Chenge akaidi agizo la polisi la kusitisha kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,904
2,000
Agizo la Jeshi la Polisi nchini la kusitisha kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa limeonekana kutoathiri ratiba za Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge ambaye ameendelea na mikutano ya hadhara jimboni kwake.

Taarifa kutoka jimboni humo zimeeleza kuwa Chenge amekuwa akifanya mikutano ya hadhara katika vijiji mbalimbali na Alhamisi iliyopita alianza na eneo la Buchani, mkutano uliomalizika salama bila kuwepo kizuizi chochote. Katika mikutano hiyo, Mtemi Chenge ameendelea kuwasisitiza wananchi wake kupuuza kauli za kisiasa zinazotolewa na wapinzani wake bali waangalie namna anavyotekeleza ahadi alizozitoa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.

Mikutano hiyo ya Chenge hutanguliwa na matangazo yanayofanywa kwa kutumia magari yenye vipaza sauti katika eneo husika.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa yeye hahusiki kutoa vibali vya mikutano na kwamba mhusika ni Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD).

Hata hivyo, OCD hakupatikana kwa wakati.Hali hiyo imedaiwa kuzua manung’uniko kwa vyama vya upinzani mkoani humo ambavyo vimeshindwa kufanya mikutano ya hadhara kutokana na kuwepo kwa zuio la Mikutano hiyo nchi nzima.Mwezi uliopita, Kamishna wa Jeshi la Polisi,Operesheni ya Mafunzo, Nsato Msanzya alitangaza kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano ya kisiasa kwa sababu za kiusalama.

“Polisi kupitia vyanzo vyake mbalimbali, imebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi,” alisema Kamishna Nsato.Kufuatia agizo hilo, Jeshi la Polisi lilizuia kufanyika kwa mikutano iliyokuwa imepangwa na CHADEMA na ACT- Wazalendo kwa nyakati tofauti.

Nionavyo
Ni bora Magufuli na polisi wake akawa clear kabisa kwamba mikutano ya upinzani hairuhusiwi na ni marufuku kuhoji utendaji wake kuliko kuzunguka zunguka mbuyu namna hii

Awatangazie upinzani kabisa kuwa mikutano yenu itaruhusiwa endapo mtaniunga mkono bila kunihoji na hata mkifukuzwa na vyama vyenu atawapangia kazi nyingine kama alivyogusia juzi
hi
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,027
2,000
Jana nilimshuhudia Dr Mollel Mbunge wa Siha kupitia Chadema akifanya mkutano na wananchi wa Siha.....na yeye amekaidi???
 
eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
14,072
2,000
Wacheni porojo huyu yuko jimboni kwake akihimiza maendeleo na kupeleka mrejesho kwa wapiga kura wake. Sasa mtu atoke hai na rombo akapige siasa kahama kweli? Hebu kuweni na soni.
 
ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
11,101
2,000
Wacheni porojo huyu yuko jimboni kwake akihimiza maendeleo na kupeleka mrejesho kwa wapiga kura wake. Sasa mtu atoke hai na rombo akapige siasa kahama kweli? Hebu kuweni na soni.
Unamzungumzia Mwenyekiti wa CDM au mwingine?
 
HAVARA

Member
Jul 1, 2016
25
45
Chenge ni mti mkavu umewashinda ccm,na serkali.Je si ndiye aliyekataa kuhojiwa na tume ya maadili? Wabunge wa ccm wakamzawadia uenyekiti wa bunge.Eti na yeye yumo kwenye kamati ya maadili ya bunge.Aibu aibu aibu!!!!!!!
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
57,215
2,000
Katazo hilo ni kwa ájili ya vyama vya upinzani tu.....bado hamuelewi
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,658
2,000
Agizo la Jeshi la Polisi nchini la kusitisha kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa limeonekana kutoathiri ratiba za Mbunge wa Bariadi, John Chenge ambaye ameendelea na mikutano ya hadhara jimboni kwake.

Taarifa kutoka jimboni humo zimeeleza kuwa Chenge amekuwa akifanya mikutano ya hadhara katika vijiji mbalimbali na Alhamisi iliyopita alianza na eneo la Buchani, mkutano uliomalizika salama bila kuwepo kizuizi chochote. Katika mikutano hiyo, Mtemi Chenge ameendelea kuwasisitiza wananchi wake kupuuza kauli za kisiasa zinazotolewa na wapinzani wake bali waangalie namna anavyotekeleza ahadi alizozitoa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.

Mikutano hiyo ya Chenge hutanguliwa na matangazo yanayofanywa kwa kutumia magari yenye vipaza sauti katika eneo husika.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa yeye hahusiki kutoa vibali vya mikutano na kwamba mhusika ni Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD).

Hata hivyo, OCD hakupatikana kwa wakati.Hali hiyo imedaiwa kuzua manung’uniko kwa vyama vya upinzani mkoani humo ambavyo vimeshindwa kufanya mikutano ya hadhara kutokana na kuwepo kwa zuio la Mikutano hiyo nchi nzima.Mwezi uliopita, Kamishna wa Jeshi la Polisi,Operesheni ya Mafunzo, Nsato Msanzya alitangaza kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano ya kisiasa kwa sababu za kiusalama.

“Polisi kupitia vyanzo vyake mbalimbali, imebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi,” alisema Kamishna Nsato.Kufuatia agizo hilo, Jeshi la Polisi lilizuia kufanyika kwa mikutano iliyokuwa imepangwa na Chadema naACT-Wazalendo kwa nyakati tofauti.

Nionavyo
Ni bora Magufuli na polisi wake akawa clear kabisa kwamba mikutano ya upinzani hairuhusiwi na ni marufuku kuhoji utendaji wake kuliko kuzunguka zunguka mbuyu namna hii

Awatangazie upinzani kabisa kuwa mikutano yenu itaruhusiwa endapo mtaniunga mkono bila kunihoji na hata mkifukuzwa na vyama vyenu atawapangia kazi nyingine kama alivyogusia juzi
Kwani wewe hujui kuwa Mkulu amepiga STOP mikutano ya hadhara na hata mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa vya upinzani pekee?

Wakati huo huo akatoa 'ruksa' kwa chama chake cha CCM kuendelea na mikutano ya ndani, kongamano na hata mikutano ya hadhara bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi....
 
KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,525
2,000
huyo john chenge wana undugu wowote na andrew chenge?

Ni Andrew Chenge, naona kuna makosa ya kiuandishi
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,459
2,000
Jana nilimshuhudia Dr Mollel Mbunge wa Siha kupitia Chadema akifanya mkutano na wananchi wa Siha.....na yeye amekaidi???
Naam, na huo ushahidi wako unadhihirisha ukigeugeu wa Polisi kwa kiwango kikubwa zaidi. kwa nini wasiwe consistent? m singi wa kuzuia mikutano ni nini hasa? kama unahurusu hapa na kuzuia pale? au wanaruhusu ile tu ambayo haitakuwa na "kick" ?
 
chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,904
2,000
Kwani wewe hujui kuwa Mkulu amepiga STOP mikutano ya hadhara na hata mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa vya upinzani pekee?

Wakati huo huo akatoa 'ruksa' kwa chama chake cha CCM kuendelea na mikutano ya ndani, kongamano na hata mikutano ya hadhara bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi....
nataka aseme waziwazi kuondoa utata
 
Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,155
2,000
Agizo la Jeshi la Polisi nchini la kusitisha kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa limeonekana kutoathiri ratiba za Mbunge wa Bariadi, John Chenge ambaye ameendelea na mikutano ya hadhara jimboni kwake.

Taarifa kutoka jimboni humo zimeeleza kuwa Chenge amekuwa akifanya mikutano ya hadhara katika vijiji mbalimbali na Alhamisi iliyopita alianza na eneo la Buchani, mkutano uliomalizika salama bila kuwepo kizuizi chochote. Katika mikutano hiyo, Mtemi Chenge ameendelea kuwasisitiza wananchi wake kupuuza kauli za kisiasa zinazotolewa na wapinzani wake bali waangalie namna anavyotekeleza ahadi alizozitoa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.

Mikutano hiyo ya Chenge hutanguliwa na matangazo yanayofanywa kwa kutumia magari yenye vipaza sauti katika eneo husika.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa yeye hahusiki kutoa vibali vya mikutano na kwamba mhusika ni Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD).

Hata hivyo, OCD hakupatikana kwa wakati.Hali hiyo imedaiwa kuzua manung’uniko kwa vyama vya upinzani mkoani humo ambavyo vimeshindwa kufanya mikutano ya hadhara kutokana na kuwepo kwa zuio la Mikutano hiyo nchi nzima.Mwezi uliopita, Kamishna wa Jeshi la Polisi,Operesheni ya Mafunzo, Nsato Msanzya alitangaza kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano ya kisiasa kwa sababu za kiusalama.

“Polisi kupitia vyanzo vyake mbalimbali, imebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi,” alisema Kamishna Nsato.Kufuatia agizo hilo, Jeshi la Polisi lilizuia kufanyika kwa mikutano iliyokuwa imepangwa na Chadema naACT-Wazalendo kwa nyakati tofauti.

Nionavyo
Ni bora Magufuli na polisi wake akawa clear kabisa kwamba mikutano ya upinzani hairuhusiwi na ni marufuku kuhoji utendaji wake kuliko kuzunguka zunguka mbuyu namna hii

Awatangazie upinzani kabisa kuwa mikutano yenu itaruhusiwa endapo mtaniunga mkono bila kunihoji na hata mkifukuzwa na vyama vyenu atawapangia kazi nyingine kama alivyogusia juzi
Mikutano ya siasa iliyokatazwa ni ile yenye malengo ya uchochezi dhidi ya maamuzi ya serikali na bunge lake. Hususani ile ya wabunge wa upinzani waliamua kutoka kwenye vikao vya bunge la bajeti kwa lengo la kupeleka hoja zilizokuwa zinajadiliwa bungeni kwa wananchi kuwahamasisha wazuie bajeti hiyo kwa nguvu ya peoples power.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom