VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Makao Mkuu ya CCM Dodoma kulizizima na kusheheni mipango ya viwango mbalimbali juu ya ujio wa Mwanasiasa Tundu Lissu aliyetarajia kurejea nchini Jumamosi ijayo, Septemba 7 mwaka huu. Ilipangwa mipango ya 'kuharibu' na 'kufifisha' mapokezi yake Uwanja wa Ndege Dar es Salaam kupitia makada wa CCM. ZILIPISHANA nyaraka za haraka na maagizo yenye vibwagizo kuhusu jambo hilo.
Makada wa CCM walipanga kuwasilisha barua leo POLISI kuomba kibali cha maandamano ya amani ya tarehe 7 Septemba mwaka huu kuunga mkono juhudi za Mawakili wa Serikali kuipambania ndege yetu inayoshikiliwa kwa amri ya Mahakama huko nchini Afrika ya Kusini. Kuwasilishwa kwa maombi hayo POLISI kungepelekea kupigwa marufuku maandamano na mkusanyiko wowote ule tarehe hiyo na nyingine kwa sababu za kiintelijensia.
Makada walijipanga kukubaliana na uamuzi wa POLISI haraka ikiwa na baraka na kujitokez kusisistiza umuhimu wa kutii sheria na maelekezo ya POLISI bila shuruti, baruti wala mashuti. Makada wangejiandaa kuona jinsi 'wapokeaji' wa Lissu wangesambaratishwa kwa Ilani ya POLISI na hivyo wao kukenua kwa furaha isiyo na karaha. Mipango ilipangika barabara.
Jana, akihojiwa na BBC, Lissu alisema kuwa safari yake ya kurejea nchini iliyokuwa ifanyike tarehe 7 Septemba mwaka huu haitawezekana kwakuwa Daktari wake amesema anahitaji kumuona tarehe 1/10/2019 na 18/10/2019 na hivyo safari yake itakuwa baada ya hapo. Kutokana na ahirisho hilo la safari ya Lissu, 'waliopania kuvuruga mapokezi yake' wamelazimika kupangua mipango yao kwa tabu na aibu kubwa.
Kila mpango mpya utakaosukwa utaanikwa hapahapa JF!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (Dodoma, Tanzania)