Chenge aandaliwa mashitaka ya rada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge aandaliwa mashitaka ya rada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 1, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,608
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  Chenge aandaliwa mashitaka ya rada

  Mwandishi Wetu Aprili 1, 2009

  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo


  Adokezwa aandae wadhamini wake

  Lengo ni kumuepusha asiende lupango


  BAADA ya kupandishwa kizimbani kwa kesi ya kusababisha ajali iliyoua watu wawili, Mwanasheria Mkuu wa zamani wa serikali Andrew Chenge, sasa anatarajiwa kufunguliwa mashitaka kuhusiana na tuhuma za rushwa katika ununuzi wa rada ya kijeshi yenye thamani Sh bilioni 40 inayomkabili na vigogo wenzake kadhaa, imefahamika.

  Habari za uhakika zimeeleza kwamba, pamoja na kuwapo juhudi kubwa za kuzuia mashitaka dhidi ya wahusika wakuu wa sakata hilo linaloigusa kwa karibu serikali ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kesi hiyo itafunguliwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa kutokana na msukumo mkubwa wa kisiasa.

  Rada hiyo ya kijeshi iliyonunuliwa kwa Pauni za Uingereza milioni 28 , iliibua utata mkubwa lakini kasi kubwa iliongezeka baada ya makachero wa uingereza wa kitengo cha Serious Fraud Office (SFO) kubaini kuwapo kwa rushwa kubwa iliyohusisha kampuni ya Uingereza ya BAE System na wanasiasa, watendaji na wafanyabiashara wa Tanzania.

  "Hakuna kitakachozuia kushitakiwa kwa watuhumiwa wa sakata la rada akiwamo Chenge kwa kuwa kuna kila aina ya ushahidi, pamoja na kuwapo kwa vikwazo kadhaa. Wenzetu wa SFO wanafanya kazi kwa maslahi yao zaidi na hapa nyumbani kuna wanaojaribu kuwasaidia watuhumiwa, lakini ni suala la wakati tu kwa sasa," kinaeleza chanzo chetu karibu na serikali.

  Chanzo hicho kiligusia kuwapo kwa ukabila katika kulindana kutokana na kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Elieza Feleshi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hosea kutoka sehemu moja na Chenge, lakini wote wamekwisha kukanusha kupitia gazeti moja la kila wiki (si Raia Mwema) kufanya kazi kwa ukabila.

  Awali ilielezwa kwamba mwishoni mwa wiki, Chenge alijulishwa kuhusiana na maandalizi ya kesi dhidi yake, akihusishwa na rushwa ili aweze kuandaa wadhamini, lakini taarifa hizo zimekanushwa vikali na pande zote zinazohusika wakiwamo watu walio karibu na mwanasiasa huyo ambaye amekuwa gumzo kwa muda mrefu sasa kutokana na kuhusishwa kwake na sakata hilo.


  Tayari imethibitishwa pasi shaka kwamba Watanzania wane wazito wametajwa kuwa watuhumiwa wakuu wa sakata la rada, huku nyuma yao kukiwa na watendaji kadhaa wa idara na asasi nyingine za serikali walioshiriki katika mchakato huo kabla na wakati wa ununuzi wake.

  Waliotajwa moja kwa moja na nyaraka rasmi pamoja na Chenge yumo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk. Idriss Rashidi, ambaye wakati wa mchakato huo alikuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kabla ya kustaafu na kuingia katika sekta binafsi.

  Baada ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Mkapa kwa miaka kumi, mwaka 2005 Chenge aliwania ubunge jimbo la Bariadi Magharibi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuteuliwa kuwa Waziri wa Afrika Mashariki kabla ya kuhamishiwa wizara ya Miundombinu, ambako alilazimika kujiuzulu kutokana na kashfa ya rada.

  Chenge alilazimika kujiuzulu nafasi yake baada ya kutajwa hadharani kuhusika kwake na ununuzi wa rada na kubainika kumiliki akaunti nje ya nchi yenye kiasi kikubwa cha fedha ambazo yeye aliziita kuwa ni ‘vijisenti.'

