Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,826
2,000
1539.jpg

1538.jpg

1536.jpg

1527.jpg

1523.jpg

Polisi akiokota mabaki ya bajaji bila kuvaa gloves

1521.jpg

1520.jpg

1528.jpg

Sakata lingine lilikuwa kwa familia ya Chenge hasa upande wa mtoto wake wa kike ambaye aliondoka kituo cha Polisi na kwenda nyumbani kubadilisha nguo mara ya kwanza alikuwa amevalia suruali na brauzi , akaenda kubadili na kuvaa gauni jambo liliwashangaza baadhi ya watu waliofurika hapo polisi,
Pia muda wote alikuwa bize akiongea na simu huku akiwa amevalia miwani meusi.Picha zaidi gonga http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=265671http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=265671http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=265671

Either alijikojolea ama ni mambo ya ushirikina hayo,tutaona mengi sana.
Hata hivyo inasikitisha sana kuona polisi hao wakishughulika kiholela,ukicheki picha utaona kwamba wanatafuta mazingira ya kumaliza kesi na si kusaidia upelelezi wa kesi....Gari ilivyoharika hapo mbele inashangaza sana ni kivipi aliendesha hado nyumbani kama vile it wasn't such a big deal,bajaji imegongwa nyuma lakini ni wazi gari ya Chenge iliwagonga marehemu moja kwa moja,(direct hit) either iliwachanganya marehemu na Bajaj,ama ni kwasababu Bajaj iko wazi na hivyo ikawa rahisi kwa gari ya Chenge kuwagonga wao moja kwa moja bila kuwa na kizuizi,kuna wanaosema gari ya Chenge ili wadrag marehemu kwa umbali flani,hilo linawezekana kwani inaonyesha hapo kwa chini mbele kwenye hiyo pick up kulikuwa na mwili uliokuwa direct hit kwani kuna mabaki ambayo bado yako stucked,na kwasababu hakusimama,basi aliwamalizia mbali.

Anyways,kama ni ajali basi tu,ila inasikitisha sana.
 
Recta

JF-Expert Member
Dec 8, 2006
855
195
Na hata kama huyo dereva hajapatikana,bado kuna ushahidi wa kutosha tu wa kupress charges,kuna aliyekuwa akiendesha bila insurance,akiwa mlevi na kwenda kuigonga Bajaj na raia wema kina dada wa watu,pia hakusimama na alikwenda polisi kesho yake.

Mkuu jmushi1, ninavyofahamu mimi mpaka sasa hivi ni kwamba, ajali hiyo imetokea leo asubuhi majira ya saa 10. Sidhani kuwa alikwenda polisi kesho yake, kwasababu ili hiyo iweze kuwa kweli, inabidi muda huu upite hadi itakapopita saa usiku huu.
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,397
2,000
1539.jpg

1538.jpg

1536.jpg

1527.jpg

1523.jpg

Polisi akiokota mabaki ya bajaji bila kuvaa gloves

1521.jpg

1520.jpg

1528.jpg

Sakata lingine lilikuwa kwa familia ya Chenge hasa upande wa mtoto wake wa kike ambaye aliondoka kituo cha Polisi na kwenda nyumbani kubadilisha nguo mara ya kwanza alikuwa amevalia suruali na brauzi , akaenda kubadili na kuvaa gauni jambo liliwashangaza baadhi ya watu waliofurika hapo polisi,
Pia muda wote alikuwa bize akiongea na simu huku akiwa amevalia miwani meusi.Picha zaidi gonga http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=265671

hiyo picha ya binti ambaye aliwashangaza wengi, ni ipi? ilituthibitishe tuhuma au sifa uliompa. namba ya jpg pls.
 
Adili

JF-Expert Member
Nov 3, 2007
3,142
2,000
Sasa hapa ndio kesi inatakiwa iwe moto, sababu kwanza ni hit and run, pili ni lazima yeye aprove beyond resonable dought kwamba alikuwa sober. Nadhani hapa ndio mahala muafaka kwa kumfunga maisha huyu jamaa... Hii ingekuwa nchi za west District attorney angkuwa anashangilia, maana kubuild hii kesi ni simple.
Moja ameuwa bila kukusudia lakini akiwa amelewa
Pili, ni hit and run ambayo nadhani ni crime kwa Tanzania.
Combine hizi mbili then unaweza kumpeleka more than 20yrs jela.... Kama muendesha mashitaka kasoma sheria na sio kubabi hii kesi ni easy kushinda.

Ongeza kumgonga mwenzako ukitokea nyuma!
Mhe. ana kesi ngumu!
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,826
2,000
Mkuu jmushi1, ninavyofahamu mimi mpaka sasa hivi ni kwamba, ajali hiyo imetokea leo asubuhi majira ya saa 10. Sidhani kuwa alikwenda polisi kesho yake, kwasababu ili hiyo iweze kuwa kweli, inabidi muda huu upite hadi itakapopita saa usiku huu.

