Chelsea yaichapa AC Milan 5-0

mwanaizaya

Senior Member
Apr 26, 2008
133
1
Chelsea yaichapa AC Milan 5-0

Moscow, Russia

NICOLAS Anelka amejiweka katika nafqsi nzuri ya kuwa miongini mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha kocha Phil Scolari wa Chelsea baada kufanya mapinduzi makubwa na kuiangamiza AC Milan.

Mfaransa huyo alifunga mabao zaidi dakika ya 58 tangu kujiunga na timu hiyo miezi sita iliyopita.

Hivi sasa Scolari amesisitiza kwamba mshambuliaji huyo aliyenyakuliwa kwa kitita cha pauni milioni 15, atakuwa tegemeo msimu ujao kutokana na kumvutia Mbrazil huyo.

Anelka aliwafunga m,abingwa wa zamani wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mabao manne kati ya matanbo.

Scolari alisema: “Uwezo huu ni muhimu kwa Anelka lakini hata kwangu na mashabiki kuwa na imani naye.

“Ni kitu cha kufurahisha kujitumana na kufunga mabao manne dhidi ya AC Milan. Sasa atajiamini na wachezaji wenzake watamwamini pia. Nilimweleza kwamba, ninataka acheze katikati, siyo nyuma kulia ama kushoto kama ilivyokuwa msimu uliopita.

“Ni muhimu sana, hivi sasa tuna mshambuliaji mmoja, Anelka.

“Nimempongeza kwa mabao yake lakini la muhimu kwangu ni kumwona akicheza kwa kiwango kizuri na kwa uhuru zaidi kuliko alivyocheza katika mechi zilizopita.”

Anelka aliifugia mabao Chelsea msimu uliopita tangu ajiunge nayo kwa kitita kikubwa akitokea Bolton, Januari.

Alianza kwa kuisumbua ngome ya wapinzani wake ambapo mlinda mlango Milan, Zeljko Kalac alikuwa na kazi ya ziada. Mchezaji wa zamani wa Leicester hataweza kuisahau Chelsea.

Alitumia dakika tatu kupata bao la kwanza. Mpira wa adhabu uliopigwa na Frank Lampard kutoka upande wa kushoto uliwakosa wote na kujaa wavuni pembeni ya mlinda mlango, Kalac.

Dakika tatu baadaye, mlinzi, Giuseppe Favalli alipiga mpira kichwa na kumkuta Anelka ambaye alifunmga bao la kwanza.

Wakati kocha wa Milan, Carlo Ancelotti akifikiria kwamba mpira uliopigwa hautaleta madhara, mlinda mlango, Kalac aliukosa mpira ambao ulipigwa na Anelka na kujaa wavuni.

Dakika mbili kipindi cha pili, washambuliaji wa Chelsea kwa ushirikiano wao walimwezesha Florent Malouda kufunga moja ya mabao ya timu hiyo.

Hakuna cha kushangaza, Scolari alipumua baada ya kikosi chake kufungwa kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Lokomotiv Moscow Ijumaa kuwa na furaha.

Aliongeza: “Matumaini ya mchezo wetu wa ufunguzi dhidi ya Portsmouth utakuwa mzuri. Lakini, ninaweza kusema nina asilimia 85 kwa timu yake kushinda.”
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom