Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

Mbishi ni wewe, Mkuu Mwiba! Tangu lini usajili unakuwa na period? Unasajili gari tarehe fulani lakini si kuanzia tarehe fulani hadi tarehe fulani! Hata mimi nisie na gari naweza kutambua hilo. Na hivi tangu lini Commissioner wa Bima anasajili magari?

Ubishi usio na maana ndio unakuangusha katika mada zako zote.

Amandla...........


Wakuu mtatoana macho bure ile ya juu ni rd licence. Well kutokana na hiyo kuwa valid mpaka siku ajali inatokea very likely hata insurance ilikuwepo ambayo ni valid lakini haikubandikwa. Ntamshangaa sana muheshimiwa AC kama alikuwa anakumbuka ku-update rd licence lakini bima hakumbuki. Maaana bima ndiyo the most important.

Angalizo jingine kuhusu hiyo receipt hapo juu ni kwamba maandishi yake ni ya kuchapisha wakati ya biima siku zote huwandikwa kwa peni maaluum.
 
Wakuu,

Hivi hili suala la usalama barabarani, hakuna mtu ambaye anaijua sheria vizuri akatuelemisha ipasavyo? Nimesoma hoja mbalimbali hapa naona nyingi zinapingana.

Je ni lazima sticker iwe imebandikwa mbele ya gari? Kama haijabandikwa nini adhabu yake.
Kwa UK ni road licence tu ambayo inatakiwa ibandikwe mbele ya gari lakini na yenyewe hata ukisahau kubandika sio kosa bora uwe nayo wakati huo unasimamishwa au uweze kuipeleka polisi kwa muda uliopewa. Je kwa Tanzania sheria ikoje?

Je ni lazima bima pia ubandike mbele ya gari? Suppose umeisahau ndani ya gari au nyumbani, hilo ni kosa?

Kwa wengine ni muhimu kupata hili somo maana mara nyingi tukiwa nyumbani, magari ya kuazimwa na marafiki, unaweza kufikiri lina kila kitu kumbe kuna vitu vinakosekana. Ni vizuri tukielemishana kwa faida ya wote.

Hizo load license zingine ni kama zinauzwa barabarani bila hata kuangalia gari kama ni zima, je sheria inasemaje?
 
hizo picha zinasikitisha!
Katika picha hizo unazosema zasikitisha, hata zile mbili ambapo Chenge aka Vijisenti anaonekana anapunga mkono anatabasamu kama yuko kwenye utambulisho wa Ubunge au sendoff??? Hapa Chenge naona wala hasikitiki kabisa!!!! Haya tusubiri kuona kama JAMHURI itaonyesha masikitiko yake kwa kumpa Chenge aka Vijisenti adhabu kali inayofaa.
 
Hii ajali ya Chenge imejaa utata kibao, nakubalina na wengi kwamba ajali ni ajali yeyote anaweza kuipata, ila hii inatume sijui ngapi zimeundiwa tume labda hii ya treni.

ila wasiwasi wangu hii ajali inamengi.
ichunguzwe kwamba chenge alilewa wapi na kiasi gani.
Je ni kweli chenge anafahamiana na msichana mmojawapo na Chenge na hao wasichana kama walikutana dar.

Dereva wa bajaji alikufa au aliuwawa.
Na kama hakufa alikimbiaje na kwa ukubwa wa ajali.
Ni nani aliwaita polisi au polisi walijuaje.
je chenge alifuatwa na nani kumpeleka nyumbani ni baada ya polisi kuja au kabla
Na je ni mazoea ya chenge kuendesha gari au ni siku ile tu
Je ni kweli chenge alikuwa pekee kwenye gari lake.
Na je ni kweli bajaji ilikuwa na dereva au ni fiksi??
Je wasichana wale walikufa kwenye ajali au walikwishakufa kabla ya ajali???
Kama dereva hajafa au hajauwawa ni wazi hapakuwepo dereva wa bajaji.

Kabla ya ajali Chenge alikuwa wapi na nani na aliondoka saa ngapi eneo alilokuwepo kabla ya ajali na aliondoka na nani au alikuwa nani kwa usiku ule.

sijui kama polisi watafutilia haya yote au ndio ile ya marehemu alikuwa na hatia .

wanaJF leteni data
 
Mmh jamani hii habari ina utata.kama kweli Chenge alikuwa akifahamiana na mmoja wa marehemu ni wazi kwamba walikuwa wote kwenye maraha then wakatofautia kitu.Wadada wakaamua kukodi bajaji kuondoka na chenge labda hakufurahishwa akaamua kuwafukuzia.Ni mtazamo wangu tu wana jf
 
Naomba kuuliza katika hao waliokufa hakukuwa na albino? Maana sasa hatuaminiani hati, labda mzee aliambiwa hili lazima afanye mwenyewe
 
1537.jpg


Hebu tuonyeshe Model,make na vehicle number kwenye hiyo karatasi ya kati ,mbona mnakuwa wabishi hiyo ni risiti ya kuisajili gari na sio Bima ,ile ya juu ambayo inamalizika 22/o4/09 ndio bima ya gari ,karatasi zote tatu zipo kwenye gari yangu ila hiyo ya kati hata ya kwangu ni ya zamani sana,sikumbuki mara ya mwisho nilienda kuisajili lini maana imebadilika rangi kwa joto la bongo.

Ninaanza kuwa na mashaka na macho yako. Kweli mwiba hauchagui mguu wa kuchoma.
Nilikushauri utoke hapo nje soma gari yoyote hapo utakuta tunayokwambia. This is not bla bla brother! Kama unamiliki gari na huna Road License na Insurance basi wewe tunataka kusikia kesho uko mahabusu kwa kosa la kuiibia Jamhuri ya muungano ya Tanzania. Inawezekana hujui hata plate number zinanunuliwa na zinauzwa na special agent tu, sio kama zamani unajichorea na marker pen unaishia!
Jaribu kuwa mwelewa na usikurupuke tu.
 
Last edited:
Habari za kufahamiana na mmoja wa marehemu ambaye alikwisha fanya kazi katika Casino lililopo Mwanza Hotel zinafahamika vema Mwanza. Na mzee wa vijisenti anadesturi ya kuvinjari japo kwa nadra eneo hilo awapo Mwanza. Hii inazidisha mashaka ya tukio zima.
 
Mmh jamani hii habari ina utata.kama kweli Chenge alikuwa akifahamiana na mmoja wa marehemu ni wazi kwamba walikuwa wote kwenye maraha then wakatofautia kitu.Wadada wakaamua kukodi bajaji kuondoka na chenge labda hakufurahishwa akaamua kuwafukuzia.Ni mtazamo wangu tu wana jf

.....baada ya kuwafukuzia, katika pyurukushani za kuwakamata akagonga bajaj....dreva wa bajaji ikawaje? (kakimbia, kapewa chake mapema akimbie? bajaji ilitegeshewa haikuwa na abiria na hao wasichana wameuawa kwingine halafu wakabwagwa hapo ku set ajali?) .....inanichanganya, polisi tumieni profession yenu na ikiwezekana mumkodiishe Prof Maji Marefu au Manyaunyau awasaidie kufuatilia kila lead..... kumbuka huyu mtu ana utalamu wa ziada (kumbuka alivyomwaga vitu bungeni halafu polisi ikashindwa kuviona)....
 
Sasa naanza kuona sababu ya kuundwa kwa tume,pale penye ajali hapakuonekana damu hata tone zaidi ya mgando wa nyamanyama kwenye ngao ya Toyota,na hata kipaa cha Bajaji hakikuonekana,kwa jinsi ya nyamanyama zille zilivhogandia ni lazima michirizi ya damu ingeonekana imetapakaa na kurukia sehemu kibao za magari na hata barabarani ,Chenge amegonga wafu.
 
Sasa naanza kuona sababu ya kuundwa kwa tume,pale penye ajali hapakuonekana damu hata tone zaidi ya mgando wa nyamanyama kwenye ngao ya Toyota,na hata kipaa cha Bajaji hakikuonekana,kwa jinsi ya nyamanyama zille zilivhogandia ni lazima michirizi ya damu ingeonekana imetapakaa na kurukia sehemu kibao za magari na hata barabarani ,Chenge amegonga wafu.

JF kiboko, wanachama tunavyo analyse hali iliyokutwa kwenye tukio na polisi wangekuwa wanafanya hivi mbona vibaka na mafisadi wote wangekuwa wamekamatwa. Ni imani yangu kuwa wote tunaochangia hakuna mmoja wetu aliyekuwepo pale Oysterbay saa 9 hadi 10 ajali inaposema kutokea, ni mawazo tu, sina hakika, kama yupo aliyekuwepo atupe basi live tuache mambo ya kufikirika!! ....
 
JF kiboko, wanachama tunavyo analyse hali iliyokutwa kwenye tukio na polisi wangekuwa wanafanya hivi mbona vibaka na mafisadi wote wangekuwa wamekamatwa. Ni imani yangu kuwa wote tunaochangia hakuna mmoja wetu aliyekuwepo pale Oysterbay saa 9 hadi 10 ajali inaposema kutokea, ni mawazo tu, sina hakika, kama yupo aliyekuwepo atupe basi live tuache mambo ya kufikirika!! ....
Siku hizi si lazima uwepo kwenye tukio kuna operesheni za upasuaji zinafanywa mkuu wa upasuaji yupo nchi nyingine kabisa ,hata future hospital utakuwa huna haja ya kwenda hospital ,mtatumia system kama yahoo au Hotmail charting na cam ipo pembeni unaeleza matatizo na kukakua sehemu kama una uvimbe,basi unaambiwa kanunuwe dawa zinazofaa kwa marazi yako ,credit card itakuwa ndio zinatumika kwa kulipia kwa hospitali za aina hiyo.
Halafu picha zinazungumza sauzend words si hasha kama wale makachero wa tume wanapita hapa JF wakakumbukia baazi ya mambo muhimu ambayo waliyasahau au yataonekana kuwasaidia kwenye uchunguzi.
Hatujapatiwa ile picha ya ukuta uliosemwa ulikuwa na matundu ya risasi wakati Zombe alipodai palitokea marushiano ya risasi na aliowatuhumu majambazi ndio maana hadi leo kesi inapigwa danadana lakini kwa hii virutubisho kibao vya kesi vimewekwa hapa bado hukumu tu,nafikiri atafungwa maisha.
 
MWIBA: hili la kugonga wafu pia nilikuwa naliwaza -- hasa baada ya kusoma Mwananchi ya leo (Jpili). Inawezekana huyo marehemu Vicky ambaye gazeti linasema huenda alikuwa "samsingi" yake na Vijisenti kusisitiza ahudimiwe na na yeye ktk hoteli moja huko Mza -- alikuwa na nyaraka muhimu ambazo alimuibia -- si lazima niseme katika mazingira yapi -- na akawa anakana kuziiba na/au kugoma kuzirudisha.
 
Last edited:
Yote weka kando tunahitaji kujua dereva wa Bajaji yupo wapi ? Ukichukulia Bajaji madereva wake wanakuwa maarufu na viwete.
 
Ajali Dar: Chenge adaiwa kujuana na mmoja wa marehemu

Frederick Katulanda,Mwanza
SAKATA la ajali ya gari la Andrew Chenge ambalo limesababisha vifo vya wanawake wawili, limeingia katika sura mpya baada ya ndugu wa wasichana hao kudai kuwa Chenge alikuwa akimfahamu mmoja wa marehemu.

Chenge ambaye alikuwa Waziri na Mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, aliingia matatani baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga "bajaji" usiku wa kuamkia juzi na kuua wanawake wawili ambao ni Beatrice Costantine ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanza na mmiliki wa saluni ya kike na Vicky George Makanya.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Mwanza baadhi ya ndugu waliohojiwa na Mwananchi Jumapili akiwamo mama mzazi wa Vicky, walisema wanafahamu Chenge kuwa alikuwa akimjua ndugu yao Vicky.

Akizungumza na Mama wa marehemu Vicky, Nazifa Kambi nyumbani kwao Iloganzala ambako kuna matanga alisema amesikitishwa na taarifa za upotoshaji zilizoeleza kuwa mwanae na rafiki yake walikuwa wakienda Zanzibar kwa ajili ya kufunga ndoa jambo ambalo alilipinga na kueleza kuwa alikuwa akija Mwanza baada ya kutoka Zanzibar ambako walikwenda kununua vifaa vya saluni ya mwenzake.

"Ajali hii inanipa mashaka makubwa kutokana na kupokea taarifa za kupotosha za kufunga ndoa," alisema.
Alisema pia amepata taarifa kutoka kwa wafanyakazi wenzake kuwa Chenge walikuwa wakifahamiana na Vicky na kwamba kila mara alipokuwa akifika Mwanza Hotel alikuwa akimtaka kumhudumia vinywaji yeye.

Nazifa alisema marehemu Vicky ambaye alikuwa mfanyakazi wa Mwanza Hotel katika kitengo cha King Casino ambayo kwa sasa inajulikana kama The Stone, hata yeye mwenyewe aliwahi kumsikia mwanaye kuhusu mbunge huyo kumtaka atoke nyumbani kwenda kumhudumia siku ambayo hakuwa kazini.

Ameiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo ili kupata nini kilichosababisha ajali hiyo.
Kwa upande wa msemaji wa familia ya Beatrice, kaka wa marehemu, Andrew Costantine akiwa Kiseke kwenye matanga alisema wanachofahamu wao ni kuwa dada yake amepatwa ajali akiwa njiani kurejea hotelini walikofikia ya JVL Hotel iliyopo Mwananyamala wakati wakitoka Oysterbay kwa ajili ya kuchukua mizigo yao tayari kwa kuondoka Dar es Salaam kwenda Mwanza.
Andrew alieleza kuwa tayari marehemu na rafiki yake walikuwa wamekwisha kutoka Zanzibar ambako walikwenda kununua bidhaa na vifaa vya saluni ya kike ambavyo vimekutwa hotelini walikokuwa wamefikia.
Alisema marehemu hakuwa amekwenda kufunga ndoa Zanzibar kwa vile alikuwa na mume wake ambaye ni mzungu raia wa Marekani na kwamba mpaka anafikwa na mauti mme wake alikuwa nje ya nchi.
Alisema habari zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa walikuwa wakienda kufunga ndoa siyo za kweli.
"Wakati wakiondoka alimuaga rafiki yake Khadija Hassani ambaye ndiye alimuachia nyumba yake na wakati akiwa Zanzibar alimtumia fedha kwa ajili ya kuwalipia ada ya shule watoto, sasa mambo mengine hakuna anayejua tunaomba uvumulivu msiba uishe," alieleza.

Alisema mpaka sasa Chenge ameahidi kusaidia familia kusafirisha miili ya marehemu hao, lakini bado hawajapokea lolote kutoka kwake na wanaendelea kumsubiria wakati polisi wakikamilisha taratibu za uchunguzi huku na wao wakijipanga kusafirisha miili ya ndugu zao.
Msiba hii imeacha simanzi Jijini Mwanza na kuwa gumzo kubwa huku ukizua minog’ono ya hapa na pale na baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wengine wakishangazwa na tukio hilo na jinsi jeshi la polisi lilivyounda tume kushughulikia ajali hiyo tofauti na ajali nyingine.
Marehemu hao waliondoka Jijini Mwanza Machi 24, mwaka huu kwa safari ya kibiashara Dar es salaam na baadaye Zanzibar na walikuwa wakitarajiwa kureja Ijumaa Machi 27, Beatrice ameacha watoto wanne ambao wanasoma shule tofauti za bweni na mwenzake Vicky ameacha mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Chege kwa simu jana hazikuzaa matunda jana.

My Take; I wonder if it was a coincidence kuwa Mh Chenge amejikuta akimgonga mtu aliyekuwa akimtafuta kila alipokuwa akienda Mwanza,kama alikuwa akimwita akampe huduma hata wakati akiwa off ama likizo basi nitashangazwa kama hawakuwa na mawasiliano wakati mwanadada huyo akiwa hapo Dar.
Hii ni dalili kwamba kuna mambo mengi yakawa yamefichwa,unaweza kuwa ni set up kama huyo mwanadada alizidi kumwandama Mheshmiwa,mheshimiwa akaona ni kama blackmailing.
Toka mwanzo picha za tukio la ajali na maelezo vinapingana sana,ukichanganya na ukweli kuwa dereva amepotea na merehemu hawawezi kutoa ushahidi,labda hayo mambo ya insurance na mengineyo ni ya ku tutoa nje ya pointi.
 
...Kwa maana hii skendeli hili lishageuka kuwa mauaji ya kukusudia?! kaaazi kweli!
 
Yote weka kando tunahitaji kujua dereva wa Bajaji yupo wapi ? Ukichukulia Bajaji madereva wake wanakuwa maarufu na viwete.

Kama huyo dereva alitimua baada ya ajali na mpaka sasa hajulikani alipo,mmiliki wa hiyo bajaj si anaweza julikana mana hiyo bajaj imesajiliwa. Halafu huyo mmiliki amtaje dereva aliyempatia japo muda mwingine bajaj ni kama taxi, madereva wanapeana waendeshe abiria japo atajulikana tu sema kupatikana kwake kwa kujisalimisha ndiyo utata.
Ila sasahivi habari ya chenge kujuana na mmoja wa marehemu itakuwa imevuruga taswira ya ajali tuliyopata kabla,sijui yeye mwenyewe atasemaje juu ya hilo!
 
Baadhi ya magazeti ya kila siku ya leo hapa bongo (siyo ya udaku) yameandika kuwa Chenge kakiri kuwa alikuwa anamfahamu Vicky. Radio Clouds nayo imetangaza kuwa Chenge kakiri kuwa alikuwa anamfahamu Vicky. Habari ndiyo hiyo!!!! Kumgonga na kumuua mtu unayemfahamu kiasi cha kuwa hata akiwa off unaomba aje akuhudumie hotelini ni kitu kizito chahitaji tafakari ya kina!!!!
 
Mh mbona yeshakuwa makubwa? Sasa tuelewe vije ila nadhani ni ajali tu kama ajali nyingine hakujua kama anamgonga mtu anayemfahamu imetokea tu.

Mh. Chenge una makosa please msimsakizie dereva wa bajaj
 
Back
Top Bottom