Marashi
JF-Expert Member
- Apr 14, 2018
- 2,774
- 4,269
Jarida la The Economist limeeleza kwamba tafiti zimeonesha watoto wanaozaliwa kwa njia ya kawaida huwa na kinga imara zaidi ya watoto waliozaliwa kwa njia ya upasuaji.
Utafiti umebaini kwamba mtoto anapozaliwa kwa njia ya kawaida hukumbana na kinyesi cha mama wakati wa hekaheka za kuzaliwa na kupelekea kumeza baadhi ya chembechembe za kinyesi cha mama na hiyo humsaidia kuimarisha kinga ya mwili kutokana na bakteria za kinyesi cha mama.
Kupitia utafiti huo wataalam wameeleza kwamba hata walipojaribu kumlisha kinyesi cha mama mtoto aliyezaliwa kwa upasuaji bado kinga yake haikuimarika ukilinganisha na mtoto aliyejilia mwenyewe chembechembe za mavi 'labour'.
Jambo hili linaukweli kiasi gani au ni propaganda za mabeberu tuzipuuze?