  Kwa upande wake, Dk. Rashidi, baada ya kuondoka BoT mwaka 1998, aliingia katika sekta binafsi ikiwamo benki ya Akiba Commercial, Vodacom Tanzania na benki ya NMB kabla ya kuteuliwa tena kuongoza Tanesco aliko hadi sasa.

  Watuhumiwa wengine wawili wakuu waliotajwa ni pamoja na mtuhumiwa mkuu ambaye kwa sasa amekimbilia nje ya nchi Shailesh Pragji Vithlani na mshirika wake mkuu kibiashara Tanil Somaiya.

  Chenge, Dk. Rashidi, Vithlani na Somaiya wote wametajwa kuwa washiriki wakuu waliowaongozwa wengine katika kufanikisha biashara hiyo tata kwa upande wa Tanzania kila mmoja kwa sasa amekwisha kuchunguzwa kuhusiana na suala hilo.


  Wakati Chenge alishiriki kwa kiasi kikubwa kama Mtaalamu wa sheria, Dk. Rashidi ametajwa kushiriki kama mtaalamu na mhusika mkuu wa mambo ya fedha akiwa Gavana wa BoT.

  Taarifa zinaonesha kwamba Vithlani na Somaiya walikuwa na hati za kiapo zenye kuwapa mamlaka ya kisheria kuwakilisha kampuni iitwayo Envers Trading Corporation.

  Uchunguzi unaonyesha kwamba Envers Trading ililipwa dola za Marekani milioni 12 na kampuni nyingine iitwayo Red Diamond Trading, iliyofunguliwa mwaka 1998 katika visiwa vya Virgin ambavyo ni sehemu ya dola ya Uingereza.

  Red Diamond Trading ilikuwa na uhusiano mkubwa na kampuni iitwayo BAE Systems, ambayo ilitengeneza na kuuza rada iliyouziwa serikali ya Mkapa mwaka 2002.

  Imedaiwa kwamba Red Diamond iliweza kujinufaisha kwa kutumia mianya ya kisheria katika visiwa vidogo vya Caribbean ambako kampuni kama hiyo zinaweza kuficha taswira ya akaunti zake benki ikiwa ni pamoja na majina ya wamiliki wake.

  Akihojiwa na wapelelezi wa Uingereza, Somaiya, ambaye anamiliki kampuni ya Shivacom ya mjini Dar es Salaam, alikiri kuwa na hati zao za kiapo zenye kuwapa mamlaka ya kisheria kuwakilisha kampuni iitwayo Envers Trading Corporation kwa miezi 11.

  Somaiya alikiri katika mahojiano hayo kwamba yeye na "rafiki yake mkubwa" Vithlani wanamiliki kwa pamoja kampuni iitwayo Merlin International.

  Hata hivyo, nyaraka za SFO zinaonyesha kwamba Somaiya kupitia kwa wakili wake aliiambia Takukuru kwamba aliacha kuwa mwenye hisa na mkurugenzi wa Merlin International kipindi ambacho tayari biashara ya rada ilikuwa imekwisha kamilika.

  Kwa sasa Vithlani pekee ndiye anayetafutwa na ameshitakiwa kwa kutoa taarifa za uongo kuwa sio mmiliki wa Envers Trading na kuhusu kupokea dola 390,000 kwa biashara ya rada wakati ukweli ni kwamba alilipwa kitita cha dola milioni 12.

  Tayari makachero wa Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Mazito ya Uingereza (Serious Fraud Office-SFO) wamekwisha kuomba ushirikiano wa wenzao wa Tanzania katika kuwahoji na kuwapekua watuhumiwa wakuu wa sakata hilo.

  Tayari SFO kwa kushirikiana na vyombo vya dola vya Tanzania, Uswisi na Ufaransa wamebaini kuwapo kwa Dola za Marekani milioni 12 (Sh. bilioni 13.8), ambazo zililipwa kwa siri kwa maofisa wa juu wa serikali kupitia Vithlani kama kamisheni, fedha zilizolipwa kupitia benki ya Uswisi.

  Imefahamika kwamba umepatikana ushahidi mzito wa kuthibitisha malipo yaliyofanywa na British Aerospace Engineering (BAE) kuwa ni hongo kwa wale waliopitisha ununuzi huo, malipo yaliyofanywa wakati wa utawala wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

  BAE ilifanya mipango miwili tofauti na Vithlani ambapo kwanza, makubaliano ilikuwa ni kusaini malipo ya kamisheni ya asilimia moja, baada ya kupitishwa kwa ununuzi wa rada wa Dola za Marekani milioni 40.

  Mwezi mmoja baada ya kupitishwa kwa ununuzi huo na serikali, BAE iliilipa kampuni ya Merlin International Ltd hapa nchini, jumla ya Dola za Marekani 400,000.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dr. Rashid tumbo joto, afadhali Chenge kaanza kuzoea kufikishwa mahakamani (kesi ya kugonga watu na kuua). Hivi huyu Somaiya ndio alikuwa na kesi Kenya na imeripotiwa katorokea India?, manake huyo Somaiya aliyetoroka wanasema alikuwa anahitajika pia Tanzania. Ukifisadi utaishi kwa mashaka siku zote, "mbio za sakafuni huishia ukingoni...".
   
 3. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sasa nafikiri wakati wa kusema kweli umefika, chenge najua hatukubali kushitakiwa peke yake, Je Mkapa atatjwa kwenye hii kashifa kama mwanzo wa kutajwa kila sehemu anapohusika.

  Huwezi kuwatenganisha Mkapa na Chenge hata kidogo, kama chenge atashitakiwa basi Mkapa ajiandae vinginevyo moto utawaka
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,608
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  Mie bado naamini huu ni usanii tu wa kuelekea 2010 siku zote hizi walikuwa wapi? Pia kabla ya kuwashtaki wazirudishe pesa zilizo kwenye bank accounts za nje za Chenge na Idrissa huko hazina haraka iwezekanavyo.
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kuna wakati wa kula huku umezungukwa na harufu nzuri za misosi na kuna wakati wa ulichokula kukutoka.
  Mbaya ni pale kikutokapo kupitia mdomoni na puani baada ya kukaa tumboni kwa muda wa kutosha.
  Nchi zetu bado changa sana kujua madhara yote ya kuiba fedha za wananchi.

  Sisi tuliambiwa tutakula Nyasi, wao watanyea debe.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu BAK,

  Mbona kila siku nawaambia kuwa hii ni michezo ya kuigiza? Hata wakipelekwa mahakama hatafungwa mtu. Siku ikitokea hivyo labda JK awe ametupwa nje ya Ikulu. Na afadhali mzee wa watu Dr Salimu aliukosa urais. Sijui angefanyaje na haya madudu!
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kabla onyesho halijaanza ni lazima kuandaa jukwaa.
  Jukwaa linaandaliwa.
  Onyesho likianza hakuna kurudi nyuma.

  Vita kali ya kukatilia mbali tabaka tawala siku zote huanza wakati wa Amani.
  Wakati wa Amani Tabaka tawala hudhani Amani ndiyo mlinzi wao mwaminifu.
  Ukianzisha Vita ya namna hiyo wakati wa Machafuko hutofanikiwa kwani wanatabaka watakuwa macho wakikusubiri.
   
 8. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  watu wa mkapa wanakamatwa sasa hivi ,
  je watu wa kikwete (RA,EL) watakamatwa baada ya kikwete kutoka madarakani
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Jamani BAK hii haikuwa habari kwa ajili ya Fools Day??? Huwa najihadhari kupeleka kitu makini cha kweli kwenye media siku ya FOOLS. Sasa tuhakikishie kama hii habari ya jana 1st April si ya Fools. Aotherwise, kama ni kweli hi hatua njuri japo always ni mass attraction but matokea zero.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,460
  Trophy Points: 280
  Wana JF, niliwahi kusema huko nyuma, serikali inakurupukia mahakamani ili kujenga cheap popularity na watu, lakini baadhi ya kesi zenyewe, hazina legal merit. hata hiyo kesi ya vithlani is nothing. hii kesi ya radar is anoher nothing. Naomba muamini msiamini, hawana cha kufikisha mahakamani.
  Uthibitisho kama kagoda kaanzisha kampuni hewa, kalamba bilioni 40. akaifuta hiyo kampuni, hivyo kagoda is non existance hakuna wa kumshitaki. lakini zile fedha, yaani hizo bilioni 40, ziliingizwa kwenye accounts za watu na makampuni ya ukweli. kama hili la wazi limeshindikana, litakuwa hili la ada ambalo ni la siri.
  Chenge fedha ni zake. bila link zimetokaje BAE zikamfikia, then its nothing na hakuna kesi yoyote, labda serikali iifungue tuu ili kuongeza kura za 2010.
   
 11. c

  catimwa New Member

  #11
  Apr 2, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijaelewa vizuri mchakato mzima wa unuzi wa rada mwaka 2002, je mwaweza kunisaiia utaratibu uliotakiwa kufuatwa ili chenge na wenzanke wasiwe watuhumiwa?
   
 12. c

  catimwa New Member

  #12
  Apr 2, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  expected procurement officer
   
 13. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninachojua mimi ni kuwa hii kesi inachunguzwa na waingereza wenyewe na ndio drivers (kama sivyo naomba nisahihishwe) otherwise ingeshatupiliwa mbali na kusahaulika siku nyingi au basi imeisha. At any point JK hana credits za kujipa kwenye hili maana hata baada ya evidence zote hizo hajamchukulia hatua zozote za kinidhamu. Hata kama uchunguzi bado unaendelea, sababu hiyo hiyo iliyomtoa kwenye uwaziri ilitakiwa kumtoa kwenye uongozi mwingine wowote, sio kwa hiari, bali mkuu wake kushupaa. This never and will never happen.

  Sina hakika though kwamba hawa washtakiwa wakitakiwa mahakamani kesi zitaendeshwa kwa sheria na vyombo gani - JK na wafuasi wake watakuwa na influence gani for Chenge, maana hao waingereza watakuwa wanaifuatilia pia. Ninachojua pia ni kwamba ukitaka kumwona mtanzania alivyo mchapa kazi, mpe bosi wa kizungu!
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,608
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  Mkuu DC, ahsante sana Mkuu. Kauli yako ni kweli kabisa maana hakuna dalili zozote za kupandishwa kizimbani fisadi Chenge alias Mzee wa Vijisenti labda ni mmoja wa wale ambao 'nchi itawaka moto' kama wakipandishwa kizimbani. Kweli CCM imeshika 'utamu'
   
 15. C

  Chief JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Na kesi ya akina Lukaza imeishia wapi? Haitajwi siku hizi. Hizi kesi zote kwei ni usanii mtupu.
   
 16. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tuchukulie kwamba majambazi yameanzisha kampuni ya ulinzi, yakaajiri vijana na kuwafanyisha mazoezi, kisha kwenda kuvamia benki na kuiba na hatimaye kuifuta kampuni. Kwa hiyo logic yako hiyo then hakuna wa kumshtaki kwasababu kampuni ni non-existance.

  Hiyo argument yako huwa inatumika sana siku hizi. Mimi sio mwanasheria, lakini hainiingii akilini. Kama wewe ni muhasibu na kwa makusudi ukaisaidia kampuni yako kuiba, then nadhani wewe binafsi sio shahidi tu bali ni mshiriki kamilifu wa wizi huo. Hata kama ulitumwa na bosi wako ukaibe.

  Kufanya kazi kwa niaba ya kampuni hakukupi wewe immunity ya kuvunja sheria za nchi. Tena kwa maslahi yako binafsi. Ingekuwa hivyo mbona kila mwizi duniani angekuwa anaunda kampuni ambayo anaivunja baada ya wizi kufanyika.

  Na nadhani hilo la linki ya pesa zilizoenda kwenye hiyo account ya Chenge umeliona mikoni chini miguu juu. Sio kwamba walianza na account ya Chenge na kuanza kushangaa fedha hizo zimetoka wapi. Ni kwamba walikutana na account ya Chenge wakati wana-trace fedha za rada zilienda wapi. Kwa hiyo hakuna linki ya kutafuta. I stand to be corrected.
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi hamjabaini tu kuwa habari yenyewe ni ya April 1
   
 18. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Yes it was april fools, ndio maana hajapandishwa kizimbani mpaka leo.
   
 19. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Fresh mystery on Chenge`s billions
  By Guardian on sunday team  23rd August 2009


  [​IMG]
  Email  [​IMG]
  Print  [​IMG]
  Comments
  [​IMG]
  Andrew John Chenge  The source of Andrew John Chenge's $1.5million(Sh2.1bilion) found in his offshore bank account in Jersey, last year, remains a mystery as local investigators failed to connect the dots on whether the billions are part of the radar's kickback pays amounting to $12million. But, as the mystery about the source of Chenge's billions deepens, the UK's Serious
  Fraud Office (SFO) still strongly believes that $1.5million (Sh2.1billion) found in the offshore bank account of Tanzania's former Attorney General and Cabinet minister last year, is part of the radar's kickback pays.

  The fresh twist on the source of the money sharpens the contradiction between the two credible institutions currently investigating the radar scam – SFO and the local Prevention and Prevention of Corruption Bureau (PCCB).
  By-products of the contradiction include deeper controversy, wider mystery and bigger confusion over who actually pocketed the huge kickback pays from radar paymaster Sailesh Vithlani.

  According to a reliable source within the PCCB, the anti-graft agency has failed to establish whether the Chenge billions are part of the radar's kickback pays or not. The move cast a bleak a future on the much-awaited case that has drawn public attention since the revelation that the UK's BAE System paid a total of $12million to Vithlani.

  "We haven't received any credible evidence linking Chenge's billions to the radar deal…but that doesn't mean it is the end of the road, "a senior official of the PCCB investigation team told The Guardian on Sunday under conditions of anonymity.

  "His file is still pending as we try to tie the dots together, but so far , we haven't found a direct link of his billions to the radar kickback payments."
  But contacted on Friday, the SFO official close to the investigation emphatically maintained that "there's clear evidence that the billions are part of the radar's deal until proven otherwise."

  Speaking to The Guardian on Sunday over the phone, the SFO official who earnestly requested anonymity said, "What you are telling me is news to me…we have every clear evidence to prove that this was part of the radar deal; but if someone claims that there's no link then he should wait for our final report."

  SFO version

  In March last year, UK investigators probing the controversial $40m BAE radar deal claimed that ex-Infrastructure Minister Cheyo received $1.5m (2.1bn/-) in kickbacks from the deal through a slush fund he set up in the UK island of Jersey.

  According to SFO's draft, Chenge received payments through six credit transfers between June 19, 1997, and April 17, 1998, while he was serving as Attorney General.

  The SFO draft further claimed that, the monies were paid to account No.59662999 owned by Franton Investment Limited through Bank Code No 204505 of Barclays Bank Plc. The SFO proved beyond reasonable doubt that Chenge owns Franton Investment- a registered company that appears to have been established primarily to facilitate the transfer of the money.
  According to information provided by the Jersey Authority, the $1.5m was transferred from a Frankfurt branch of Barclays Bank to Chenge's account at a Jersey branch.

  Chenge resigned last year after the SFO's revelations that he had $1.5m in his offshore bank account suspected to have been obtained from the $12m payoff that broker Sailesh Vithlani took from BAE System, the UK's biggest arms supplier.

  He is alleged to have told his banker that the $1.5m was professional earnings from his work as a lawyer, but later contradicted himself, saying the money was a combination of inheritance and family savings, adding that 25 percent of the money belonged to his wife.

  The SFO believes that Vithlani had made payments to Tanzanian public officials in a position of influence in the BAE System contract negotiations, in which he brokered the purchase of military radar at an inflated price and skimmed a cut for himself and those who aided him in committing the crime.

  UK investigators also believe that Chenge was one of the top people to receive a payoff from Vithlani because without the AG's agreement, the financing package for the radar could not have gone through.

  The AG's office under Chenge was required to comment on and approve the financing package to purchase the radar deal, for which Tanzania was forced to borrow from the Barclays Bank Plc. The $12m back-door payment to Vithlani, Chenge and others, represented 30 percent of the contract value.

  In the wake of the saga, Chege shocked the public by casually remarking that the money in question was "vijisenti", which loosely translates as "peanuts".
  SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY


  My Take: Corruption On Top of Corruption..!! Tanzania..!!!
   
 20. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  zile pesa ni za meremeta siyo rada, hapo Chenge kishashinda kiulaini tu. Unajua kwanini? kwasababu hawataki kuifunua meremeta, mambo ni funika kikombe mwanaharamu apite.
   
Loading...