'Chenga' ya Lissu yawachanganya 'walimpania' kuvuruga mapokezi yake, wapangua mipango yao kwa taabu kubwa

Sijawahi kumwona mhaya akiwa na akili ya kipuuzi kama wewe
Wewe nae1 sisi tulijua hawezi kuja, na ninakuhakikishia hata baada ya hizo tarehe hatakuja kama mnavyofikiria. Chezea ndevu sio serikali.
 
Tatizo lenu nyinyi vijakazi wa chakubanga mnadhani kila mpinga ccm yupo nje ya ccm.

Mnajidanganya sana wengine wapo ndani ya chama tena wana nafasi kubwa sana
Hata chenga hii pia ufipa wanaingia chaka...hii uliyowapiga ni chenga ya mwili. Endelea kujikita ndani ya kiini chao, utatuletea taarifa zao. Unafanya kazi nzuri kuwafanya wakuamini.
 
Hizo Serikali ni ngapi zilianguka!!!? Kama Napolion alianguka, naye Hitler na mwenzi wake Mussolini wakafa kama mende, unatamba nini Sasa!!? Mhe. Lisu atarudi nchini mwake, na Mungu aliyemwokoa na risasi 38 hajafa, Yu hai milele na milele.
Itakayoanguka ni hiyo serikali yako ya kikatili iwapo itaendelea na mipango yake miovu dhidi ya raia wema mfano wa Lisu. Mungu Mwenyezi aliyemwokoa Lisu, ameipa onyo hiyo Serikali, na kama itazidisha kiburi, iwe tayari kuikabili hasira ya YAHWE.!!!
Ukiwa dreva wa basi, ni bora ugonge mmoja barabarani kuliko kumkwepa ukahatarisha maisha ya abiria wote ndani ya basi. Busara zinaelekeza hivyo.
 
Wewe inaonekana kwenu ni kule kikukwe wanapo kula nyama za watu
Ukiwa dreva wa basi, ni bora ugonge mmoja barabarani kuliko kumkwepa ukahatarisha maisha ya abiria wote ndani ya basi. Busara zinaelekeza hivyo.
 
Makao Mkuu ya CCM Dodoma kulizizima na kusheheni mipango ya viwango mbalimbali juu ya ujio wa Mwanasiasa Tundu Lissu aliyetarajia kurejea nchini Jumamosi ijayo, Septemba 7 mwaka huu. Ilipangwa mipango ya 'kuharibu' na 'kufifisha' mapokezi yake Uwanja wa Ndege Dar es Salaam kupitia makada wa CCM. ZILIPISHANA nyaraka za haraka na maagizo yenye vibwagizo kuhusu jambo hilo.

Makada wa CCM walipanga kuwasilisha barua leo POLISI kuomba kibali cha maandamano ya amani ya tarehe 7 Septemba mwaka huu kuunga mkono juhudi za Mawakili wa Serikali kuipambania ndege yetu inayoshikiliwa kwa amri ya Mahakama huko nchini Afrika ya Kusini. Kuwasilishwa kwa maombi hayo POLISI kungepelekea kupigwa marufuku maandamano na mkusanyiko wowote ule tarehe hiyo na nyingine kwa sababu za kiintelijensia.

Makada walijipanga kukubaliana na uamuzi wa POLISI haraka ikiwa na baraka na kujitokez kusisistiza umuhimu wa kutii sheria na maelekezo ya POLISI bila shuruti, baruti wala mashuti. Makada wangejiandaa kuona jinsi 'wapokeaji' wa Lissu wangesambaratishwa kwa Ilani ya POLISI na hivyo wao kukenua kwa furaha isiyo na karaha. Mipango ilipangika barabara.

Jana, akihojiwa na BBC, Lissu alisema kuwa safari yake ya kurejea nchini iliyokuwa ifanyike tarehe 7 Septemba mwaka huu haitawezekana kwakuwa Daktari wake amesema anahitaji kumuona tarehe 1/10/2019 na 18/10/2019 na hivyo safari yake itakuwa baada ya hapo. Kutokana na ahirisho hilo la safari ya Lissu, 'waliopania kuvuruga mapokezi yake' wamelazimika kupangua mipango yao kwa tabu na aibu kubwa.

Kila mpango mpya utakaosukwa utaanikwa hapahapa JF!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (Dodoma, Tanzania)
Kamanda umenistua!
Kwani ile kesi tuliyokuwa tunaiombea washindwe WAMESHINDA?
 
Back
Top Bottom