Chenge Afanya Tena: Asimamisha Kesi ya Jinai Ili Afanye Shughuli Zake Kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge Afanya Tena: Asimamisha Kesi ya Jinai Ili Afanye Shughuli Zake Kwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tk, Jun 12, 2009.

 1. t

  tk JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bunge lakwamisha kesi ya Chenge
  Dar Leo – Alhamisi – Juni 11 2009
  Na Rehema Maigala, Kinondoni
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni leo imelazimika kuahirisha kesi inayomkabili Waziri wa zamani Wizara ya Miundombinu, Andrew Chenge kutokana na vikao vya Bunge vinavyoendelea Mkoani Dodoma.
  Mshitakiwa Chenge anashtakiwa pamoja na mwenzake Majid Ghalib (26), mbele ya HakimuEmilius Mchauro wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ambapo kesi yao imesomwa na Mwendesha Mashitaka David Mafwimbo.
  Akiahirisha kesi hiyo Hakimu Mchauro amesema kuwa, Mahakama imelazimika kuahirisha kesi hiyo kutokana na mshitakiwa Chenge kuiomba Mahakama ifanye hivyo kwakuwa anahudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma.
  Alisema kuwa mshitakiwa huyo ameomba pia apewe ruhusa baada ya kumaliza vikao hivyo aende nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.
  “Kutokana na sababu hizi nalazimika kuahirisha kesi hii hadi Agosti 13 mwaka huu” amesema Hakimu Mchauro.
  Mwendesha Mashitaka Mafwimbo awali amedai kuwa, mshitakiwa Chenge anashitakiwa kwa makosa manne ambapo mshitakiwa Ghalib Ghalib anadaiwa kutotunza kumbukumbu za mwajiri wake.
  Wakati mshitakiwa Chenge anadaiwa kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya Victoria George na Beatrice Costantino pia kuendesha gari bila ya bima ambao ni uendeshaji wa kizembewa gari na kusababisha uharibifu wa bajaji.
  Ajali hiyo ilitokea saa 10 alfajiri baada ya gari T 512 ACE Toyota Pick Up Hilux alilokuwa akiendesha Chenge kuigonga pikipiki aina ya Bajaji yenye namba za usajili T 736 AXE waliyokuwa wamepanda wanawake wawili waloikuwa wakitoka Maisha Club.
  Wanawake hao Victoria George na Beatrice Costantine walipoteza maisha muda mfupi kutokana na kuumia kichwani na kutokwa damu.
   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hivi kipi ni urgent? Haki au? Huwa nashangaa hekima ya hawa waheshimiwa mahakimu.
   
 3. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2009
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 915
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  kuomba ruhusu ni haki ya mshitakiwa,mbaya ni kutokuonekana mahakamani bila ya kutokutoa taharifa
   
 4. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,744
  Likes Received: 3,182
  Trophy Points: 280
  Lakini chenge, wewe una mungu wako binafsi kwani amekuahidi uhai milele. kweli ni haki kuhudhuria vikao au shughuli zozote kuliko kuwatendea haki marehemu. Kuwa na roho ya imani kidogo
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hakimu kaona aepushe beef kati yake, au judiciary, na Chenge, au hata legislature.Hapa yangekuja mambo ya precedent na influence etc.

  Chenge anaogopwa kiaina kwa influence yake, na kesi hii haijafika stage ya kupewa mijaji vichaa ile inayoangalia rule of law, kesi iko chini bado na vihakimu vinakumbuka huyu bwana juzi tu alikuwa AG, anaweza kupiga simu mbili tatu kesho keshokutwa mtu anapigwa transfer Newala huko aende kucheka na Simba mla watu.

  We unafikiri mambo yanavyoenda huko serikalini mchezo.

  Hakimu akiangalia grounds anazo.Chenge mbunge, kweli kuna kikao cha bunge muhimu.

  Akaona badala ya kununua beef kwa bei rahisi mwachie mzee mzima ajinafasi tu, kesi inamngoja.

  In all reality Chenge ana haki ya kuomba udhuru, tatizo si Chenge kupewa udhuru, tatizo wananchi wa kawaida huwa wanapigwa chini na hawapewi nafasi kama hizi hata kama wanaumwa.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Ni kweli watu wa kawaida huwa hata hawapewi nafasi hata kuhoji ayaaa yetu macho tunasubiria hizo episodes zijazo tuone mwisho wake....maana makosa yako wazi....ila najua itakuja kuwa fine tu....
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa China haya mambo ya Chenge yangeshasahaulika mda mrefu!! Angekuwa ameshapigwa risasi..kwa manufaa ya wengi!

  Mimi bado naona tunahitaji sheria za China kwa kama 10 yrs ili kuleta sanity na nidhamu ktk nchi yetu!
   