Tatizo ni kwamba hakuripoti tukio wakati ule ule,kuliondoa gari lile eneo la ajali ni kosa baya kuliko hata kukimbia na kuliacha gari kwani ushahidi unakuwa preserved,sasa unaona polisi wenyewe hata gloves hawajavaa,ni wazi nia yao ni kulipuwa kazi imalizike kwani picha inaonyesha jamaa anakusanya ushahidi kama vile anakusanya nguo zake kwenda kufua ama furushi la mitumba ama taka taka za kwenda ku dispose off.
Pia inasemekana dereva aliruka alipoona anagongwa,that means Bajaj ilikuwa imesimama,hauwezi kumchomekea mtu halafu eti upate nafasi ya kuruka,watu wanajua maana ya kuchomekea? Ina maana distance ni fupi,kama ni kweli aliruka wakati anaendesha Bajaj,basi ni wazi Chenge na yeye alikuwa na distance ya kutosha kumwezesha kujaribu kukwepa ajali,tofauti na hapo bajaj ilikuwa imesimama...Hilo liko wazi base on common sense.
 
Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,610
1,250
Hata barara zenyewe zimekalia kusababisha ajali,hivi taa za barabarani zilikuwa zikiwaka ,halafu hiyo Bajaj inaonekana iligongwa kwa mbele ,watu habari inaonesha wamepotosha ukweli ,kwa jinzi picha cinavyoonekana ni kuwa hii ilikuwa face to face.
 
Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,610
1,250
Dah izo picha zinawaonyesha watoto ,kwa kweli Tz ni shida ndio mnaona wenyewe hapo ,sisi tunayajua maana tupo katikati ya jiji,si mnawaona hao watoto hata nywele hawana ,nywele zinakataa kuota kwa ziki ,hawana lishe bora.Ndio maana yake.Hakuoti kitu.
 
Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,610
1,250
Polisi anaokota vizibiti hana hata gulovu. Hivi akihojiwa kwa nini hakuvaa glovez atajibu nini ?
 
Recta

JF-Expert Member
Dec 8, 2006
855
195
Ohooo!

Habari ninazozipata sasa zinadai wameenda na mkuu Andrea Chenge kwenye eneo la tukio, ndo wamerudi kituo cha polisi O'bay sasa hivi.

Kifupi, inasemekana Chenge alikuwa anaendesha gari ambalo Insurance (bima) yake ime-expire (imeisha muda wake) tangu 2007

Mkuu Invisible, inawezekanaje kuwa gari alilokuwa akitumia Mhe. Chenge lilikuwa halina insurance (ime expire) wakati sticker ya usalama barabarani inaonekana kwenye windscreen kuthibitisha kuwa lilikaguliwa na afisa wa usalama barabarani siku za karibuni zaidi?
 
Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
0
Cha kushangaza zaidi gari la Mh,Chenge alilopata nalo ajali lilikuwa halina insurance ya mwaka huu kwani aliyokuwa aikitumia ni ya mwaka 2007 ambayomtayari muda wake umeshaisha zaidi ya miaka 2.

1537.jpg
 
Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Ah, alikuwa anaendesha gari bila insurance na kugonga watu na wakafa? Hakuna jinai hapo? Hebu tufafanulieni wataalamu wa sheria.
 
Moelex23

JF-Expert Member
Oct 8, 2006
501
250
statement ya chenge, kupitia habarileo::::

""""Bajaj ile ilikuwa inataka kupita gari jingine lililokuwa likitoka Morogoro Stores, bahati mbaya kukawa na gari lingine linakuja, ile bajaj ikabana upande wangu na mimi nilikuwa katika mwendo wa kati ya kilometa 80 hadi 100 kwa saa," alidai Chenge. Alidai kuwa baada ya kuona bajaj ile inakwepa gari la mbele wasigongane uso kwa uso, alirudi upande wa kulia ndipo alipoigonga ubavuni kushoto. "Gari la nyuma lingesimama, dereva wake angeweza kueleza vizuri, ila baada ya ajali nikasikia watu wanaita 'Chenge! Chenge!' nikajua niko salama, nikashuka," alidai. ""

Conclusion yangu ni kuwa:::

Chenge ndiye aliyekuwa anataka kuipita bajaj kwa mwendo wa kasi, na alipoona kuna gari linakuja upande wa kulia akakwepa head on collision ndio akarudi kwenye lane iliyokuwa bajaj, na kuigonga kwa upande wake wa kushoto.

Swali gumu nalopata ni kwanini dereva wa bajaj kakimbia?? Sioni sababu yoyote ya yeye kukimbia?? Je amekimbia au kawekwa sehemu?? Nadhani utata wote upo hapo, lakini kiutaalamu hii accident picha na maelezo ya chenge, conclusion ni hiyo tu, yeye ndiye aliyekuwa anataka kuovertake.
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,522
2,000
statement ya chenge, kupitia habarileo::::

"""“Bajaj ile ilikuwa inataka kupita gari jingine lililokuwa likitoka Morogoro Stores, bahati mbaya kukawa na gari lingine linakuja, ile bajaj ikabana upande wangu na mimi nilikuwa katika mwendo wa kati ya kilometa 80 hadi 100 kwa saa,“ alidai Chenge. Alidai kuwa baada ya kuona bajaj ile inakwepa gari la mbele wasigongane uso kwa uso, alirudi upande wa kulia ndipo alipoigonga ubavuni kushoto. "Gari la nyuma lingesimama, dereva wake angeweza kueleza vizuri, ila baada ya ajali nikasikia watu wanaita 'Chenge! Chenge!’ nikajua niko salama, nikashuka,“ alidai. ""

You'd make a damn good investigator.
 
Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
1,195
1539.jpg

Chenge alirudije nyumbani?

Wanamwita Chenge "Harvard Lawyer," ambaye hakujua kwamba you never leave the scene of an accident!

Akiendesha 80 to 100km/hr (up to 60 miles/hr) mitaa ya Morogoro Stores, Oysterbay, residential areas!

Hanunui insurance, tajiri mkubwa, Mbunge mtunga sheria na maadili ya CCM, former AG, "Harvard Lawyer."
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,826
2,000
statement ya chenge, kupitia habarileo::::

"""“Bajaj ile ilikuwa inataka kupita gari jingine lililokuwa likitoka Morogoro Stores, bahati mbaya kukawa na gari lingine linakuja, ile bajaj ikabana upande wangu na mimi nilikuwa katika mwendo wa kati ya kilometa 80 hadi 100 kwa saa,“ alidai Chenge. Alidai kuwa baada ya kuona bajaj ile inakwepa gari la mbele wasigongane uso kwa uso, alirudi upande wa kulia ndipo alipoigonga ubavuni kushoto. "Gari la nyuma lingesimama, dereva wake angeweza kueleza vizuri, ila baada ya ajali nikasikia watu wanaita 'Chenge! Chenge!’ nikajua niko salama, nikashuka,“ alidai. ""

Conclusion yangu ni kuwa:::

Chenge ndiye aliyekuwa anataka kuipita bajaj kwa mwendo wa kasi, na alipoona kuna gari linakuja upande wa kulia akakwepa head on collision ndio akarudi kwenye lane iliyokuwa bajaj, na kuigonga kwa upande wake wa kushoto.

Swali gumu nalopata ni kwanini dereva wa bajaj kakimbia?? Sioni sababu yoyote ya yeye kukimbia?? Je amekimbia au kawekwa sehemu?? Nadhani utata wote upo hapo, lakini kiutaalamu hii accident picha na maelezo ya chenge, conclusion ni hiyo tu, yeye ndiye aliyekuwa anataka kuovertake.

Hii habari inazidi utata tu,mara alichomekewa mara sijui nini....Kwanza tunajuwa sheria zaetu za barabarabi ni keep left,sasa mtu aliyekuwa mbele yake alienda vipi upande wa kulia na wakati gari ya Chenge yenye we imepondeka upande wa kushoto?
Ama sheria za barabarani zimebadilika..Kama kuna mwenye kuweza kutueleza vizuri hapo ningeshukuru maana sijaielewa hii...Mtu akiwa mbele yako akijaribu kulipita gari jingine anakuwa upande wako wa kulia,na akirudi anakuwa mbele yako...Sasa what the heck is this kwamba yeye alimgonga ubavuni?
Halafu anasema gari ilikuwa inatokea morogoro store,means haikuwa kwenye lanes bali iikuwa inaingia barabarabi,sasa Bajaj ilikuwa inaikwepa ama ina overtake? Duh!
 
Jan 16, 2007
721
0
Changa la macho!Kwa kitendo cha ajari na kuua watu na kujisalimisha polisi kisheria sawa lakini kama ajali na mtu kama change kutiwa ndani wakati uchunguzi unaendelea ili ni changa la macho kwani tukio lake tofauti na la Ditto ambae alimpiga mtu risasi.Ingeniingia kichwani kama Change angelijisalimisha katika vyombo vya sheria kwa tuhuma za rushwa na ufisadi.Tunafahamu ya kua serikali ya Uingereza imekamilisha uchunguzi wake na kuwataja wahusika.Hapa serikali badala ya kuchukua hatua na kumkamata mtu huyu kwa makosa ya ufisadi na kumkabidhi katika vyombo vya sheria wanaanza kuzusha makosa mengine ili kutupoteza na kutusahaulisha makosa makubwa yanayomkabili Mzee wa visenti sasa gumzo wanataka kulihamishia katika ajali.Sitashangaa kama hiyo ajali imepangwa au hakuwepo kabisa hilo ni changa la macho.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mwazange

JF-Expert Member
Nov 16, 2007
1,056
1,225
Hivi jamani hatuwezi kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja? Kwa nini tusimuulize kuhusu kashfa nyingine lakini?....unamuanzishia tu 'by the way' vipi kuhusiana na kashfa zinazokutanda ndugu muheshimiwa??
Akituponyoka hapo tunaweza tusimpate tena huyo.....
Lakini kweli mjua sheria ndio mvunja sheria....Attorney General hajui kama kuendesha gari bila ya bima ni kosa Tanzania??? Ama kweli....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom