Chenge apewe nafasi ya Uspika, Ndugai apumzike ili kuiepusha CCM na aibu

Kasegela

Senior Member
Mar 24, 2019
127
261
Katika ulimwengu wa sasa,ulimwengu ambao watanzania wengi wana uelewa na kuweza kuhoji kila sentensi inayotolewa na Kiongozi,ni wazi kuna haja yakurekebisha Bunge letu.

Baada ya utumushi wa Spika Ndugai,nimelinganisha na Spika aliepita vs mahitaji ya wananchi kwa sasa.

Nimekubali kuwa Mama Makinda alilimudu Bunge.

Sijawahi kuona Spika dhaifu katika uhai wa Bunge letu kama Ndugai.

Sababu kubwa za udhaifu wa Ngugai ni mbili.

1.Hakuwa Chaguo la Rais Magufuli,Ndugai alijataliwa na chaguo lao alikuwa Dr.Tulia .

Ndugai akapiganiwa na wafia chama,waliposhindwa nguvu hadi wapinzani wakaingilia kati,nakumbuka Zitto Kabwe alihaha usiku kwa usiku kuhakikusha Ndugai anaputishwa na CCM kuwa Mgombea wa Uspika.

Ni wazi watu waliangalia madhara wanayoweza kupata wananchi na taasisibya Bunge ikiwa Tulia angekuwa Spika wa Bunge.

Tangu hapo,ndugai alijiona ni Marginalized .

Akaanza kusaka kukubalika mbele ya Rais Magufuli kiasi cha kusahau kuwa yeye ni kiongizi wa muhimili unaotakiwa kuisimamia serikali ya Rais Magufuli.

Hapo ndipo mambo yalipoharibikia,Ndugai akachagua kuwa kiongozi alijisalimisha kwa serikali na kugeuka kuwa muhimili wa kudhibiti bunge.

Yaani Ngugai yupo pale kupambana na wabunge waluochagua badala ya kupambana na mawaziri wanaotoa majibu yasiyotekelezeka.

Huyo ndio Ndugai alieushiwa pumzi.

2.Ugonjwa,Ndugai baada ya kuapishwa kuwa Spika,aliugua na kulazimika kwenda matibabu India.

Akiwa India Naibu Spika ndiye aliliongoza Bunge,alifanya kila jambo kuhskikisha Ndugai akirudi asiwe na nguvu wala ushawishi wowote kwa Bunge na serikali,ukweli Dr.Tulia alimnyoosha.

Nakumbuka Tulia alirejesha fedha za Bunge serikalini huku wabunge wakiwa hawana hata fedha za Stationary.

Ndugai aliporejea,alilazimishwa kufuata mifumo iliyokwisha simikwa na Tulia.

Kwa nguvu aliyomkuta nayo Tulia ,Spika alilazimika kumnyenyekea Tulia ili Uspika wake usihojiwe kwenye chama.

Kwa sababu hizo mbili ndio chanzo cha Udhaifu wa Ndugai.

Lakini Ndugai mwenyewe kwa binafsi yake sio dhaifu,ni kiongozi shujaa na makini.

Kakini kazidiwa nguvu,na namna pekee ya kulinda cheo chake ni kuungana na watu ambao yeye anaamini hawezi kushindana nao.

Msimshambulie jamani,kufanya hivyo kunazidi kumuumiza,kunamuharibu kisaikolojia.

Jinsi ya Kumsaidia Nguga kwa sasa ni kumshauri ashuke kutoka kwenye nafasi ambayo yeye sio chaguo.

Abaki kuwa mbunge wa kawada,bila shaka ataendelea kutafuna posho na marupurupu ya Spika,tutamwita Spika Mstaafu.

Nafasi yake apewe Mtemi Chenge,Huyu ni msomi wa sheria,jasiri na mtu mwenye roho ngumu.

Akipewa kiti cha Spika,hata chama cha mapinduzi kitaimarika,serikali itawajibishwa bungeni kwa nguvu mpya,ari mpya na kasi mpya.

Chenge kwa sasa hana chakupoteza,na zaidi ya yote ni mwanaseria aliebobea akiwa kasoma chuo bora Dunuani.

Kama na wewe unamkubali Chenge kuchukua nafasi ya ndugai weka maoni yako.

Muhimu maoni yako yakenge kumsaidia Ndugai kuliko kumbedha,kumbagaza na kumdhalilisha.
Nawasilusha.

CC.Jackton Mnyerere,Pasco,Yeriko,Udertaker,Jingalao,
 
Wote tunaujua mgogoro wa CAG na Spika kadhalika namna dada Tulia alivyokwamisha kujadiliwa hoja binafsi ihusuyo maslahi ya watumishi wa umma.

Mambo hayo mawili yanaweza kuwapa CCM wakati mgumu kwenye kampeni za 2020 na hasa ukizingatia ingizo jipya la ACT wazalendo.

Ndipo sasa naitazama hii hali kama fursa muhimu kwa mzee Chenge ambaye " ameutamani" uspika kwa muda mrefu.

Niwatakie Alhamisi ya Amri yenye baraka tele.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mara Elfu achukue Andew Chenge.
Maana Ana Sera ya Kula na Kugawia wengine pia.

Kuliko hawa wa sasa Wanaoshibisha matumbo yao tu na kuwaacha wengine wafe na NJAA.

kitendo Cha Tulia kukataa kuwapandishia Wafanyakazi mishahala kwa zaidi ya miaka minne ili hali yeye anajiongezea mshahala na marupurupu mengine KILA KUKICHA ni mfano hai wa ROHO MBAYA ya watawala wa awamu hii ya TANO.

Mara Elfu Spika awe Mzee wetu Chenge.
Anashiba nasisi tunashiba.
 
Wote tunaujua mgogoro wa CAG na Spika kadhalika namna dada Tulia alivyokwamisha kujadiliwa hoja binafsi ihusuyo maslahi ya watumishi wa umma.

Mambo hayo mawili yanaweza kuwapa CCM wakati mgumu kwenye kampeni za 2020 na hasa ukizingatia ingizo jipya la ACT wazalendo.

Ndipo sasa naitazama hii hali kama fursa muhimu kwa mzee Chenge ambaye " ameutamani" uspika kwa muda mrefu.

Niwatakie Alhamisi ya Amri yenye baraka tele.

Maendeleo hayana vyama!
Kwa taarifa yako hapo mjengoni ktk watu ambao mh hataki hata kumsikia ni huyo chenge tena anatafutiwa target muda sii mrefu mtajionea wenyewe gaani mtu kila kashfa ya nchi hii yumo na inajulikana kabisa alafu wakampe uongozi?
 
chenge hawezi lilia kazi ndogo kama ya uspika katika umri huo,kwanza hata uenyekiti wa bunge ni kama anasaidia tu,,yule hana presha na madaraka
 
Sawa mkuu .......hata Lowassa tulisubiri hatimaye tukaona bila mabishano!
Kwani lowasa si vitisho vya kuzuiliwa acout zake hela ilitoko wee unafikiri alirudi kwa kuunga mkono kama mlivyodhani?
Hata huyo chenge wenu yatamkuta tuu ni suala la muda tuu
 
Back
Top Bottom