Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,748
2,000
Chenge amesomewa mashtaka matatu likiwepo la kusababisha vifo vya watu wawili.

Ni kwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Emirius Mchaura.
Mwendesha Mashtaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi David Mafimbo.
Chenge anadaiwa kufanya makosa hayo Machi 27 mwaka huu majira ya 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selasie, karume eneo la Osterbay, Kinondoni.

Mafimbo:
Katika shitaka la kwanza Chenge unashitakiwa kwa kusababisha kifo kupitia uendeshaji wa kizembe katika barabara ya umma, na maelezo ya kosa ni kwamba ukiwaunaendesha gari yenye Namba T. 513 ACE Toyota Hilux Double Cabin uliendesha gari hiyo kizembe na kushindwa kuchukuwa tahadhari kama inavyotakiwa huku ukiendesha upande wa kulia zaidi uliigonga Bajaji yenye namba T 736 AXC, kweli au si kweli?.

Chenge: Si kweli.

Mafimbo: Katika shitaka la pili, Chenge unashitakiwa kwa kusababisha vifo vya watu wawili, na maelezo ya kosa ni kwamba mnamo Machi 27 mwaka huu majira ya 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selasie, karume Osterbay wilaya ya Kinondoni ukiendesha gari bila kuchukuwa taadhari uliigonga Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili Victoria Gorge na Beatrice Constantini, kweli au si kweli?

Chenge: Si kweli.

Mafimbo : Shitaka la Tatu ni kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa bajaji, jibu kweli au si kweli?

Chenge: Si kweli.
Baada ya Chenge kukana mashtaka yake yote ASP Mafimbo alimweleza Hakimu Mchauru kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Definately majibu hapo yatakuwa si kweli. Kuendesha gari kizembe maana yake nini? kuendesha ni kuendesha tu. Huwezi kuhusisha neno uzembe liwe sawa na kuendesha (mfano) ukiwa umelewa!

Kwani hawakupima umbali wa michubuko ya breki kukadiria gari ilikuwa inakwenda mwendo gani? au hawawezi kutathmini mbonyeo wa gari husika na ki Bajaj kujua the force of an impact?

...shitaka la kukimbia eneo la tukio halikuhusishwa?

aaarrgghh, haya bana...wanasheria na sheria zao.
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,589
2,000
Chenge= Vicky!!!!!???? There is a hidden agenda in them!!!! Uchunguzi wa kina ukifanyika tutapata mengi kuhusiana na ajali hii na wahusika(Chenge, Vick, Beatrice). At that dead hour driving??? From where??? Was it a coincidence kukutana pale kwenye scene i.e pale alipowagongea???

Uchunguzi wa kweli ukifanyika kuanzia Mwanza tracing ya communication ya mobile ya Vick plus that of Chenge then tutapata jambo hapo. Tuanzie hapo then mengine yaendeleee!!!!!!

At the same time, Chenge anathubutu kutabasamu, nilitegemea angekuwa na simanzi. Nashauri apelekwe kupimwa akili!!!!! Ningekuwa mimi Chenge, ningekuwa nimezimia sijaamka.Tena nisingeweza kujieleza kwa sasa, ningehitaji muda ili niweke akili sawa. Yaani hajali binadamu kabisa, au kwa kuwa anajua pengine kulikuwa na bifu katia yao?? Alikuwa anawakimbiza hao kina dada/mama!!!!

Low class Chenge, Bull sheet.
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
1,225
Ah hebu wanasheria nisaidie maana mimi pale Laws sikukaaga sana. Hivi nini maana ya kukana mashtaka wakati kweli kakosa? Sielewi anapokataa kugonga wakati kagonga na kuua? Mi hata sielewi
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,814
2,000
Uta define vipi kuendesha gari kizembe?

Mimi nilifikiri wataweka pia kuendesha gari kwa speed kubwa (80km/h) kinyume na barabara husika?

Mzee wa Visenti atashinda hii case au kuambiwa alipe fidia.

Ila dunia hii matatizo yakikuanza hayatoki kirahisi.
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,589
2,000
Chenge nakuambia hizi roho za hawa akina mama na majonzi ya watoto wao half orphans vitakugeukia. You will pay for them soon!!

Kesi yenyewe imeshapikwa, Nilitegemea ningeona kuwa kosa kubwa ni hit and run. Kwa nini aligonga na kuua badala ya kwenda polisi akaenda nyumbani?? Anajidai na pesa ila si mwisho wa kila kitu hapa duniani. Atakuwa amehonga sana ili mashtaka yake yawe mepesi? Ndiyo maana wale askari walikuwa wanakenyua meno kwani wanajua chakula cha ulaini kimekuja!!!

Natamani kulia jamani.

Chenge anza kuomba msamaha mkeo!!!! Naamini umeshamfanyia vituko vingi sana vya umalaya (data zipo). Umechukua wake za vigogo wenzako kwa majigambo (data zipo). Umesababisha wanawake vigogo kuwekeana bifu kwa sababu yako, tena wengine ni watendaji wakubwa serikalini (data zipo). Ulisababisha kiongozi mwandamizi serikalini kupata stress ya hali ya juu pale ambapo unatembea na mke wake, na kwa bahati mbaya wakamleta baba huyo katika wizara yako (data zipo). Chenge wewe ni mchafu.
 
Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,951
2,000
inavyosemekana ni kuwa Chenge na marehemu vicky walikuwa ni marafiki wa muda mrefu.

ila siku ile ya tukio,walikuwa wakipata kinywaji pamoja akiwa na rafiki yake huyo waliepata ajali pamoja. ilipokuwa inakaribia hiyo saa kumi alfajiri walikorofishana chenge na huyo vicky,ndipo wakaamua kuchukua kibajaj waondoke zao kwa hasira. huyu bwana aliporudi akaambiwa jamaa wameshaondoka na kibajaj,ndipo akaamua kuwafukuza alipkuwa karibu kukifikia akajaribu kubloc kwa mbele ndipo ajali ikatokea.

Kwa hiyo habari ndiyo hiyo,mama nae kule mwanza kathibitisha mahusiano ya chenge na binti yake huyo kwa hiyo wasitupige changa la macho.!!!!!!

Ya leo kali, mbona hadithi hii inakuwa kama ina ukweli fulani kasoro tu kuwa kama Chenge angeblock kwa mbele si bajaj ndiyo inge mgonga na dreva wa bajaj kuumia. Picha zaonyesha gari ya Chenge imebondeka mbele kushoto ila baja sina uhakika kama ni nyuma au mbele!!!
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,947
2,000
Mafisadi wametuibia na kutufanya tuishi kwa taabu na dhiki tukiwahoji wanasema "hivyo ni visenti tu" kwa kutukejeli na sisi tunabaki kunung'unika tu.
Sasa wana ua na kutabasamu huku wapambe wao wanakejeli umasikini wetu, MNADHANI NINI KITAFUATA? maana kunung'unika kwetu pekee hakuwastui hata kidogo.
 
macinkus

JF-Expert Member
Sep 15, 2007
260
170
pale mwanzo, ilisemwa chenge alikuwa hana bima kwenye gari lake. ilikuwepo ya 2007. sasa inasemekana bima ilikua kwenye gari/ au alikua ameisahau nyumbani!!! kwa sasa kwa kua kuna kampuni nyingi za bima sio kweli kwamba hiyo bima iliyopatiana baada ya juzi imekatwa baada ya ajali na kuwa backdated ili kukwepa kosa jingine la kuendesha gari kwenye barabara ya umma bila bima?

bongo kila kitu kinawezekana.

macinkus
 
Ng'azagala

JF-Expert Member
Jun 7, 2008
1,287
1,250
Dereva wa Bajaj yu wapi?????????????????????????????????????
kakimbia au kafichwa???????????????????
 
Zion Train

JF-Expert Member
Jun 5, 2008
501
195
ninashindana na fikra zanzu, mara zinasema inawezekana mara haiwezekani, nimeona ngoja nishare nanyi ninachofikiria, mie naona kama chenge anamlinda mtu wa familia yake ambaye inawezekana ndiye amefanya ajali hiyo na kukimbia,yeye kama yeye anajijua ni chenge kainunua, hainipi kabisa mtu upate ajali na wenzio wamekufa wewe siku ya pili hupo kwenye eneo la tukio unachekelea kama hamna kubwa lililotokea,hivi msichana wake tuliyeambiwa mwanzoni kwamba alikuwa akibadili badili nguo nihaje?ni fikra zangu tu.
 
Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
1,195
Wanasheria wa Bongo wanatia huruma walivyomsomea shitaka Chenge.

Chenge, kosa la kwanza unashitakiwa kwa kuendesha kizembe na kusababisha.......kweli, si kweli?

Mimi ningejibu: Kweli, nashitakiwa!
 
Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,951
2,000
Mbona hawajamfungulia na shitaka la kuendesha gari huku akijua Insurance yake imekwisha toka 2007?
Hapo mnategemea kesi ya rushwa itafunguliwa hapo endeleeni kuvuta shuka tu mtu tayari anapeta uswazi kama kawa.
 
Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,603
1,500
Mwanzoni kabisa nilisema kama muendesha mashitaka ana akili, basi hii kesi ndio njia pekee ya kumfunga Chenge. Lakini nilivyoona hizo argument zake naona kabisa kwamba hakuna kesi hapo, Chenge ni mwanasheria na anaujua mfumo wa sheria ya Tanzania nje ndani. Sasa kama utabuild case kishenzi shenzi kama huyo muendesha mashitaka then at the end of the day Chenge will get away from this.

Point kubwa ya kuanzia kwanza ni kutofautisha mchele na chuya. Jee chenge anamjua kweli mmoja wa waliokufa? Na kama anamjua jee wanajuana vipi? Jee masaa machache kabla ya chenge kuingia barabarani alikuwa wapi? Na kama kuna ushahidi unaodai alikuwa Kempiski, Jee muendesha mashitaka anaweza kutumia nguvu ya kimahakama kuwahoji wadumu wa Kempisiki kuelezea kwamba Chenge alikuwa na nani? Jee alikunywa pombe gani?? Na kwa wingi gani? Jee alikuwa anaendesha gari akiwa na akili zake timu, kutokana na benchmark za Tanzania. Baada ya hapo unamsaka dereva wa bajaji nae aweke statement zake sawa.....

Vinginevyo Chenge atashinda.
 
Tuandamane

JF-Expert Member
Feb 2, 2008
1,221
1,225
Chenge amesomewa mashtaka matatu likiwepo la kusababisha vifo vya watu wawili.

Ni kwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Emirius Mchaura.
Mwendesha Mashtaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi David Mafimbo.
Chenge anadaiwa kufanya makosa hayo Machi 27 mwaka huu majira ya 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selasie, karume eneo la Osterbay, Kinondoni.

Mafimbo:
Katika shitaka la kwanza Chenge unashitakiwa kwa kusababisha kifo kupitia uendeshaji wa kizembe katika barabara ya umma, na maelezo ya kosa ni kwamba ukiwaunaendesha gari yenye Namba T. 513 ACE Toyota Hilux Double Cabin uliendesha gari hiyo kizembe na kushindwa kuchukuwa tahadhari kama inavyotakiwa huku ukiendesha upande wa kulia zaidi uliigonga Bajaji yenye namba T 736 AXC, kweli au si kweli?.

Chenge: Si kweli.

Mafimbo: Katika shitaka la pili, Chenge unashitakiwa kwa kusababisha vifo vya watu wawili, na maelezo ya kosa ni kwamba mnamo Machi 27 mwaka huu majira ya 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selasie, karume Osterbay wilaya ya Kinondoni ukiendesha gari bila kuchukuwa taadhari uliigonga Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili Victoria Gorge na Beatrice Constantini, kweli au si kweli?

Chenge: Si kweli.

Mafimbo : Shitaka la Tatu ni kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa bajaji, jibu kweli au si kweli?