 8. t

  tk JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kuomba udhuru kwa mahakama ni jambo la kawaida lakini uwe udhuru wa kweli. Kwa mfano kama wewe umetenda kosa la jinai na ukafikishwa mahakamani, huwezi kuiomba mahakama iahirishe kesi kwa sababu eti upate muda wa kurudi kazini kwako ukamalizie kazi zako. Hiyo sijawahi kuisikia maishani. Kwa mtu wa kawaida utaonekana punguwani hata kuweka ombi kama hilo.

  Pili ugonjwa kweli ni dharura inayokubalika lakini nayo ina masharti yake. Ni lazima daktari atoe kwa maandishi kuwa siku ile ya kesi ni budi uwe hospitali kwa matibabu ili kuokoa maisha yako. Mfano wa karibu ni kama walivyofanya kwa Jeetu Patel alipotaka kwenda India, napo walimkatalia. Lakini katika issue hii, mgonjwa kwanza anakwenda kazini kwa mwezi mzima na nusu baada ya hapo ndio anakwenda kwa matibabu. Hiyo urgency ya ugonjwa iko wapi?

  Ili kuleta usawa kwa raia, ni lazima Jaji Mkuu aingilie swala hili ama sivyo akitoka SA kutakuwa na mikutano ya kamati za bunge, mara safari za wabunge etc, etc, Kwa kuwa hakimu kisha weka precedence itabidi wamkubalie. Mwisho wa yote kesi itakwisha kimya kimya.
   
 9. Mukuru

  Mukuru Member

  #9
  Jun 12, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni dhahiri TZ kuna sheria aina mbili......ya watu wa kawaida (wahishiwa) na ya vigogo (waheshimiwa). Suala la kesi ya Chenge ni kiini macho hivyo pamoja na ushahidi wa wazi kwa baadhi ya makosa aliyotenda (mfano la kuendesha gari isiyo na bima), ataishia kulipa faini. Kama alivyoimba Bushoke, wengi walio magerezani ni watu masikini!
   
 10. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tatizo si la Mh Chenge hata kidogo, tatizo ni sheria za nchi.
  Dhamana ya chenge ina masharti gani?.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jun 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  hivi ni watu wangapi ambao wana kesi zao mahakamani na kazi zao ambazo wanahitaji kuhudhuria vikao na mikutano mbalimbali?
   
 12. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  separation of power tanzania bado iko chini sana! Hakimu anamuogopa mbunge...hahaha! Kosa la jinai, mtu unakimbilia kwenye vikao bunge? its a joke and a mockery to the judiciary!
   
 13. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2009
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  It's only in Tanzania where this kind of stupidity is allowed to flourish. This is unheard of, the defendant is the one who is calling the shots.
   
 14. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Inawezekana kuna maelfu na maelfu ya watu wana kesi zao mahakamani na kazi zao ambazo wanahitaji kuhudhuria, lakini hapa kitu cha kuangalia ni masharti ya dhamana aliyowekewa mwenye kesi yanasemaje?. Kesi hazifanani, hivyo na masharti ya dhamana hayafanani. Angalia masharti ya dhamana ya chenge yanasemaje?
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwani ditopile yuko wapi?? chenge asubiri kidogo
   
 16. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  huyu mtu kwa tuhuma zake zote hizo hakutakiwa kuwa mbunge mpaka leo.alitakiwa ajiuzulu.na sheria pia kweli.
   
 17. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Na wabunge nao wangemwimbia kale ka wimbo ka zamani tulikofundishwa shuleni,,,
  Paulo usijekucheza na sisi una mikono mchaaaaaaaaaaaaaaaafu.
   
 18. t

  tk JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa kawaida masharti ya dhamana huwekwa kuhakikisha kuwa mshitakiwa anapohitajika mahakamani anapatikana na akikosa dhamana yake hufutwa na mali ziliziomdhamini kuchukuliwa na waliomdhamini kutiwa hatiani wakati huo huo mshitakiwa anaendelea kutafutwa.

  Kuhusu kuahirishwa kwa kesi, huku hakuhusiani kabisa na masharti ya dhamana bali uendeshaji wa kesi. Kwani haiwezekani iwekwe katika masharti ya dhamana kuwa ikiwa utakuwa na kazi nyingi basi kesi yako itaahirishwa!
   
 19. Mukuru

  Mukuru Member

  #19
  Jun 14, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninavyofahamu mtumishi wa umma kama una kesi mahamakani unasimamishwa kazi na kulipwa nusu mshahara hadi hapo kesi yako itakapomalizika. Inawezekana masharti ya kazi ni tofauti kwa wabunge....mwenye ufahamu naomba anisaidie kwa nini mpaka leo Chenge na wengineo wenye ajira za serikali wanaendelea kufanya kazi wakiwa na kesi mahamakani?
   
Loading...