Chenge aiponza BoT

Buswelu

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
1,998
351
Chenge aiponza BoT

na Waandishi Wetu

KUGUNDULIKA kwa akaunti ya mabilioni ya fedha inayohusishwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) katika benki moja katika visiwa vya Jersey, Uingereza, hivi karibuni, kunaonekana kuwashtua na kuwaamsha usingizini wabunge.

Hali hiyo ilidhihirika jana wakati wa semina ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ambapo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed aliitaka Benki Kuu (BoT) kutoa ufafanuzi wa sheria inayoruhusu wananchi kuweka fedha katika benki za nje.

Hata hivyo, swali hilo la Hamad Rashid kwa maofisa wa BoT waliokuwa wakiwaeleza wabunge kuhusu shughuli mbalimbali za taasisi hiyo, lilikosa majibu ya papo kwa papo.

Maofisa hao wa BoT waliwaomba wabunge kuwapa muda hadi leo hii ili waje kutoa majibu ya swali hilo, na mengine kadhaa yaliyoulizwa ambayo kimsingi yalihitaji majibu yaliyoandaliwa na yanayojitosheleza.

Hamad Rashid katika swali lake aliloliuliza pasipo kumtaja kwa jina Chenge, aliuliza iwapo sheria zilikuwa zikiruhusu watu binafsi kumiliki akaunti nje ya nchi.

“Nataka kujua, je, sheria inaruhusu mtu kuweka fedha za kigeni nje ya nchi?” alihoji Rashid na kuongeza kwamba hivi sasa imani ya Watanzania kwa BoT imeshuka kutokana na tuhuma za ufisadi zinazoikabili benki hiyo.

Ingawa hakuweka bayana, swali hilo lilionekana dhahiri kutoa mwelekeo unaomhusu Chenge ambaye hivi karibuni akaunti yake hiyo ya nje ya nchi ilikutwa ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja ambazo ni karibu shilingi bilioni 1.2.

Fedha hizo za Chenge ambazo uchunguzi wake unaendelea, ziligunduliwa na makachero wa kitengo cha uchunguzi wa makosa makubwa ya rushwa cha nchini Uingereza (SFO), wanaochunguza mkataba wa mauzo ya rada, yaliyofanywa kwa Serikali ya Tanzania na Kampuni ya BAe Systems ya nchini humo mwaka 2002.

Zaidi ya suala hilo, mbunge huyo alitaka pia kufahamu namna madini yanavyosaidia wachimbaji wadogo, huku akihoji msaada wa BoT kwa wamachinga, aliodai kuwa wanachangia asilimia 30 ya bajeti ya serikali.

Awali, Pantaleo Kessy wa BoT, aliyewasilisha mada ya sera na ubadilishanaji wa fedha za kigeni, alisema ipo sheria inayomzuia mtu kuweka fedha nje ya nchi.

Mbali na mbunge huyo, kamati pia imetaka kufahamishwa ukweli kuhusu kushuka kwa kiwango kikubwa kwa uchumi wa Tanzania na akiba ya fedha za kigeni zilizopo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Naibu Waziri wa Mipango na Fedha, Omari Mzee, alisema idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki bado ni ndogo.

Alisema kati ya Watanzania zaidi ya milioni 35, wanaotumia huduma hizo ni milioni 1.6 tu, sawa na chini ya asilimia tano ya watu wote waliopo nchini.

Kugundulika kwa fedha hizo za Chenge katika akaunti moja ya nje ya nchi, hatimaye kulimlazimisha mwanasiasa huyo ajiuzulu wadhifa aliokuwa akiushikilia wa Waziri wa Miundombinu.
 
Wanahabari wajanja sana!wanataka tu kuuza magazeti!ukisoma hii habari huyo mbunge aliyeuliza swali hakutaja jina!pia mimi naona siyo Chenge peke yake ndo mwenye acount nje
 
Wanahabari wajanja sana!wanataka tu kuuza magazeti!ukisoma hii habari huyo mbunge aliyeuliza swali hakutaja jina!pia mimi naona siyo Chenge peke yake ndo mwenye acount nje

Kichwa cha habari hakiendani na habari.
 
Kwani BoT wanashindwa swali hili rahisi au basi tu hawakutaka kulijibu kwa sababu ni viongozi wengi tu wamejilimbikizia mali?
 
Ni kosa raia kuweka `vijisenti` nje - BoT

2008-05-30 09:11:04
Na Mashaka Mgeta

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema ni kosa la kisheria, kwa raia kuhifadhi fedha za kigeni katika akaunti zilizo nje ya nchi.

Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge, kuhifadhi Dola milioni moja za Kimarekani kwenye benki moja kisiwani Jersey, Uingereza.

Bw. Chenge aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa takriban miaka 10.

Mchumi Mwandamizi wa BoT, Dk. Kessy Pantaleo, aliyasema hayo, wakati akitoa mada kuhusu sera za fedha za kigeni na ukadiriaji viwango vya kubadilisha sarafu, kwa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi.

Manaibu Gavana wa benki hiyo, Bw. Enos Bukuku na Bw. Juma Reli, walihudhuria semina hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya BoT jijini Dar es Salaam jana.

``Hairuhusiwi pale unapokuwa na vijisenti vyako, vikiwa ni fedha za kigeni, kuzihifadhi nje ya nchi... Legally is not allowed,`` alisema akimaanisha kisheria haikubaliki.

Hata hivyo, Dk. Pantaleo, hakueleza kwa undani kuhusu kosa hilo, lakini Nipashe, ilipowasiliana na Naibu Gavana, Bw. Reli, alisema sheria hiyo inahusu fedha zilizotoka ndani ya nchi.

``Sheria inayozuia hifadhi za fedha za kigeni nje ya nchi, inatitwa Foreign Exchange Act, na inahusu fedha za kigeni zilizotoka ndani kwenda kuhifadhiwa nje ya nchi,`` alisema.
Hata hivyo, Dola milioni moja zinazodaiwa kuhifadhiwa na Bw. Chenge huko Uingereza, hazijajulikana kama zilitoka ndani ama nje ya nchi.

Taasisi ya kuchunguza makosa makubwa ya jinai nchini Uingereza (SFO), inatafuta taarifa ili kubaini asili ya `vijisenti` vya Bw. Chenge, kama zilitokana rushwa katika ununuzi wa rada kutoka kampuni ya BAE System ya nchini humo ama la.

Bw. Reli, alisema licha ya kuwepo sheria hiyo, BoT haina utaratibu wa kufuatilia fedha za Watanzania zilizohifadhiwa nje ya nchi.

``Ikibainika kuwepo fedha za kigeni zilizohifadhiwa nje ya nchi zimetoka hapa nchini, ni matatizo kwa mujibu wa sheria hiyo,`` alisema.

Naye Mkurugenzi wa Mfumo wa Taifa wa Malipo (National Payment System) katika BoT, Bw. Dadi Bernard, alisema serikali haijaamua kuingia katika mfumo huo unaotumia teknolojia ya kisasa.

Alisema mfumo huo una faida nyingi, zikiwemo uharaka wa malipo na wigo mpana wa uwazi katika kufuatilia mzunguko wake.

Hata hivyo, alisema kuna uwezekano kuwa, hatua hiyo inatokana na taratibu za kiutendaji serikalini.

Naye Mchumi Mwanadamizi, Dk. Johannes Aikaeli wa BoT, alisema mikopo ya benki hiyo kwa sekta binafsi, imeongezeka kwa kasi, wakati ile ya serikali ikipungua.

Dk. Aikaeli, alisema kiwiano, kwa kulinganisha na jumla ya amana, mikopo katika sekta binafsi ilikua kutoka asilimia 54.6 Juni, mwaka jana, kufikia 61.8 Aprili mwaka huu.

Alisema katika kipindi hicho, mikopo ya serikali ilipungua kutoka asilimia 36.8 kufikia 31.1.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi, Dk. Abdallah Kigoda, alisema kuna haja ya kupata ufafanuzi kuhusu maelezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, kuhusu uwezo wa serikali kupunguza asilimia ya pato lililotegemewa kwa wafadhili.

Bw. Pinda, alikaririwa akisema kutokana na ufanisi katika makusanyo ya mapato yake, utegemezi wa serikali kwa wafadhili utapungua kutoka asilimia 42 ya bajeti mwaka huu, kufikia 30.

``Tunataka kujua ni kwa namna gani pengo hili kubwa linaweza kupungua katika kipindi kifupi cha takribani mwaka mmoja,`` alisema.

SOURCE: Nipashe
 
sasa hao wabunge si wawabane watafute watu waliotoa pesa tanzania wakazipeleka nje?sasa wote macho yao yapo kwa mtu mmoja!kichekesho kweli!
 
Nzoka na Hollo, 'ufisadi' wa habari ni jambo kubwa hivi sasa linalo turudisha nyuma. Fikiria hiyo habari juu imeandikwa na 'waandishi wetu'; sijui wangapi walikuwa hawa wamejikusanya na kuandika ka-article kenye paragraph tatu zilizo nyambulishwa ili kui-stretch habari ambayo ingeweza kabisa kuandikwa kwa paragraph moja tu?!

Bila kuwatetea viongozi wanaosimama kwenye majukwaa ya siasa kuhubiri mikopo ya saccos na uwekezaji nyumbani kuwa ni jambo nambari moja, hali wao wakitenda vinginevyo... kifupi, hii habari ime 'fisadiwa' if you allow me to put it that way.
 
na za Mkapa zilizoko Zurich, zilitoka ndani au zilikuwa huko tokea awali?
 
Hawa maofisa walishindwaje kutoa majibu palepale?au wameenda kujipanga kupindisha sheria?tusubiri majibu yao leo.
 
Kichwa cha habari hakiendani na habari.

Nzoka na Hollo, 'ufisadi' wa habari ni jambo kubwa hivi sasa linalo turudisha nyuma. Fikiria hiyo habari juu imeandikwa na 'waandishi wetu'; sijui wangapi walikuwa hawa wamejikusanya na kuandika ka-article kenye paragraph tatu zilizo nyambulishwa ili kui-stretch habari ambayo ingeweza kabisa kuandikwa kwa paragraph moja tu?!

Bila kuwatetea viongozi wanaosimama kwenye majukwaa ya siasa kuhubiri mikopo ya saccos na uwekezaji nyumbani kuwa ni jambo nambari moja, hali wao wakitenda vinginevyo... kifupi, hii habari ime 'fisadiwa' if you allow me to put it that way.
yaani mengine yaliyoandikwa humo ni marudio tu!kila mtu anafahamu chenge alijiuzulu kwa nini?ila ndo kama unavyoona wanarudia tena kwenye magazeti!
nakwambia kila kitu hapa kwetu kinapita tu!ilianza EPA,richmond jamaa hadi leo sijui wanalipwa!sasa leo tunang'ang'ania chenge kitu bado kipo kwenye uchunguzi!Tanzania ni tamu sana kuitawala!
 
na za Mkapa zilizoko Zurich, zilitoka ndani au zilikuwa huko tokea awali?

Mkapa alishasema hana hela Uswisi wala nje ya Tanzania. Alisema haya kwenye mkutano wa G8 kule Scotland mwaka juzi sijui. Tena alisema mbele ya ulimwengu kwenye live TV UK, ITV. Alisema kwa confidence ya hali ya juu huku mashavu yametuna akimeremeta. So usimsingizie unless una concrete evidence lol.
 
Nzoka na Hollo, 'ufisadi' wa habari ni jambo kubwa hivi sasa linalo turudisha nyuma. Fikiria hiyo habari juu imeandikwa na 'waandishi wetu'; sijui wangapi walikuwa hawa wamejikusanya na kuandika ka-article kenye paragraph tatu zilizo nyambulishwa ili kui-stretch habari ambayo ingeweza kabisa kuandikwa kwa paragraph moja tu?!

Bila kuwatetea viongozi wanaosimama kwenye majukwaa ya siasa kuhubiri mikopo ya saccos na uwekezaji nyumbani kuwa ni jambo nambari moja, hali wao wakitenda vinginevyo... kifupi, hii habari ime 'fisadiwa' if you allow me to put it that way.
Hapa ndo wananiacha hoi.
 
Mkapa alishasema hana hela Uswisi wala nje ya Tanzania. Alisema haya kwenye mkutano wa G8 kule Scotland mwaka juzi sijui. Tena alisema mbele ya ulimwengu kwenye live TV UK, ITV. Alisema kwa confidence ya hali ya juu huku mashavu yametuna akimeremeta. So usimsingizie unless una concrete evidence lol.

Ng'wanone, mambo ya kuongea kwa konfidensi achana nayo bana... wanasiasa wengi tunawajua wanahiyo confidence..... lakini wengi umeshaona jinsi wanavyoishia kula 'matapishi yao wenyewe'...hapa bongo tu umeona, na natumaini unamkumbuka Collin Powell alivyo onyesha hadi ki-toy cha lorry la WMD kuonesha mfano wa mambo huko Iraq ambacho CIA walikuwa wamemtayarishia mbele ya kadamnasi ya UN!

Vivo hivyo uliona vituko vya mtu huyu machachari:
07-minister.jpg

.... na uhakika hatima ya yote hayo uliiona na kuitafakari mwenyewe!

....ila hapo kwenye mashavu kumerameta na kusupport mkuu. mashavu yake yamekwiva utafikiri amekuwa akitafuna sugar-free JoJo kama ishirini hivi kwa mpigo zenye strawberry flavor tangu kuzaliwa!!
 
Ng'wanone, mambo ya kuongea kwa konfidensi achana nayo bana... wanasiasa wengi tunawajua wanahiyo confidence..... lakini wengi umeshaona jinsi wanavyoishia kula 'matapishi yao wenyewe'...hapa bongo tu umeona, na natumaini unamkumbuka Collin Powell alivyo onyesha hadi ki-toy cha lorry la WMD kuonesha mfano wa mambo huko Iraq ambacho CIA walikuwa wamemtayarishia mbele ya kadamnasi ya UN!

Vivo hivyo uliona vituko vya mtu huyu machachari:
07-minister.jpg

.... na uhakika hatima ya yote hayo uliiona na kuitafakari mwenyewe!

....ila hapo kwenye mashavu kumerameta na kusupport mkuu. mashavu yake yamekwiva utafikiri amekuwa akitafuna sugar-free jojo 26 kwa mpigo from birth!!

Mimi nimeripoti kama ilivyokuwa! Evidence yake ilikuwa infronti ofu ze TV.
 
Wanahabari wajanja sana!wanataka tu kuuza magazeti!ukisoma hii habari huyo mbunge aliyeuliza swali hakutaja jina!pia mimi naona siyo Chenge peke yake ndo mwenye acount nje

Kweli kabisa kichwa cha habari kimepotoshwa,Chenge ameiponzaje BOT?

Suala la kulaumu lielekezwe BOT ambao kwa kujua sheria ipo lakini hawakuwahi kuitumia kuzuia viongozi kutunza pesa za kigeni nje ya nchi.

Hizi sheria za Tanzania hujulikana tu wakati wahusika wamebanwa au kukumbwa ,lakini kama hazijaulizwa unapeta bila wasiwasi.
 
....Nzoka, sasa hapo utakuwa umejitoa vipi kutoka kwenye kundi kama hilo hapo juu la "waandishi wetu" ?!

Sioni vimefanana vipi.

Kutokana na article, Chenge ameiponza vipi BoT?

Mimi nimeripoti kutoka maneno ya Mkapa mwenyewe as it was said. Tena ngoja niwaombe ITV huo mkanda. At a small price wanakutumia.

Sasa wewe kama una evidence tofauti na hii, itakuwa poa sana. Maana haya maneno yake, yalisababisha hadi Tanzania kufutiwa deni (ingawa am sure tumejiingiza mkenge sehemu nyingine e.g madini etc). Maneno yake haya ndo yalimfanya apewe imani na viongozi wa nje ulaya, na hadi Sharon Stone akatoa mchango wa $10K kwa neti za mbu in promptuu pale Davos 2005, akasema na 'President Mkapa needs help today'.

Scroll hadi dakika ya 52

Ukitaka kuona hapa;
Mkapa Begging For Money For Poor Tanzania

Angalia Mkapa anavyochekelea. Sasa wewe mtu mwenye roho nzuri kama Mkapa anaweza akaweka hela nje ya Tanzania? What evidence do you have otherwise?

Ina maana kadanganya hadi mrembo Sharon Stone?
Kuna watu wanatoa pesa zao kwa roho nzuri, sasa wakijua ziko diverted? Huyu huyu Sharon Stone katoa mpya juzi kuhusu China. Je kibao kikigeuziwa bongo na Africa?

Kama una evidence mimi nitaenda pale Parliament Square nipige rent free camping (Conditions apply, offer stands only during summer time with bikinis passing by. Offer may be withdrawn without notice!!).
BrianHaw.jpg
 
Back
Top Bottom