Buswelu
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 1,998
- 355
Chenge aiponza BoT
na Waandishi Wetu
KUGUNDULIKA kwa akaunti ya mabilioni ya fedha inayohusishwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) katika benki moja katika visiwa vya Jersey, Uingereza, hivi karibuni, kunaonekana kuwashtua na kuwaamsha usingizini wabunge.
Hali hiyo ilidhihirika jana wakati wa semina ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ambapo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed aliitaka Benki Kuu (BoT) kutoa ufafanuzi wa sheria inayoruhusu wananchi kuweka fedha katika benki za nje.
Hata hivyo, swali hilo la Hamad Rashid kwa maofisa wa BoT waliokuwa wakiwaeleza wabunge kuhusu shughuli mbalimbali za taasisi hiyo, lilikosa majibu ya papo kwa papo.
Maofisa hao wa BoT waliwaomba wabunge kuwapa muda hadi leo hii ili waje kutoa majibu ya swali hilo, na mengine kadhaa yaliyoulizwa ambayo kimsingi yalihitaji majibu yaliyoandaliwa na yanayojitosheleza.
Hamad Rashid katika swali lake aliloliuliza pasipo kumtaja kwa jina Chenge, aliuliza iwapo sheria zilikuwa zikiruhusu watu binafsi kumiliki akaunti nje ya nchi.
Nataka kujua, je, sheria inaruhusu mtu kuweka fedha za kigeni nje ya nchi? alihoji Rashid na kuongeza kwamba hivi sasa imani ya Watanzania kwa BoT imeshuka kutokana na tuhuma za ufisadi zinazoikabili benki hiyo.
Ingawa hakuweka bayana, swali hilo lilionekana dhahiri kutoa mwelekeo unaomhusu Chenge ambaye hivi karibuni akaunti yake hiyo ya nje ya nchi ilikutwa ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja ambazo ni karibu shilingi bilioni 1.2.
Fedha hizo za Chenge ambazo uchunguzi wake unaendelea, ziligunduliwa na makachero wa kitengo cha uchunguzi wa makosa makubwa ya rushwa cha nchini Uingereza (SFO), wanaochunguza mkataba wa mauzo ya rada, yaliyofanywa kwa Serikali ya Tanzania na Kampuni ya BAe Systems ya nchini humo mwaka 2002.
Zaidi ya suala hilo, mbunge huyo alitaka pia kufahamu namna madini yanavyosaidia wachimbaji wadogo, huku akihoji msaada wa BoT kwa wamachinga, aliodai kuwa wanachangia asilimia 30 ya bajeti ya serikali.
Awali, Pantaleo Kessy wa BoT, aliyewasilisha mada ya sera na ubadilishanaji wa fedha za kigeni, alisema ipo sheria inayomzuia mtu kuweka fedha nje ya nchi.
Mbali na mbunge huyo, kamati pia imetaka kufahamishwa ukweli kuhusu kushuka kwa kiwango kikubwa kwa uchumi wa Tanzania na akiba ya fedha za kigeni zilizopo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Naibu Waziri wa Mipango na Fedha, Omari Mzee, alisema idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki bado ni ndogo.
Alisema kati ya Watanzania zaidi ya milioni 35, wanaotumia huduma hizo ni milioni 1.6 tu, sawa na chini ya asilimia tano ya watu wote waliopo nchini.
Kugundulika kwa fedha hizo za Chenge katika akaunti moja ya nje ya nchi, hatimaye kulimlazimisha mwanasiasa huyo ajiuzulu wadhifa aliokuwa akiushikilia wa Waziri wa Miundombinu.