila mtu anaita vyombo vya habari ...anabwabwajika ..iwe hovyo au with sense. Kila mtu ni kiongozi...Tena ajiona wa kutukuka!!

Kila mtu ni kiongozi na kila mtu anaweza kuchukua sheria na kuitumia anvyotaka.Hakuna kkiogozi mwanye ujasiri wa Ukweli na haki..

Mkuu wa wilaya....Mwalimu mkuuu...Balozi....Kibaka....All is just hopelesss!!

Kwanini Chenge asifanye alivyofanya? Haswa Chenge? why not?

Ujeuri unaonyeshwa na wengine umefanyiwa nini? Kwani yeye hana jeuri? Kwani jeuri ya Kagoda imefanywa nini? Kwani jeuri ya mitambo ya umeme etc imefanywa nini?

Kwani yeye hana jeuri? Just shoot!!!!

Nchi imekuwa ya kuchezewa na kila mtu sasa!!!

Ni mpaka Viongozi watakapo ondoa DHIHAKA na USWAHIBA na kufanya kazi tuliyowapa ...ndipo tanzania itarudi kwenye mstari...vinginevyo....?...Unaweza kubunia!!!

Hapo sheria si itapindishwa tuuuu!

Eeeeh Mungu Ibariki Tanzania tuepushe na maadui dhidi yetu ili JF idumu tuzidi kuwajua watanzania walivyo wakarimu na moyo wa upendo, asante baba kwa jina takatifu nawasilisha sala yangu.

Polesa sana ndugu Chenge, pamoja na ufisadi ulionao hili ni tatizo la kawaida na linaweza kumpata yeyote ambaye ni mdau kweny vyombo vya moto.
Mwenyezi Mungu zilaze roho za marehemu mahalai pema peponi, utupe moyo wa kujipa tahadhari, wape hekima viongozi wetu watambue usafiri wa bajaj na piki piki si salama wakati wa usiku na hata hao wanaoendesha vyombo hivyo sio madereva waliofuzu
 
Balaa hiyo imeanza? sasa saa tisa za usiku alikuwa anatoka wapi mzee wa visenti au ndio kwenye vikao vya mafisadi? Ila ana vijisenti ataachiwa tu hata kama ana kosa. Wamempima kilevi kwenye damu wakati huo. Itaambiwa bajaji imemgonga. Gonga wewe uone?
 
Alikuwa anaendesha yeye mwenyewe. Ajali ilitokea jana usiku na aligonga bajaji kwa nyuma na kuiburuza umbali mrefu kidogo kiasi cha kuwezakupoteza maisha ya wasichana wawili. Anatarajiwa kufikishwa mahakama ya kinondoni.

Kesi yake inasubiri wakuu wa police kutokana na wadhifa wake serikalini. Ilikuwa saa tisa usiku wa kuamkia leo asubuhi.

TISA UCKU??? LAZIMA ALITOKA KWA MGANGA HUYO, ushahidi tosha hata bungeni ucku alikuwa yeye akimwaga upupu ...
 
Back
Top Bottom