Elections 2010 Chemsha mbongo-jubu maswali yote kwa ufasaha na umakini

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Chemsha bongo

Wandugu nimetumiwa maswali yafuatayo na jamaa yangu mmoja ili nimsaidie lakini binafsi yamenishinda, nadhani atakuwa kapewa asignment katika hii kozi fupi ya maandalizi ya uchaguzi. Plz mchango wenu utanisaidia kumjibu.

1. Ni rais gani duniani anayeamini kwamba kukaa madarakani miaka mitano ni kujifunza ili baadaye ukipewa fursa ya miaka mingine tena aweze kuwa mfanisi?

2.Rais wa kwanza Duniani kuwa na rekodi ya kuanguka anguka mbele ya kadamnasi ni

3.Ni Rais gani duniani anaye amini kwamba suala la urais ni la kifamilia zaidi na siyo la kitaifa?

4.Rais wa kwanza duniani kutamka hadharani kwamba hajui umaskini wa watu
wake unatokana na nini, ni................


5. Rais wa kwanza anaechukulia wingi wa magari kama kipimo cha maisha
bora! ni.............

6. Rais wa kwanza duniani anaepata ulinzi wa nguvu za Giza.(mnajimu) ni..........

7. Rais wa kwanza Duniani aliyesema watoto wadogo wa shule kupata mimba ni
kiherehere chao ni...........

8. Rais wa kwanza anayeogopa kuwaburuza mahakamani mafisadi ila ana uwezo mkubwa wa kumuwekea fitina mwizi wa mke wa mtu ni.........

9.Rais wa kwanza duniani aliyetumia 60% ya mabango yote ya biashara nchini
kwake kujinadi wakati wa kampeni ni..........

10. Ni Rais gani Duniani ambaye kwa mtazamo wake anahisi kafanya kazi kubwa nchini kwake kiasi cha kujisikia fahari kubwa kumuandaa mwanaye ili naye siku moja afuate nyayo zake...............

11. Rais wa kwanza Africa kudanganywa vibaya mno na wasaidizi wake ni........

12. Rais wa kwanza kusini mwa jangwa la sahara kufanya safari nyingi za nje ya nchi ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakaini ni..............

13. Ni rais gani duniani ambaye akiwa madarakani ndani ya miaka mitatu kaoa mabint wawili wenye umri sawa na wanawe, lakini hapendi ifahamike japo dini yake ina mruhusu?

14. Ni rahisi gani Duniani ambaye anaamini katika utawala wa sheria na amesaini sheria ya uchaguzi wa Taifa lake, kwa bahati mbaya amekuwa wa kwanza kuzikiuka
 
Mh! hata mii sijui, ila mimi nashangaa hao waliomchagua huyo raisi had akawa raisi wao!! Nawashauri wakipata tena nafasi ya kuchagua huyo wala wasimfikirie, watumie kura zao vyema kuwapa raisi atakae wasaidia kuleta mabadiliko. Kama ingekua mimi mfano kwa sasa kwa kua tanzania tunaelekea katik uchaguzi nitamchagua Dr Slaa. Nawashauri nanyi mfanye hivyo.
 
Back
Top Bottom