Chenge: Si kweli.
Baada ya Chenge kukana mashtaka yake yote ASP Mafimbo alimweleza Hakimu Mchauru kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hakimu Mchauru aliweka wazi masharti ya dhamana ambapo alimweleza mshtakiwa kuwa anatakiwa kusaini hati ya dhamana ya milioni 1/- NA kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini hati ya dhamana ya milioni 1/-.

Chenge alikamilisha masharti hayo ya dhamana aliyotakiwa kuyatekeleza na kesi imeahirishwa hadi 30 April mwaka huu.

Kesi iifanyika chumba kidogo cha mahamama alichukuwa takribani dakika 10 hadi 15 tangu Chenge alipowasili mahakamani hapo, ambapo alifika na kupitiliza moja kwa moja kwenye chemba na hakimu kuanza kuendesha kesi huku waandishi wa habari wakisikiliza kesi wakiwa nje ya chumba kutokana na chumba hicho kuwa na nafasi ndogo isiyotoshereza watu wengi kuingia.

Nje ya mahakama ndugu wa Chenge walisikika wakiwasema vibaya waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo na kutaka kuwazuia wasimpige picha Chenge.

“Hivi mnazani kwakumpigapicha ndugu yetu mtaondokana na umaskini? Kama mnadhani mtatajirika kutokana na kesi hii ya leo basi tutaona kama mtaondokana na umaskini,” alisikika mmoja wa ndugu wa Chenge akiwaambia waandishi wa habari.

Umati wa watu ulifurika katika mahakama hiyo waliofika ili kumshuhudia Kiongozi huyo wa serikali akifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yake.

Chenge alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa 6 mchana akiwa kwenye gari ya polisi na baada ya kuachiwa kwa dhamana aliondoka na gari binafsi yenye namba T ASP 362.

Jamani hapa tumeliwa hakuna kesi hapo, police wameacha kitu cha muhimu sana (kumpima kama alikuwa amekwanywa na kiwango gani) na naamini mwameacha kwa makusudi kabisa, na hii kesi mpaka inefika hapa wamemlead ili ashinde... hii nchi inatakiwa ikombolewe na wananchi na nguvu za wananchi anasivo tutabaki tunajikanyaga hapa hapa tuu... daraja kati ya wakubwa na wananchi ni kubwa sana kama lilivo daraja wa watumishi wa serikali wanaotakiwa kutoa huduma kwa wanchanchi lilivo kubwa... nchii hiii inatakuwa kukombolewa sasa...na wanachi wenyewe...KEEP YOUR HEAD UP!!!
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
1,225
Hivi ni kweli yeye ndie aliekuwa anaendesha? Ni yeye ndie aliyegonga nani amethibitisha gari lililohusika na ajali lilikuwa linaendeshwa na mh. Chenge? Mbona anaonekana kama mtu aliyegonga paka tu barabarani? Not big deal kwake?
 
Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,175
1,195
Mwanzoni kabisa nilisema kama muendesha mashitaka ana akili, basi hii kesi ndio njia pekee ya kumfunga Chenge. Lakini nilivyoona hizo argument zake naona kabisa kwamba hakuna kesi hapo, Chenge ni mwanasheria na anaujua mfumo wa sheria ya Tanzania nje ndani. Sasa kama utabuild case kishenzi shenzi kama huyo muendesha mashitaka then at the end of the day Chenge will get away from this.

