Chemba: Washukiwa watatu wa ujambazi wauawa na wananchi wenye hasira kali

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Watuhumiwa watatu wa ujambazi wameuawa kwa kushambuliwa na wananchi wa kijiji cha Maziwa wilayani Chemba mkoani Dodoma mara baada ya kumvamia mmoja wa wafanyabiashara wa kijiji hicho na kufyatua risasi hewani kisha kumnyang'anya fedha takribani shilingi milioni moja za mauzo ya duka ambapo wananchi walifanikiwa kuendesha msako na kuwashambulia.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Gilles Muroto amesema watuhumiwa hao wa ujambazi walikutwa pia na bunduki aina ya Short Gun iliyotengenezwa kienyeji.

Katika tukio lingine kamanda Muroto amesema wamewakamata vijana wanne wakiwa na noti bandia zipatazo 3181 zote za dola mia ambapo amesema uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea ili kuwakamata watuhumiwa wengine waliohusika katika kutengeneza noti hizo.

Aidha katika hatua nyingine msemaji wa jeshi la polisi nchini ACP Barnabas Mwakalukwa ametoa taarifa kwa umma juu ya kifo cha aliyewahi kuwa mkuu wa jeshi hilo nchini Samweli Pindugu aliyefariki dunia jijini Dar es Salaam.

ITV
 
Kila siku tunazungumzia kitu kimoja tu picha mkuu habari kama hii bila picha kweli.
 
sasa mtu unakuwa na dola noti feki uzipeleke wapi kama sio kujilipua huko.. bora zingekuwa Tsh unaweza kutumia mtaani na watu wasishtuke
 
Back
Top Bottom