Kwanza tusimlaumu mwendesha mashtaka maaana yeye kama yeye anapelekewa faili tu toka kituoni. Yeye anadeliver what is in the file. Mpelelezi wa kesi akishamaliza kupepeleza anapeleka fail kwa mkuu wake an hapo fail hupelekwa kwa DPP for futher action. DPP ndo waamuzi. Kwa mfumo wa Tanzania ni vigumu sana kwa Polisi wetu kujenga kesi ya kuweza kumfunga mtu. Ndo maana utaona wengi wa wafungwa wamefungwa kwa kosa la mtu mwingine na sio kosa lake hasa ukizingatia hatujui sheria na haki zetu. Na wale wenye uwezo wa kifedha hufungwa kwa kuwa hawataki kutoa chochote, hivyo wengi hufungwa kwa kukomolewa tu.
Chenge ni mtu anajua huu mchezo mchafu na jinsi ya kuwafanya waandike atakavyo yeye. Kama alitoka akaenda nyumbani ndo akaenda kuripoti Police wewe ungefanywaje? Kama mtu anaendesha gari lisilokuwa na bima na hii hata kwenye charge sheet haikuwepo, unategemea nini? Hii yote ni kudhihirisha kuwa kuna liharufu flani hivi hapo, tena yeye mwenyewe amekiri kuwa anamfahamu binti mmoja Vicky! Anamfahamu vipi? Mimi nafikiri kuwa labda hii ni part one ya kesi inayomkabili Chenge! Kuna tume imeundwa na Kova ya kuchunguza hili tukio! Je, tume hii itatoa ushaidi mahakamani kwa kesi ya traffic ama kwa hiyo kesi ambayo wanaichunguza?
Wadanganyika tutaendelea kudanganyika tu tena baada ya kupewa tusenti hutu twa 2point something kama rambirambi.
 
Tuandamane

JF-Expert Member
Feb 2, 2008
1,221
1,225
Chenge= Vicky!!!!!???? There is a hidden agenda in them!!!! Uchunguzi wa kina ukifanyika tutapata mengi kuhusiana na ajali hii na wahusika(Chenge, Vick, Beatrice). At that dead hour driving??? From where??? Was it a coincidence kukutana pale kwenye scene i.e pale alipowagongea???

Uchunguzi wa kweli ukifanyika kuanzia Mwanza tracing ya communication ya mobile ya Vick plus that of Chenge then tutapata jambo hapo. Tuanzie hapo then mengine yaendeleee!!!!!!

At the same time, Chenge anathubutu kutabasamu, nilitegemea angekuwa na simanzi. Nashauri apelekwe kupimwa akili!!!!! Ningekuwa mimi Chenge, ningekuwa nimezimia sijaamka.Tena nisingeweza kujieleza kwa sasa, ningehitaji muda ili niweke akili sawa. Yaani hajali binadamu kabisa, au kwa kuwa anajua pengine kulikuwa na bifu katia yao?? Alikuwa anawakimbiza hao kina dada/mama!!!!

Low class Chenge, Bull sheet.

Huyu Ndio Chenge wa kweli sasa tunaanza kumuona...hata kama bado akili yake haijakaa sawa kama binadamu huezi kuchekelea kwenye ishu nzito kama hii.. hebu Chenge ajaribu kufikiri kwa sekunde je ni vp kama ndo ingelikuwa amemgonga mmoja wa nduguye aliewaambia waandishi jana mahakamani kuwa wataandika sana tuu na wataishia kuwa maskini
 
Heri

JF-Expert Member
Aug 28, 2007
353
250
Polisi wetu wamechemsha. Baada ya ajali wasinge mruhusu Chenge kwenda nyumbani.
Walitakiwa kumuhoji na kuandikisha statement yake immediately pamoja na kuanaglia kama alikuwa under influence ya alcohol na kwa kiasi gani.
Kwenda nyumbani kunampa uwezo wa kupanga maelezo .
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
1,225
Polisi wetu wamechemsha. Baada ya ajali wasinge mruhusu Chenge kwenda nyumbani.
Walitakiwa kumuhoji na kuandikisha statement yake immediately pamoja na kuanaglia kama alikuwa under influence ya alcohol na kwa kiasi gani.
Kwenda nyumbani kunampa uwezo wa kupanga maelezo .

Heri Chenge hakuruhusiwa Fataki huyu alijiruhusu mwenyewe akakimbia kabla polisi hawajafika eneo la tukio.
 
mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,679
1,250
Nasikia Marehemu mmojawapo alikuwa anafahamiana naye na alikuwa akimtunza Mwanza Hotel.Sasa walikuwa wanatoka mahali wakatofautiana na kuhujumiana au vipi?Halafu huyu Mzee wa vijisenti alikuwa anatoka wapi saa 10 usiku?Uchunguzi utatupa jibu kama vijisenti havitaingilia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom